U-nyancha, U-suba, U-girango na U-luo-imbo unavyoitafuna jimbo la Rorya

OBWERE

Member
Jan 14, 2011
46
8
U-NYANCHA, U-SUBA, U-GIRANGO NA U-LUO-IMBO UNAVYOITAFUNA JIMBO LA RORYA

Na, Mwl Chacha Matete
Idara ya Elimu ya Ufundi- MUST

Nianze kwa kumnukuu Baba wa TAifa Mwl. J.K. Nyerere akiongea na wafanyakazi katika sherehe za Siku ya Wafanyazi kitaifa mjini Mbeya 01/05/1995 katika uwanja wa Sokoine - Mbeya. Baba wa taifa alitaja nyufa zinazoitafuna taifa ambazo ni udini, ukabila, rushwa. Akiongelea ukabila Baba wa taifa alisema kuwa watanzania wameanza kutambuana kwa ukabila. Kwamba kiongozi hana sifa, hana uwezo na hakubaliki lakini mtu anasisitiza kuwa atamchagua kisa ni wa kabila lake. Kiongozi ni mla rushwa, ni mbadhirifu, hakubaliki, hana dira lakini ni mmmmhh ni kabila langu*.....alisema JKN. Na Tusimwache mgombea mzuri, sifa zooooote anazo lkn mmmmhh Mkara?

Sote tunaona kinachotokea nchini Kenya ukabila unavyowatafuta, ili uwe kiongozi wa nchi hio aidha uwe mkikuyu au upate sapoti ya wakikuyu. Mauaji ya Kimbari (genocide) nchini Burundi yaliowaondoa kina Prince Louis Ludovico Rwegasore, Melchior Ndadaye, Cyprian Ntaryamira, Meja Jenerali Jean Baptiste Bagaza na Juvenile Habyrimana wa Rwanda ilikuwa ni kwa sababu ukabila kati ya wahutu na watutsi, Ukabila nchini Uganda nao ni mkubwa sana kati ya Ankole na Baganda dhidi ya makabila madogo madogo ya Acholi, Karamajong' nk, ugomvi kati ya Riek Machar na Salva Kirr nchini Sudan Kusini ni kwa ya ukabila kati ya *Lwer na Bor* Mauji ya akina Mohammed Siad Bare na Farah Aidid nchini Somalia ni ukabila (koo), Igbo na Yoruba dhidi ya Fulani na Hausa nchini Nigeria ni ugomvi wa kikabila. Mifano ni mingi sana Africa

Kwetu Tanzania ukabila ni kama haupo japo ipo mioyoni mwa watu. Shukrani kwa kazi nzuri alioifanya baba wa taifa Mwl JKN kwani alifanya kazi kubwa sana kuitokomeza. Tanzania MTU akiongelea kabila lake,mkoa, wilaya au kanda lake anaongelea kwa kificho akihisi atasutwa, atasemwa au atashtakiwa.

Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa ubunge, urais na udiwani Oct 2020 tayari jimbo la Rorya limegawanyika kama sio kumeguka katika sehemu kuu mbili uliochukua sura ya utarafa na ukabila. Wilaya ya Rorya ambayo ina tarafa nne (Nyancha, Suba, Girango na Luo-imbo). Tayari Suba na Nyancha wanaonekana kuungana na kutengeneza Muungano wa Suba one na Suba two wakijipa jina la utani la *Watengwa* au *Yatima* ( Suba 1 - kwasababu tarafa hilo hukaliwa na 98% na wasuba na Suba 2 ni Nyancha kwasababu kuna jamii ya wasuba 45-50% hivo ni ndugu) na pia wote ni watengwa a.k.a yatima, huku tarafa ya Girango na Luo-imbo (japo wanajificha) wakiunda muungano wa G6 au *wateule*

Nitaeleza:

Wakazi wa Suba na Nyancha wanajiita Watengwa kwasababu wanaona wametengwa sana na kubaki nyuma sana kimaendeleo hususan huduma za kijamii za serikali ambazo kiuhalisia ni gharama nafuu kuliko za binafsi. Kutengwa huku kunakoelezwa umefanywa makusudi na mbunge anayemaliza muda wake ili iwe rahisi kuwatawala tofauti na wabunge waliowahi kuongoza jimbo la Rorya (Edward Oyombe Ayila, Mabere Nyaucho Marando na Prof Philemon Sarungi). Wanaeleza kuwa:

1. Tarafa ya Nyancha na Suba ndizo zenye wakazi wengi kuliko Girango na Luo-imbo. Nyancha ina wakazi wapatao 145,647, ikifuatiwa na Suba yenye watu 70,299 huku umoja wa wateule (G6) Girango ikiwa na watu 68,873 na mwisho ni Luo-imbo ikiwa na wakazi 41,087 kwa mantiki hio umoja wa Suba 1&2 una wakazi wengi na ndio wenye kura za maamuzi kwny chaguzi zote. Kutengwa kwao kunafananishwa na kisa cha Wahutu na watutsi nchini Rwanda na Burundi.

2. Huduma za kijamii pamoja na kwamba kundi la Watengwa ndio yenye wakazi wengi lakini kimaendeleo hasa huduma za kijamii wameachwa mbali sana na umoja wa G6 (wateule). Wakazi wa Nyancha wanamlalamikia LOA na Charles Ochele Ombuto (COO) aliekuwa mwenyekiti wa H/W kuwa wanaipendelea waziwazi tarafa ya Girango na Luo-imbo mfano mpaka sasa hivi pamoja na kuwa na shule za sekondari zaidi ya 12 lakini hawana High school huku Umoja wa Wateule wakijimwayamwaya na High school 2 za serikali na 2 za binafsi. Mpaka naandika makala hii Nyancha pamoja na kuwa idadi ya watu 145647 haina kituo cha afya, kwa kuona hivyo LOA na COO wanahisi kichinjio safari hii itakuwa Nyancha wana haha sasa hivi kujenga kituo cha afya *Nyamagaro* ikisemekana kuwa ni tegesha kwa ajili ya uchaguzi na baada ya uchaguzi ujenzi utasitishwa.

3. Kiuchumi na Mapato
Kundi la Watengwa ndio wanaochangia 65% ya mapato ya wilaya ya Rorya. Senta zenye shughuli kubwa na mapato makubwa yoote yapo Suba 1&2. Mfano:

A: Ni Shirati na Kinesi ndiyo zinaongoza kwa kuingizia mapato makubwa sana wilaya ya Rorya, wafanyabiashara wakubwa wa rejareja na jumla wanapatikana hapo lakini maendeleo yanaelekezwa Girango.

B: Mialo mikubwa ya ziwa Victoria iliopo wilaya ya Rorya zote zinapatikana Suba 1&2. Ni Ruhu, kinesi, kibuyi na vingine vidogo vidogo upande wa Suba 1 na Nyangabo, Busanga, Gabimori, Nyanchabo, kwakiberiti, Sota, Masonga, Michire, isegere upande wa Suba 2, yote haya yanatoa makusanyo makubwa sana kwa wilaya lakini unajua kuwa Shirati ipo kilomita 3 tu kutoka ziwani lakini hawana huduma ya maji mpaka Leo?

C: Minada mikubwa ya mifugo na bidhaa yoote yanapatikana kwa Watengwa. Ni Nyamaguku, Shirati, Randa,...wakazi Suba 1&2 wanasema hawajahi kusikia mnada wa Ng'ombe ulioko Girango lakini unajua kuwa barabara ya kinesi kwenda Baraki haipitiki huku Mirare kwenda Nyamasanda unaendesha baiskeli huku umeachia steringi?

Wananchi wa mang'ore, kobondo, mauwe, chuchuri, Nyamagina, Rodi, Nyakenge, Nyangoto, Soroneta, Obuya nk huko Girango meno yoote nje huku wakishangilia utawala wao wa miaka 20 mitamu ya asali na maziwa. Wenzangu na mimi kutoka Kitahiro, Keng'nyi, kibuyi, kihunda, kwisense, isenge, kyamkami, Nyamimi, Bugendi, Nyamwita wakiambulia T-shirts na kofia wakati wa uchaguzi huku G6 wakiwaonea huruma kwa kuwapa chumvi za 500, kanga na kofia za LOA. Toka mradi wa maji wa KMT ufe kuna watoto waliozaliwa na wameoa sasa hivi hawajui na hawajawahi kuona bomba la maji pale Shirati.

