Uadilifu wa Wakurya ulificha madhaifu ya Polisi

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Habari wana JF

Matukio mawili ta hivi juzi kule Mtwara na Kilindi mkoani Tanga kwa polisi kutuhumiwa kuua imekuwa habari nzito sana nchini Tanzania.

Polisi wanaonekana kupoteana badala ya kulinda raia na mali zao sasa wanatuhumiwa kuhujumu jitihada za raia na mali zao.

Lakini naona kama jeshi la polisi liko kwe mabadiliko makubwa sana( TRANSFORMATION) kuanzia mchakato wa ku recruit mpaka mpaka kuwafundisha kazi askari wetu.

Zamani kidogo jeshi likiajiri zaidi WAKURYA kutoka mkoani Mara lakini pia kutoka vijijini zaidi kuliko kualota watu stand hasa mijini.

Lakini pia ikikuwa ni watoto wa wakulima na wafanyakazi waliokulia kwenye malezi bora sana ya kujua utu ni nini.

Siku hizi ili uwe askari polisi kwanza lazima uwe umepitia JKT kwa mafunzo, uwe umesoma mpaka kidato cha nne ama kuendelea bila kujali mtoto kalelewa katika mazingira gani.

Lakini pia watoto wengi wa askari ndio wako huko na huenda huko baada ta kukosa option nyingine. Wengine wengi huenda huko polisi baada ya kuwa wavuta madawa ya kulevya na kuwa wasumbufu kwa familia zao hivyo kutupwa huko ili familia zao zipate ahueni kidogo.

Wengi wao hata lugha zao za asili kwa maana ya VENECULAR LANGUAGE hawazijui kwa maana kwamba hatujui kama ni Watanzania wa makabila gani japo pia ukabila haukubaliki kama kigezo cha kupata ajira lakini katika kujuana ni muhimu sana.

Polisi wamekuwa na tamaa sana kuliko kuipenda kazi waliyo omba kuifanya. Wametanguliza maslahi binafsi mbele wapate hela kwanjia yeyote ili maisha yao yawe bora huku wakisahau utu wa Watanzania wenzao.

Si kila mtu anaweza kuwa askari hata kama amesoma bila kuangalia background yake. Tutaajiri wahuni, wauaji, vibaka na wezi kuwa askari tuwape silaha nzitoza kutulinda kisha watazigeuzia kwetu tena nandicho kinachotokea sasa.

Kuna haja ya kuangalia upya sera zetu za ajira kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Tusiangalia tu vyeti vyao bila kuangalia uadilifu wao toka utotoni mwao pamoja na makuzi yao pia
 
Kwa kweli jeshini ukikosa majina ya Chacha, Wambura, Mwita n.k ni sawa na timu ya Yanga bila wa-Congo
 
Back
Top Bottom