Uaminifu

Uaminifu

Dinnah

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
791
Reaction score
1,062
Habari wakuu

Napenda nichukue nafasi hii kueleza nilicho jifunza siku ya Leo,huenda miongoni mwetu yupo atakaye guswa na somo hili

Nanukuu mafundisho

UAMINIFU
Kuna maana nyingi sana za uamifu,nitaziweka nilizo jifunza siku ya Leo,nawe kama unajua maana zaidi ya nilizoorodhesha hapa unaweza ongezea katika comment ili tuendelee kuongeza maarifa.

Maana za uaminifu

1_Ni kutekeleza jambo lolote kadri inavyo paswa kutekeleza.
2_kufanya jambo kikamilifu,vizuri na kwa uhakika bila kupindisha kama inavyopaswa.
3_ni neema ya MUNGU kwa watu wote waliookoka na wasiokoka
4_Ni tunda la roho ambalo kwa waliookoka ni lazima liwepo,maana usipo kuwa mwaminifu huna roho wa Mungu ndani yako.

Wagalatia 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo,furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,UAMINIFU.

Mf,ukiwa mwaminifu kazini unapandishwa cheo,ukiwa mwaminifu kwa Mungu unakusaidia kuendelea kiimani na kiroho

Kuna wakati watu wa kawaida wanachoka kuwa waaminifu,lakini wale waliookoka lazima wasichoke kuwa waaminifu sababu uaminifu ni tunda la roho lili ndani yao waliookoka

Nikizungumzia waliookoka ni wale walio kubali na kukiri kwa ulimi wao kwamba Yesu kristo ni BWANA na mwokozi wa maisha yao.

Luka 16:10-12
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana,huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia;na aliye dhalimu katika lililo dogo,huwa dhalimu katika lililo kubwa pia11Basi kama nyinyi hamkua waaminifu katika Mali ya udhalimu ni nani atakaye wapa amana ya kweli?12Na kama hamkuwa waaminifu katika Mali ya mtu mwingine,ni nani atakaye wapa iliyo wenu wenyewe?.

Hii inaonesha kwa namna gani tunapaswa kuwa waaminifu.
Mungu anataka tuwe waaminifu katika mambo yote,maana aliye mwaminifu katika jambo dogo huwa mwaminifu katika kubwa pia mf kuwa waaminifu katika
Kazi
Familia
Shughuli zetu za kila siku

lile jambo unalolidharau na kuliona dogo,usilidharau lifanye kwa uaminifu
Kuwa mwanifu katika
Ndoa
Kwa watoto wako
Kazini
Katika biashara
Kilimo
Mungu atakupandisha kutoka ngazi ya chini hadi ya juu
Hata wakati wa shida endelea kuwa mwaminifu soma mifano katika biblia mf wa ayubu alipata majaribu lakini alibaki kuwa mwaminifu mbele za Mungu.
Yusuph alipata shida lakini alibaki kuwa mwaminifu mbele za Mungu

Kumbuka jambo lolote usifanye kwa ajili ya binadamu,ili akuone,Fanya kwa ajili ya Mungu maana anatuona na anaona hadi yasirini yaliofichika ambayo mwanadamu hawezi kuona
Zaburi 12:1
BWANA,uokoe,maana mcha Mungu amekoma,maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
 
Frustrated mother.
Umeshajizehekea unataka mimeo awe mwaminifu umesahau kipindi kile ulivyokua unaringa na kubadilisha wanaume. kwendrah kule
 
Frustrated mother.
Umeshajizehekea unataka mimeo awe mwaminifu umesahau kipindi kile ulivyokua unaringa na kubadilisha wanaume. kwendrah kule
Mkuu umeelewa vizuri maada au unakurupuka tu
Jifunze kuheshimu maandiko hata kama hauheshimu watu
 
Hivi dada naomba niulize jambo. Kuokoka au Mlokole ni mtu wa namna gani?
Hakika jambo la Uaminifu limenitendea mengi mazuri
 
Hivi dada naomba niulize jambo. Kuokoka au Mlokole ni mtu wa namna gani?
Hakika jambo la Uaminifu limenitendea mengi mazuri
Ni somo lefu sana ndugu lakini ngoja nikueleweshe japo kwa ufupi

Jibu linapatikana katika

Warumi 10:9-10
9Kwasababu ukimkiri yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,UTAOKOKA 10Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata wokovu.

Bila shaka kwa neno hilo umeelewa walokole ni watu wa aina gani

Kuna Uzi upo umeandikwa kwa kina kuhusu kuokoka ngoja nikusogezee ndugu
 
Ni somo lefu sana ndugu lakini ngoja nikueleweshe japo kwa ufupi

Jibu linapatikana katika

Warumi 10:9-10
9Kwasababu ukimkiri yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,UTAOKOKA 10Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata wokovu.

Bila shaka kwa neno hilo umeelewa walokole ni watu wa aina gani

Kuna Uzi upo umeandikwa kwa kina kuhusu kuokoka ngoja nikusogezee ndugu
Wale wanaotupigiaga kelele usiku kucha mchana kutwa hata wakiugua hospital hawataki kwenda, mali hawatafuti na wanajiita Walokole, hao wapo kundi gani ndugu
 
Haki ya Mama alonizaa.

Kukuta Mwanamke ametoa muda wake kujifunza na kufundisha wengine mambo kama haya.

Kwa dunia ya sasa, nikiri kua Katika elfu moja , ni mmoja tu.

Walobaki ndo hao akina Amber rutty na mashabiki zake .

HONGERA KWA KUA ULIZALIWA KUA MKE WA MTU NASIO KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE DUNIANI.
 
Back
Top Bottom