D: Wakosoaji wa LOA na COO hawakatai kituo cha afya kiwepo Utegi wa A level kujengwa Nyanduga au Buturi lakini kwa mazingira ya kawaida hasa kiuchumi pale penye idadi kubwa ya watu ndo hufikiriwa kwanza kupewa huduma za kijamii ndipo hufautiwa na wale walio wachache na ndio maana Hospitali ya Bugando ipo Mwanza na sio Mariwa wala Busanga au Osiri.

E: Shule ya Secondari Katuru ilikuwa na sifa zote za kupandishwa hadhi na kuwa High school kulingana uwepo wa miundo mbinu za kutosha, walimu na ukongwe wake. Lakini watu wa Nyancha wanalia High level kupelekwa Buturi yenye watu 40,000 ikiingia kwa Suba two karibu mara nne.

F: Nyancha wanajiuliza hivi LOA na COO wake wameshindwa kweli kusimamia ufunguzi wa Chuo cha Uvuvi - Gabimori?......vipi kama chuo kile kingejengwa Omuga (ziwa lingekuwepo)? inasemekana chuo kimekosa maktaba tu, na sasa yapata miaka mitatu majengo yamekuwa mahame na nyumba za popo. Wanasuba wanajiuliza hivi ukimuambia mtu kutoka Kilimanjaro, Mbeya, Kagera au Tanga kuwa tuna chuo kimekosa maktaba tu kifunguliwe sasa ni miaka minne atatuelewa?

4. Wakazi wa Tarafa hizi wanalalamika kuwa wao ndo wanaongoza kwakuwa na mifugo mingi lakini hawana Lambo za kunyweshea mifugo wala majosho ya kuoshea mifugo yao wala kiwanda cha Nyama au maziwa, kata ya Nyamagaro, Nyamtinga, Kinyenche hawana hata josho moja, Lambo la mifugo pale kijiji cha *Nyambori* kimekwama na naambiwa kimeshabomolewa na maji baada ujenzi wake kusimama kwa miaka minne sasa, huku wakazi wa Kotwo wakiimba atukuzwe baba kwa kuwapa viongozi wao

5. Nimekaa miezi miwili Nyancha wakati huu wa likizo ya Korona, Wananchi wa tarafa hizi hawafichi hisia zao kuwa japokuwa wao wanaishi kandokando ya ziwa lakini hakuna Sera madhubuti ya kuendeleza kilimo na uvuvi. Kwa mujibu wa diwani mmoja (namhifadhi jina) siku mmoja alinisimulia kuwa hata mikopo ya 4% kwa vijana, 4% wanawake na 2% walemavu imewanufaisha zaidi watu wa Girango na Luo-imbo kuliko Suba 1&2 kwa 65% dhidi ya 35% wa hao wanaojiita Watengwa

6. Uchaguzi ndani ya CCM - ngazi ya Wilaya imetawaliwa na Girango zaidi, na mgombea yeyote anaetoka nje Girango lazima uwe upande wa LOA sivyo umekwisha (niliwahi kuandika hili ktk makala zangu). Mwenyekiti wa CCM wilaya anatoka Girango ambaye ni COO ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya. Wakosoaji wanajiuliza inawezekaneje akaisimamia serikali kama kiongozi wa chama. Hata mwenyekiti wa UWT mama yangu Hellen Murya ambaye anatoka Radienya - Nyancha ilibidi atafute uungaji mkono wa kambi ya Girango na ilikuwaridhisha Nyancha wakawaachia hio nafasi.

6. Wakazi wa kandokando ya mto Mori hasa vijiji vya Luanda hasa kitongoji cha Mang'orora, Orinde iliopo Kamot, Olungi iliopo kijiji cha Mori, vijiji vya Miko, Kirogo na Nyabiwe wanapata shida sana hasa kuvuka mto Mori. Kwa miaka mingi sana wameomba sana ujenzi wa daraja ilikupunguza vifo vya watu wanaokufa maji kila mwaka wakati wa kuvuka mto Mori na wengine kuliwa na mamba na viboko ambapo kwa takwimu nilizopata ndani ya miaka 10 watu wapatao 19 wamepoteza maisha yao kati ya Olungi na Nyabiwe. Pia daraja hilo lingewasaidia watu wa tarafa ya Suba njia rahisi sana kufika makao makuu ya wilaya yaliopo lngri - Juu ambapo itakuwa ni kilomita 20 tu badala ya kuzunguka njia ya utegi ambayo ni karibu kilomita 51 kutokea Kinesi au Kibuyi. Lakini wanaona kwakuwa ni daraja inayowaunganisha Suba 1&2 basi wache wafe maji.

7. Watu wa Suba wao wanalo jambo moyoni, wao wanasema hawajahi kuwa na mbunge kutoka kwao. Wabunge wote waliowahi kuongoza jimbo likiitwa Rorya ni wa kutoka Nyancha, Luo-imbo na wafalme wao ni Girango. Wanasema wanataka kula matunda kama waliokula Girango kwa miaka 20, upendeleo wa waliopata wenzao nao waupate maana kuna faida kubwa ya kuwa na mbunge kutoka kwao. Wanaweza wakawa sahihi kwa mtizamo uliojengwa na Girango lkn kwangu Mimi naona dalili za uasi hapa, sio sahihi hata kidogo.

Yapo mengi sana niliyapata na kuyaona kwa macho wakati huu wa likizo ya Korona lakini itoshe tu kusema ukiona MTU mzima analia ujue kuna jambo. *Tuwasaidiaje?*

RAI YANGU
A:
Kwangu mimi wakazi wa Rorya hawahitaji tarafa wala kabila kuwaongoza, watu hawa hawahitaji Suba one na two wala G6. Wananchi hawa wanahitaji kiongozi mwenye maono, mwenye dhamira ya kweli, kiongozi mwenye kuleta maendeleo yalio sawa bila kujali tarafa anayotoka. Hata akitoka Girango miaka 50 lakini ilhali hana upendeleo basi kwangu ndiye kiongozi hasa.

B: Tunahitaji kiongozi mwakilishi wa wananchi sio kiongozi mwakilishi wa biashara zake, kiongozi anayewatenga watu kwa misingi ya walionacho na wasionacho. Kiongozi asiegemea wenye nacho na kuwakandamiza wasionacho. Kiongozi anaejenga makundi maana ukishaunda kundi lako na kujiita *G6 WATEULE* maanake ni kuwa lazima kuna Watengwa tu nao wataungana. Tunataka haki sawa kwa wote ndani na nje ya CCM

C: Tunataka kiongozi ambaye anajua kuwa hatukumchagua kwasababu ya tarafa lake au kabila lake bali tumemchagua kwasababu ya Sera zake, maono yake, dira na falsafa zake, kwetu kabila, dini au tarafa sio mambo ya kujivunia mbele ya watu.

D: Kwangu Mimi utengano sio faida bali ni tunajichimbia kaburi na hivyo tunasubiri kuzikwa. Tunawapa faida maadui zetu hasa wezi wa mifugo ambao wanazidi kuzorotesha maendeleo ya wilaya yetu. Na tusipokuwa makini wezi hawa watatupangia na aina ya viongozi na safu ya uongozi, watatupandikizia viongozi wanaowataka safari hii

MWISHO, NIMUOMBE RAIS WETU MPENDWA NA MWENYEKITI WA CHAMA (CCM) AONE MGAWANYIKO HUU NA ATUSAIDIE KUTULETEA MGOMBEA AMBAYE ATATUUNGANISHA

RORYA NI YETU SOTE, TUUNGANE KUIJENGA RORYA

Maoni
+255 752 761116
 
Lameck Airo(Lakairo) na Ochele obuto wanaiharibu sana Rorya kwa maslahi yao binafsi hawa watu kwanza hawana elimu hata ya darasa la saba. Jimbo halina hata maendeleo hakuna tofauti kati ya rorya ya 1995 na 2020 wanajipa vyeo ili tu biashara zao ziende kiurahisi.
 
Shida kubwa iliyopo hapo ni wanarorya kuendekeza njaa! Rorya hauchaguliwi kwa sababu ya sera zako nzuri bali umebeba nini mkononi. Hao viongozi wenu mnaowalalamikia wameshajua udhaifu wenu.

Kabla hamjamuomba mwenyekiti kuwaletea mgombea mwenye sifa ulizotaja ni vema wanarorya wakajitambua kwanza kwa kuanza kusikiliza na kuchagua sera badala ya kuchagua wenye vi zawadi vya chai na maandazi.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri, haya mambo ndio yananifanyaga nitamani kurudi kuchukua fomu nitupe karata yangu nyumbani. Naipenda sana Rorya ila haya mambo yananikwaza sana. #tupendane
 
rorya kawilaya fulani maskini sana, wakiwa mijini wakaazi wake wajuaji sana ila hamna kitu hawajitambui
wananunulika kwa vipande vya kanga na pesa kidogo,migogoro isiyo isha kila uchao

makao makuu tu ya wilaya ,ikae wapi ilikuwa pinde
 
Nimekutana na Eng Clifford Wambura hapa Kigoma Anadai Analitaka jimbo na yuko kwenye mikakati nikaamuliza, wewe unaishi Kigoma ni vipi utatatua changamoto za watu wa Rorya? Hajanipa majibu yanayoeleweka Kaishia kunipiga blaa blaa nyingi tu.

