Uambiwe?!

Mimi nafikiri kwa hali ya ubinadamu kama kweli unampenda nduguyo ni vema ukamwambia au kumpa tahadhari juu ya mambo flani ambayo hayako sawa. But kama alivyosema nyamayao umwambie kistaarabu. Si lazima uanze na haloo haloooo nimemwona mwaflani kasijui nini nii...................au jana shemeji alikuwa na ,.... hapana tafuta mwanzo mzuri kisha muwe kama mwadiscuss ucheck mwelekeo wake kisha wezamalizia tu na mh kuwa makini mwenzangu maana wanaume/wake hawaaminiki..........likitoka hili toka kwako lazima mwambiwaji atahisi kuna kitu so up to yeye aombe apewe mkanda mzima au aanze chunguza mwenyewe..........Ukikurupuka itakugeukia weye.

Mwanajamii naomba usijue langu, maana jinsi unavyoremba! umeniacha hoi
 
Mwenzio nilisha unbuka nilipomwambia rafiki yangu kuwa mkewe anagawa chakula cha usiku kwa wasela. Si alikwenda kumambia mkewe kuwa mie ndio ource ya hiyo habari na matokeo yake nikawa adui ktk familia ile. Lakini baada ya kipindi cha miezi kadhaa si akawafumania laivu jamaa wakila kile chakula. Na sasa hivi wameachana na ma msapu wake na anaona aibu kuniomba radhi
 
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...

Dada Belinda hapo umemaliza kila kitu. Muhusika ataruka futi mia na wewe mtoa habari utaonekana mmbea
 
Inatofautiana sana kama mahusiano ni ndoa au ni uchumba/u-BF,GF tu
 
Nadhani hii ndo sababu kubwa ya watu kushindwa kuwaambia,
usaliti anaoufanya mmoja baina ya wapendanao,kwani mwisho wa siku,
AIBU inakuwa kwako!!!!!!!!!

Kusema kwa vyovyote unakua mmbeya, na matokeo ni kati ya haya:
  1. Aamini bila ya uchunguzi halafu waachane....
  2. Aamini kiasi fulani afanye uchunguzi...then waachane!
  3. Aamini na aamue kumsamehe....halafu wewe ile kwako...

The best way ni kumpa lead bila kumwambia......ang'amua mwenyewe kama akili bado anazo..
 
mi wala sitamlaumu mtu kwa kutoniambia nitawaelewa tu acha yaliyo sirini yakae huko nimegundua kamoyo kangu hakawezi kubeba mavitu ya kutisha,yale nayohisi kwa bahati mbaya tu nakesha macho ije kuwa na vidhibitisho.

Tatizo huwa linakuwa pale unapogundua halafu wengine huwa wanaanza kuwaambia rafiki zao "Kwanini hamkuniambia kwani mlikuwa kimya kwanini mlinificha" basi anaanza ugomvi na marafiki pia
 
yote sawa tu,mana mwisho ya Yote ni maumivu,ndo mana wanasemaga, KULIA NA KUCHEKA ZOTE NI KELELE.kwaiyo kupewa taarifa kabla au kujua mwenyewe si kigezo cha kuyapunguza MAUMIVU ambayo ndio hatma ya kuyafahamu maovu ya umpendae.
 
Kusema kwa vyovyote unakua mmbeya, na matokeo ni kati ya haya:

  1. Aamini bila ya uchunguzi halafu waachane....
  2. Aamini kiasi fulani afanye uchunguzi...then waachane!
  3. Aamini na aamue kumsamehe....halafu wewe ile kwako...

The best way ni kumpa lead bila kumwambia......ang'amua mwenyewe kama akili bado anazo..

Hivi ukweli nao ni umbeya?
 
Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.

Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?

very good Lizzy,

I was just like you when i was single, ukishaingia kwenye ndoa, ukajua maana ya ndoa na majukumu yake, siku zote utakua unasali usijue afanyayo mwenza ili ndoa yenu iwe imara na watoto wapate malezi mema

I wish ningeweza kudocument hii post halafu ten years down the road tuirejee wote, Mungu akituweka hai

:tape:
 
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...

I like this one

Ndugu yangu usiombe, majority ya relationships zinaharibiwa na watu wa karibu, intentionally au unintentionally... Ni vyema kujua tabia ya mwenzako e.g. akilewa anapenda mabibi au anatamani wanaume, akiwa safarini yuko vulnerable etc. na kusaidiana kukumbushana na kusisitiziana umuhimu wa mahusiano yenu kuliko kusikiliza na kuchapa lapa...

Mahusiano si kuangalia kakosea wapi uondoke au uadhibu, mahusiano pamoja na comfort mnazopeana, ni nafasi ya kujengana na kupunguza mapungufu through partnership

If my wife would only look for my problems au ukicheche, basi leo watoto wangu wangekua mbali na mimi, and I am sure thy would suffer

Haya ya kuambizana ni relevant mnapoanza kwani ni vyema kujuana, lakini pamoja na hayo... baadhi ya tabia za ujana zinatokana na background na mazingira ya wakati, so if you get a chance to change a person, try it

I love this topic
 
Mmh! Nisingependa kuambiwa. Maisha yetu hayamuhusu. Hata mimi ikitokea hvyo sitoweza kusema. Heri lawama kuliko fedheha.
 
Tatizo la kuambiwa ni hili cku mnapatana jamaa atakubembeleza hadi umuambie aliyekuambia wewe utajikoki nakumueleza alisanua, baada ya hapo kuna mawili either jamaa agombane nae au amtongoze sasa hapo ndio shida yenyewe.
You can say that a million times

Madhara ya hizi taarifa ni pale watu wanapopatana
 
Mimi nafikiri kwa hali ya ubinadamu kama kweli unampenda nduguyo ni vema ukamwambia au kumpa tahadhari juu ya mambo flani ambayo hayako sawa. But kama alivyosema nyamayao umwambie kistaarabu. Si lazima uanze na haloo haloooo nimemwona mwaflani kasijui nini nii...................au jana shemeji alikuwa na ,.... hapana tafuta mwanzo mzuri kisha muwe kama mwadiscuss ucheck mwelekeo wake kisha wezamalizia tu na mh kuwa makini mwenzangu maana wanaume/wake hawaaminiki..........likitoka hili toka kwako lazima mwambiwaji atahisi kuna kitu so up to yeye aombe apewe mkanda mzima au aanze chunguza mwenyewe..........Ukikurupuka itakugeukia weye.
trust me hakuna ustaarabu kwenye infidelity!!
 
trust me hakuna ustaarabu kwenye infidelity!!
MTM ustaarabu upo kwenye kitu gani unachomwambia ....kumbuka yule si mtoto mdogo ni mtu mzima badala ya kumweleza mumeo nimemkuta au anatembea na flani.......we upe hint tu............Bi dada mh hebu kuwa makini..usiamini sana wanaume............ unaishia hapo. Sasa unless ana wanaume wengi but kama mwanaume ni mumewe tu na nyeye ni mtu mzima atajiuliza why umesema hivyo ndo aanze kuchanganya akili yake na ya mbayuwayu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom