Martrix_32
JF-Expert Member
- Dec 1, 2025
- 1,022
- 2,044
Uaminifu ni tabia njema ya kuwa mkweli inayomfanya mtu akubalike na wengine hata kumpa dhamana ya kitu fulani.
Ni chombo pekee kinachofaa ndani ya mahusiano mbalimbali, kama biashara, mke na mume, mtu na mchumba, marafiki na familia.
Uaminifu ni uwezo unaoleta imani kwa mtu, na njia ya kukupeleka katika ubora wako. Si kila mtu anaweza kuaminika, tunatakiwa kuwa makini katika hilo, kwa maana madhara yake ni makubwa sana. Imani inajengwa na historia ya mtu mmoja ambaye anaweza kuaminika na ni katika sehemu ambazo ameonekana kuwa ni mkweli na mwaminifu.
Kitu cha ajabu sana kuhusiana na imani ni kwamba, inachukua miaka kuijenga lakini dakika kuibomoa. Uaminifu huanza katika mambo madogo, kama kusema ukweli, kutunza muda, kutekeleza majukumu kwa bidii bila hata kushikiliwa, N.k
~ Uaminifu ni mtaji.
~ Uaminifu unaweza badili kidogo kuwa kikubwa.
~ Uaminifu unaweza kuwafanya watu wakuheshimu.
" kitu cha gharama zaidi kikubwa duniani ni uaminifu. Watu wa bei rahisi hawawezi kuumudu"
"Hakuna urithi ulio na utajiri kama uaminifu"