UAE yaunda wizara mpya ya "furaha"

Kamanda wa Kweli

JF-Expert Member
Jul 13, 2014
1,448
845
UAE yaunda wizara ya mpya ya 'furaha'
  • 9 Februari 2016
Mshirikishe mwenzako
Image copyright AFP
Image caption Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum,Kiongozi wa UAE ,
Waziri mkuu wa Miliki za Kiarabu UAE ametangaza kuundwa kwa wizara mpya ya furaha.

Wizara hiyo mpya imeundwa katika mabadiliko yaliyotekelezwa na utawala wa kiongozi wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Sheikh Maktoum, ambaye ni kiongozi wa Dubai amesema wizara hiyo mpya furaha inaazimia ''kuchochea mtagusano baina ya wananchi wake mbali na kuhamasisha umma utosheke na kile walichonacho''.

Wizara mpya nyingine iliyoundwa ni ''wizara ya kuvumiliana''.

Sheikh Maktoum vilevile ameagiza kuunganishwa kwa wizara nyingi mbali na kutoa zabuni za kuagiza makampuni kutoka nje kuendesha asilimia kubwa ya shughuli za serikali.

"Serikali sharti iweze kunyumbulika kwa urahisi. Nafkiiri hatuitaji wizara zaidi tunachoitaji ni mawaziri wenye uwezo wa kutafsiri mabadiliko na kuatekeleza ipasavyo'' Sheikh Makhtoum aliiambia kongamano la dunia linalojadili miundo ya utawala na serikali mjini Dubai.

''Tunachotaka ni serikali changa itakayokidhi matakwa ya vijanana uma.''

Wizara ya uvumilivu inanuiwa kupalilia nguzo muhimu ya jamii ya raia wa miliki za kiarabu '' alisema Sheikh Makhtoum kupitia mtandao wake wa Tweeter.

Image copyright AFP
Image caption Wizara ya vijana nayo itaongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.
Vijana pia hawakusaulika aliunda baraza la vijana la taifa ''Youth National Council''.

Wajibu wao mkubwa ni kuishauri serikali kuhusiana na maswala yanayowahusu vijana na wataongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.

''Vijana ndio utawala ujao wa taifa hili '' aliongozea.

source : bbc swahili
 
Vijana gani hao wakati utajiri na utawala umeshikiliwa na Al Makhtoum na Al Nahyan? Lakini hii kali ya mwaka labda watawaachia vijana nao wale bata
 
Hii imekaa vizuri sana na huyo Mtawala wa Dubai ni kichwa sana. Wakati wapuuzi wengine kutwa kucha wanapandikiza chuki miongoni mwa jamii. No wonder UAE na Qatar are the most peaceful and most attractive tourist destinations in Middle East kulinganisha na wapandikiza chuki wengine kama kule Egypt ambako wakristo wamekuwa wanaishi katika mateso ya ajabu utadhani sio binadamu. Hii dunia ya muingiliano huwezi kuishi kama enzi za kale mkidhani dunia inaishia kwenye horizon - upeo wa macho.
 
Back
Top Bottom