JamiiForums mobile app
 
Tatizo kubwa mtoa hoja nae ameweka mihemko, hiawezekani watu wawili waonekane wao ndio shida. Rorya iko imra mapungufu yetu tuyaweke sawa wenyewe. Huu ni muda wa uchaguzi hofu na wivu unakuwa mwingi sana
 
Sijawahi kumsikia huyo lakairo akiongea bungeni hata kutetea au kudai jambo kwa mustakabali wa wananchi wa Rorya..!
 
U-NYANCHA, U-SUBA, U-GIRANGO NA U-LUO-IMBO UNAVYOITAFUNA JIMBO LA RORYA

Na, Mwl Chacha Matete
Idara ya Elimu ya Ufundi- MUST

Nianze kwa kumnukuu Baba wa TAifa Mwl. J.K. Nyerere akiongea na wafanyakazi katika sherehe za Siku ya Wafanyazi kitaifa mjini Mbeya 01/05/1995 katika uwanja wa Sokoine - Mbeya. Baba wa taifa alitaja nyufa zinazoitafuna taifa ambazo ni udini, ukabila, rushwa. Akiongelea ukabila Baba wa taifa alisema kuwa watanzania wameanza kutambuana kwa ukabila. Kwamba kiongozi hana sifa, hana uwezo na hakubaliki lakini mtu anasisitiza kuwa atamchagua kisa ni wa kabila lake. Kiongozi ni mla rushwa, ni mbadhirifu, hakubaliki, hana dira lakini ni mmmmhh ni kabila langu*.....alisema JKN. Na Tusimwache mgombea mzuri, sifa zooooote anazo lkn mmmmhh Mkara?

Sote tunaona kinachotokea nchini Kenya ukabila unavyowatafuta, ili uwe kiongozi wa nchi hio aidha uwe mkikuyu au upate sapoti ya wakikuyu. Mauaji ya Kimbari (genocide) nchini Burundi yaliowaondoa kina Prince Louis Ludovico Rwegasore, Melchior Ndadaye, Cyprian Ntaryamira, Meja Jenerali Jean Baptiste Bagaza na Juvenile Habyrimana wa Rwanda ilikuwa ni kwa sababu ukabila kati ya wahutu na watutsi, Ukabila nchini Uganda nao ni mkubwa sana kati ya Ankole na Baganda dhidi ya makabila madogo madogo ya Acholi, Karamajong' nk, ugomvi kati ya Riek Machar na Salva Kirr nchini Sudan Kusini ni kwa ya ukabila kati ya *Lwer na Bor* Mauji ya akina Mohammed Siad Bare na Farah Aidid nchini Somalia ni ukabila (koo), Igbo na Yoruba dhidi ya Fulani na Hausa nchini Nigeria ni ugomvi wa kikabila. Mifano ni mingi sana Africa

Kwetu Tanzania ukabila ni kama haupo japo ipo mioyoni mwa watu. Shukrani kwa kazi nzuri alioifanya baba wa taifa Mwl JKN kwani alifanya kazi kubwa sana kuitokomeza. Tanzania MTU akiongelea kabila lake,mkoa, wilaya au kanda lake anaongelea kwa kificho akihisi atasutwa, atasemwa au atashtakiwa.

Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa ubunge, urais na udiwani Oct 2020 tayari jimbo la Rorya limegawanyika kama sio kumeguka katika sehemu kuu mbili uliochukua sura ya utarafa na ukabila. Wilaya ya Rorya ambayo ina tarafa nne (Nyancha, Suba, Girango na Luo-imbo). Tayari Suba na Nyancha wanaonekana kuungana na kutengeneza Muungano wa Suba one na Suba two wakijipa jina la utani la *Watengwa* au *Yatima* ( Suba 1 - kwasababu tarafa hilo hukaliwa na 98% na wasuba na Suba 2 ni Nyancha kwasababu kuna jamii ya wasuba 45-50% hivo ni ndugu) na pia wote ni watengwa a.k.a yatima, huku tarafa ya Girango na Luo-imbo (japo wanajificha) wakiunda muungano wa G6 au *wateule*

Nitaeleza:

Wakazi wa Suba na Nyancha wanajiita Watengwa kwasababu wanaona wametengwa sana na kubaki nyuma sana kimaendeleo hususan huduma za kijamii za serikali ambazo kiuhalisia ni gharama nafuu kuliko za binafsi. Kutengwa huku kunakoelezwa umefanywa makusudi na mbunge anayemaliza muda wake ili iwe rahisi kuwatawala tofauti na wabunge waliowahi kuongoza jimbo la Rorya (Edward Oyombe Ayila, Mabere Nyaucho Marando na Prof Philemon Sarungi). Wanaeleza kuwa:

1. Tarafa ya Nyancha na Suba ndizo zenye wakazi wengi kuliko Girango na Luo-imbo. Nyancha ina wakazi wapatao 145,647, ikifuatiwa na Suba yenye watu 70,299 huku umoja wa wateule (G6) Girango ikiwa na watu 68,873 na mwisho ni Luo-imbo ikiwa na wakazi 41,087 kwa mantiki hio umoja wa Suba 1&2 una wakazi wengi na ndio wenye kura za maamuzi kwny chaguzi zote. Kutengwa kwao kunafananishwa na kisa cha Wahutu na watutsi nchini Rwanda na Burundi.

2. Huduma za kijamii pamoja na kwamba kundi la Watengwa ndio yenye wakazi wengi lakini kimaendeleo hasa huduma za kijamii wameachwa mbali sana na umoja wa G6 (wateule). Wakazi wa Nyancha wanamlalamikia LOA na Charles Ochele Ombuto (COO) aliekuwa mwenyekiti wa H/W kuwa wanaipendelea waziwazi tarafa ya Girango na Luo-imbo mfano mpaka sasa hivi pamoja na kuwa na shule za sekondari zaidi ya 12 lakini hawana High school huku Umoja wa Wateule wakijimwayamwaya na High school 2 za serikali na 2 za binafsi. Mpaka naandika makala hii Nyancha pamoja na kuwa idadi ya watu 145647 haina kituo cha afya, kwa kuona hivyo LOA na COO wanahisi kichinjio safari hii itakuwa Nyancha wana haha sasa hivi kujenga kituo cha afya *Nyamagaro* ikisemekana kuwa ni tegesha kwa ajili ya uchaguzi na baada ya uchaguzi ujenzi utasitishwa.

3. Kiuchumi na Mapato
Kundi la Watengwa ndio wanaochangia 65% ya mapato ya wilaya ya Rorya. Senta zenye shughuli kubwa na mapato makubwa yoote yapo Suba 1&2. Mfano:

A: Ni Shirati na Kinesi ndiyo zinaongoza kwa kuingizia mapato makubwa sana wilaya ya Rorya, wafanyabiashara wakubwa wa rejareja na jumla wanapatikana hapo lakini maendeleo yanaelekezwa Girango.

B: Mialo mikubwa ya ziwa Victoria iliopo wilaya ya Rorya zote zinapatikana Suba 1&2. Ni Ruhu, kinesi, kibuyi na vingine vidogo vidogo upande wa Suba 1 na Nyangabo, Busanga, Gabimori, Nyanchabo, kwakiberiti, Sota, Masonga, Michire, isegere upande wa Suba 2, yote haya yanatoa makusanyo makubwa sana kwa wilaya lakini unajua kuwa Shirati ipo kilomita 3 tu kutoka ziwani lakini hawana huduma ya maji mpaka Leo?

C: Minada mikubwa ya mifugo na bidhaa yoote yanapatikana kwa Watengwa. Ni Nyamaguku, Shirati, Randa,...wakazi Suba 1&2 wanasema hawajahi kusikia mnada wa Ng'ombe ulioko Girango lakini unajua kuwa barabara ya kinesi kwenda Baraki haipitiki huku Mirare kwenda Nyamasanda unaendesha baiskeli huku umeachia steringi?

