Marekani gizani, mshahara wa Obama wasimamishwa
------------------------------
Ikulu ya Marekani White House imetoa amri ya kufungwa baadhi ya mashirika ya serikali... Amri hiyo ya kufungwa baadhi ya taasisi za serikali ya Marekani ilitolewa jana dakika kumi kabla ya serikali kuishiwa rasmi na fedha za matumizi... Vilevile thuluthi mbili ya wafanyakazi wa serikali akiwemo Rais Barack Obama, watalazimika kufanya kazi bila ya malipo hadi mgogoro wa bajeti kati ya Warepublican na Wademokrat utakapotatuliwa.
Serikali ya Marekani imeamkia (Jana) Jumanne kwa pigo kubwa ya kufunga baadhi ya afisi za umma kutokana na ukosefu wa fedha za kuziendesha. Hili limetokana na kukosekana maafikiano kati ya mabunge mawili ya congress juu ya bajeti mpya.... Watafiti wanasema kuwa makisio yanaonesha kuwa iwapo tatizo hili litaendelea kwa zaidi ya wiki tatu, na afisi hizi kufungwa zaidi ya asili mia 0.9% ya pato la Marekani itapotezwa. Habari kutoka mjini Washington zianasema kuwa mgawanyiko wa kisiasa nchini Marekani ni mbaya sana kiasi kuwa serikali inashindwa kutekeleza majukumu.
Source Aljazeera.