Heri na fanaka ya Mwaka Mpya JF.
Mwaka 2012 umeanza kwa ishara mbaya kwa wale wanofuatia masuala ya matangamano ya Kimataifa. Ndiyo kwanza rais Barack Obama amesaini kuwekewa vikwazo benki kuu ya Iran, eti kwa sababu nchi hiyo 'ina matamanio' ya kuunda silaha za nuklia. Nimeweka neno 'matamanio' (ambitions) ndani ya vibango kwa kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna dalili yeyote kama Iran ina maatamanio hayo. Iran yenyewe inasema haina.
Lakini, hata kama inayo, so what? Kwa nini vikwazo hivyo haviwekewi wengine, ambao wanazo hasa?
Kama asemavyo Ron Paul 'ukianza mkondo wa vikwazo hatimaye utaishia vita' Hii ndivyo ilivyotokea kwa nchi zote- Iraq, Argentine,Libya.....
(Nchi pekee ambayo vikwazo havijapelekea vita ni Cuba- lakini hii ni special case- kwani Marekani ilipatana na Soviet ya wakati ule kuwa isiiguse Cuba na Soviet haitaigusa Uturuki).
Kwa mujibu wa wachunguzi wengi, vita dhidi ya Iran vitatokea kabla ya mwezi Machi mwaka huu, kutokana na sababu nyingi ambazo uki google utaelewa. Wengine watasema, matishio mengi ya namna hii yamekwishatolewa tangu 2005. Nasema safari hii ni tofauti, hasa Syria ikianguka katika miezi miwili ijayo.
Kwa wale wasio na naamna nyingine ya kupata habari za uhakika, uhasimu wa Marekani na Iran una sababu mbili muhimu
1- Iran kuwa msitari wa mbele wa kutetea haki za WaPalestine kwa vitendo (siyo kama Saudi Arabia na Waarabu wengine)
2- Hofu ya kuwa mfano wa Iran wa kujitegemea wenyewe utaigwa na madola mengine ya Mashariki Ya Kati, na hivyo kuathiri udhibiti wa Marekani wa eneo hili.
3- Kuwepo taifa lililo sawa kwa nguvu za kijeshi na Israel katika Mashariki ya Kati
Utaona kwamba suala la nuklia ni kisingizio tu. Kama unaona habari hizi hazikuhusu, fikiria tena. Iran siyo a 'push over' kama Iraq. Wairan- usi wa confuse na Waarabu- ni watu wenye ari kubwa ya kupigania nchi yao. Mfano ni katika vita vya Iran Iraq. Iraq ilikuwa inasaidiwa na nchi zote kubwa kwa silaha, na Waarabu kwa fedha. Iran ilikuwa pekee ikiwa na vikwazo vya silaha. Lakini ikaweza kumshinda Saddam na lau si kujiingiza Marekani dhahiri wangefika Baghdad, a la Tanzania!
Ninachotaka kusema ni kuwa itakapotokea vita, amini kuwa visima vyote vwa mafuta Mashariki ya Kati vitachomwa moto, na Israeli itashambuliwa kwa maelfu ya makombora- Israel itajibu kwa silaha za nuklia......
vita ya III ya dunia imeanza!