Wananchi wa mang'ore, kobondo, mauwe, chuchuri, Nyamagina, Rodi, Nyakenge, Nyangoto, Soroneta, Obuya nk huko Girango meno yoote nje huku wakishangilia utawala wao wa miaka 20 mitamu ya asali na maziwa. Wenzangu na mimi kutoka Kitahiro, Keng'nyi, kibuyi, kihunda, kwisense, isenge, kyamkami, Nyamimi, Bugendi, Nyamwita wakiambulia T-shirts na kofia wakati wa uchaguzi huku G6 wakiwaonea huruma kwa kuwapa chumvi za 500, kanga na kofia za LOA. Toka mradi wa maji wa KMT ufe kuna watoto waliozaliwa na wameoa sasa hivi hawajui na hawajawahi kuona bomba la maji pale Shirati.

D: Wakosoaji wa LOA na COO hawakatai kituo cha afya kiwepo Utegi wa A level kujengwa Nyanduga au Buturi lakini kwa mazingira ya kawaida hasa kiuchumi pale penye idadi kubwa ya watu ndo hufikiriwa kwanza kupewa huduma za kijamii ndipo hufautiwa na wale walio wachache na ndio maana Hospitali ya Bugando ipo Mwanza na sio Mariwa wala Busanga au Osiri.

E: Shule ya Secondari Katuru ilikuwa na sifa zote za kupandishwa hadhi na kuwa High school kulingana uwepo wa miundo mbinu za kutosha, walimu na ukongwe wake. Lakini watu wa Nyancha wanalia High level kupelekwa Buturi yenye watu 40,000 ikiingia kwa Suba two karibu mara nne.

F: Nyancha wanajiuliza hivi LOA na COO wake wameshindwa kweli kusimamia ufunguzi wa Chuo cha Uvuvi - Gabimori?......vipi kama chuo kile kingejengwa Omuga (ziwa lingekuwepo)? inasemekana chuo kimekosa maktaba tu, na sasa yapata miaka mitatu majengo yamekuwa mahame na nyumba za popo. Wanasuba wanajiuliza hivi ukimuambia mtu kutoka Kilimanjaro, Mbeya, Kagera au Tanga kuwa tuna chuo kimekosa maktaba tu kifunguliwe sasa ni miaka minne atatuelewa?

4. Wakazi wa Tarafa hizi wanalalamika kuwa wao ndo wanaongoza kwakuwa na mifugo mingi lakini hawana Lambo za kunyweshea mifugo wala majosho ya kuoshea mifugo yao wala kiwanda cha Nyama au maziwa, kata ya Nyamagaro, Nyamtinga, Kinyenche hawana hata josho moja, Lambo la mifugo pale kijiji cha *Nyambori* kimekwama na naambiwa kimeshabomolewa na maji baada ujenzi wake kusimama kwa miaka minne sasa, huku wakazi wa Kotwo wakiimba atukuzwe baba kwa kuwapa viongozi wao

5. Nimekaa miezi miwili Nyancha wakati huu wa likizo ya Korona, Wananchi wa tarafa hizi hawafichi hisia zao kuwa japokuwa wao wanaishi kandokando ya ziwa lakini hakuna Sera madhubuti ya kuendeleza kilimo na uvuvi. Kwa mujibu wa diwani mmoja (namhifadhi jina) siku mmoja alinisimulia kuwa hata mikopo ya 4% kwa vijana, 4% wanawake na 2% walemavu imewanufaisha zaidi watu wa Girango na Luo-imbo kuliko Suba 1&2 kwa 65% dhidi ya 35% wa hao wanaojiita Watengwa

6. Uchaguzi ndani ya CCM - ngazi ya Wilaya imetawaliwa na Girango zaidi, na mgombea yeyote anaetoka nje Girango lazima uwe upande wa LOA sivyo umekwisha (niliwahi kuandika hili ktk makala zangu). Mwenyekiti wa CCM wilaya anatoka Girango ambaye ni COO ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya. Wakosoaji wanajiuliza inawezekaneje akaisimamia serikali kama kiongozi wa chama. Hata mwenyekiti wa UWT mama yangu Hellen Murya ambaye anatoka Radienya - Nyancha ilibidi atafute uungaji mkono wa kambi ya Girango na ilikuwaridhisha Nyancha wakawaachia hio nafasi.

