Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,189
Serikali ya Emirates - UAE imeonya kuwachukulia hatua kali raia wake watakaoonyesha huruma ama kutetea Nchi ya Qatar kufuatia hatua zilizochukuliwa na nchi washirika wa kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia kuiwekea vikwazo Qatar kwa tuhuma za kufadhiri vikundi vinavyojihusisha na ugaidi. Nchi hiyo imeweka adhabu ya Dola 136,000 na adhabu ya miaka 15 gerezani.
Mimi ni mmoja wa wanaopenda demokrasia kuwa mikononi mwa watu kwa kuwa ni muumini wa Utilitarianism na wala siungi mkono uamuzi huo wa UAE. Hata hivyo najaribu kulinganisha na mazingira ya Nchi yetu kuwa suala hilo lingechukuliwaje? Ndio tujifunze umuhimu wa kuwa na umoja kwenye masuala ya kitaifa hata kama muda mwingine watawala wetu wanakosea kwani nao ni binadamu. Masuala ya rasilimali za Nchi ni lazima yatuunganishe kwa namna yoyote hasa madini yetu. Hivi tukishindwa vita simple kama hiyo itakuwaje kwa lie ya Ziwa Nyasa dhidi ya Malawi hao watu watatuunga mkono? Nawasilisha