UAMINIFU:dhana iliyowashinda wengi

UAMINIFU:dhana iliyowashinda wengi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
Ni mara nyingi tumesikia au kushuhudia wanandoa au wapenzi wakigombana kwa tuhuma za mmoja au wote kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao, usaliti umekuwa kama fasheni
Simu za mikononi zimekuwa chachu kubwa ya wapenzi kufanya usaliti, magesti na hotel zilizoenea kila kuona ya nchi, mabar na vilabu vya pombe, usafiri uliorahisishwa mno wa bajaj, na bodaboda vyote hivyo vimechangia mno kwa wanandoa na wapenzi kuvunja uaminifu wao
Aghalabu utasikia mtu akimwambia mpenzi wake, unajua mimi ni mwaminifu sana kwako sina mpenzi mwingine zaidi yako lakini ukweli ulivyo ni tofauti kabisa na akisemacho
Uaminifu ni jambo la binafsi mno, lakipekee kabisa ni fahari ya kibinafsi ambayo humpa mtu faraja na amani ya rohoni anapokuwa mwaminifu na mkweli kwa ampendaye
Huhitaji kujitapa kuwa wewe ni mwaminifu, kwakuwa haitasaidia kitu kama humaanishi ukisemacho kumbuka matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno
Natuwe waaminifu sasa kwa wapendwa wetu, tupunguze na kutokomeza kabisa mtandao wa wasio waaminifu, sema neno kama umenielewa ...!
 
Hivi dhana maana yake nini?
 
Aisee mbona kama sijakuelewa vile..... kwa hiyo kama sio mwaminifu unataka wife aniambie ana kidumu????

Uaminifu ni jambo la hinafsi mno, lakipekee kabisa ni fahari ya kibinafsi ambayo humpa mtu faraja na amani ya rohoni anapokuwa mwaminifu na mkweli kwa ampendaye

Haya maneno umeyatoa wapi????!!!! Ufahari wake ukowapi kama hata huyo unayejifanya ni mwaminifu kwake hajawahi kukuona hivyo???? Kwa nn kwanza unahisi uanimifu ni kuwa na mwanamke mmoja???? Kwa akili zako siwezi kuwa mwaminifu kwa wanawake zangu wanne????
 
Aisee mbona kama sijakuelewa vile..... kwa hiyo kama sio mwaminifu unataka wife aniambie ana kidumu????



Haya maneno umeyatoa wapi????!!!! Ufahari wake ukowapi kama hata huyo unayejifanya ni mwaminifu kwake hajawahi kukuona hivyo???? Kwa nn kwanza unahisi uanimifu ni kuwa na mwanamke mmoja???? Kwa akili zako siwezi kuwa mwaminifu kwa wanawake zangu wanne????

Wanne...!!? Du wa halali au nakazalika?
 
uaminifu na kutokua mwaminifu zote ni tabia kama ngozi so watch out!!
 
Uaminifu ni mzuri hakuna atakayebishi ila wahanga wa mapenzi pesa lazima watokwe povu ukigusia uaminifu.
 
mapana ya uaminifu ni yapi naona kama umeegemea eneo moja tu.
 
kunamaswali ya msingi sana yameulizwa na waliotangulia hapa.. Embu yajibu kwanza.
 
Uaminifu ni janga la dunia kuanzia kwa obama hadi sigimbi, bado uaminifu unarani dunia
 
Mkuu ungeenda kuuliza jukwaa la lugha maana uku wako kimapnz zaid

Silimetumika hapa na mimi sijui maana yake?
Nitachangiaje bila kujua kwa usahihi kilichoandikwa?
 
Silimetumika hapa na mimi sijui maana yake?
Nitachangiaje bila kujua kwa usahihi kilichoandikwa?

msubili mleta mada atakujb naona kaleta post alafu kaingia mitin!!!!
 
Sijaingia mitini nilikuwa napata mulo ya mchana
 
sawa mkuu ila katka hayo kuna mengi zaidi hilo. any way its okey
 
Kuaminiana siku hizi na ngumu sana na sio katika mapenzi tu, ila kumbuka uamiifu ni matendo sio maneno
 
Wanne...!!? Du wa halali au nakazalika?

Vyovyote vile.......... kama dini ingeniruhusu ningekuwa nao wengi tu, ndo mana kila mara najiuliza hiki kitu cha kuwa na mke 1 tulikitoa wapi???
 
Vyovyote vile.......... kama dini ingeniruhusu ningekuwa nao wengi tu, ndo mana kila mara najiuliza hiki kitu cha kuwa na mke 1 tulikitoa wapi???

Hata Mimi nashangaa aisee kwakuwa hata mfalme Sulleiman alikuwa na wake wengi na masuria pia ambazo kwa lugha ya kisasa wanaitwa makahaba
 
Back
Top Bottom