U-17: Tanzania vs Afrika Kusini

U-17: Tanzania vs Afrika Kusini

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
UPDATES: MATOKEO YA MWISHO TANZANIA 0 - 0 aFRIKA KUSINI

Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania(Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos) itachezwa kwa kiingilio cha sh. 2,000.

Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam ndiyo utakaokuwa mwenyeji wa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri.

Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Shelisheli. Mwamuzi wa kati ni Allister Barra wakati wasaidizi wake ni Gerard Pool na Jean Joseph Felix Ernest wakati mezani atakuwa Nelson Emile Fred. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.




Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.

Chanzo: http://shaffihdauda.com/?p=3439#sthash.JLdmVYdt.dpuf
 
Hatima ya soka letu kwa miaka minne ijayo itaamuliwa na mechi ya Leo na j2 mungu isaidie Tanzania
 
Hatima ya soka letu kwa miaka minne ijayo itaamuliwa na mechi ya Leo na j2 mungu isaidie Tanzania

Nabisha, mechi moja inawezaje kuamua hatima ya miaka minne?
 
Back
Top Bottom