6. Wakazi wa kandokando ya mto Mori hasa vijiji vya Luanda hasa kitongoji cha Mang'orora, Orinde iliopo Kamot, Olungi iliopo kijiji cha Mori, vijiji vya Miko, Kirogo na Nyabiwe wanapata shida sana hasa kuvuka mto Mori. Kwa miaka mingi sana wameomba sana ujenzi wa daraja ilikupunguza vifo vya watu wanaokufa maji kila mwaka wakati wa kuvuka mto Mori na wengine kuliwa na mamba na viboko ambapo kwa takwimu nilizopata ndani ya miaka 10 watu wapatao 19 wamepoteza maisha yao kati ya Olungi na Nyabiwe. Pia daraja hilo lingewasaidia watu wa tarafa ya Suba njia rahisi sana kufika makao makuu ya wilaya yaliopo lngri - Juu ambapo itakuwa ni kilomita 20 tu badala ya kuzunguka njia ya utegi ambayo ni karibu kilomita 51 kutokea Kinesi au Kibuyi. Lakini wanaona kwakuwa ni daraja inayowaunganisha Suba 1&2 basi wache wafe maji.

7. Watu wa Suba wao wanalo jambo moyoni, wao wanasema hawajahi kuwa na mbunge kutoka kwao. Wabunge wote waliowahi kuongoza jimbo likiitwa Rorya ni wa kutoka Nyancha, Luo-imbo na wafalme wao ni Girango. Wanasema wanataka kula matunda kama waliokula Girango kwa miaka 20, upendeleo wa waliopata wenzao nao waupate maana kuna faida kubwa ya kuwa na mbunge kutoka kwao. Wanaweza wakawa sahihi kwa mtizamo uliojengwa na Girango lkn kwangu Mimi naona dalili za uasi hapa, sio sahihi hata kidogo.

Yapo mengi sana niliyapata na kuyaona kwa macho wakati huu wa likizo ya Korona lakini itoshe tu kusema ukiona MTU mzima analia ujue kuna jambo. *Tuwasaidiaje?*

RAI YANGU
A:
Kwangu mimi wakazi wa Rorya hawahitaji tarafa wala kabila kuwaongoza, watu hawa hawahitaji Suba one na two wala G6. Wananchi hawa wanahitaji kiongozi mwenye maono, mwenye dhamira ya kweli, kiongozi mwenye kuleta maendeleo yalio sawa bila kujali tarafa anayotoka. Hata akitoka Girango miaka 50 lakini ilhali hana upendeleo basi kwangu ndiye kiongozi hasa.

B: Tunahitaji kiongozi mwakilishi wa wananchi sio kiongozi mwakilishi wa biashara zake, kiongozi anayewatenga watu kwa misingi ya walionacho na wasionacho. Kiongozi asiegemea wenye nacho na kuwakandamiza wasionacho. Kiongozi anaejenga makundi maana ukishaunda kundi lako na kujiita *G6 WATEULE* maanake ni kuwa lazima kuna Watengwa tu nao wataungana. Tunataka haki sawa kwa wote ndani na nje ya CCM

C: Tunataka kiongozi ambaye anajua kuwa hatukumchagua kwasababu ya tarafa lake au kabila lake bali tumemchagua kwasababu ya Sera zake, maono yake, dira na falsafa zake, kwetu kabila, dini au tarafa sio mambo ya kujivunia mbele ya watu.

D: Kwangu Mimi utengano sio faida bali ni tunajichimbia kaburi na hivyo tunasubiri kuzikwa. Tunawapa faida maadui zetu hasa wezi wa mifugo ambao wanazidi kuzorotesha maendeleo ya wilaya yetu. Na tusipokuwa makini wezi hawa watatupangia na aina ya viongozi na safu ya uongozi, watatupandikizia viongozi wanaowataka safari hii

MWISHO, NIMUOMBE RAIS WETU MPENDWA NA MWENYEKITI WA CHAMA (CCM) AONE MGAWANYIKO HUU NA ATUSAIDIE KUTULETEA MGOMBEA AMBAYE ATATUUNGANISHA

RORYA NI YETU SOTE, TUUNGANE KUIJENGA RORYA

Maoni
+255 752 761116
Mwenyekiti wa CCM awaletee mtu,sio kwamba nyie kama wenye eneo mna mjua atakaewafaa nyie kama nyie mpaka Magufuli awaletee mtu?

Yaani Magufuli anajua better than all of you of what leader you need na sio nyie???

Yaani mnapenda kupangiwa kiongozi?

Mavi yenu kabisa
 
Back
Top Bottom