Tz: Taifa la kusikilizia

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Watanzania na hasa viongozi wetu tumekumbwaa na ka ugonjwa kabaya sana "KUSIKILIZIA". Ule msemo maarufu "tafakari chukua hatua" is just for jokes kwenye pombe, au kwenye sherehe na sometimes mikwala ili mtoa mkwala aonekane yuko siriaz!

Hebu fikiria:

1. Tuhuma za wiki hii kuhusu Jairo na wizara yake - Jairo "anasikilizia" nini say raisi ataamua, polisi pia "wanasikilizia" wataamrishwa lini ili nao wafanye uchunguzi, Takukuru baada ya kusikilizia kwa mara ya kwanza eti wanachukua hatua ambazo muda si mrefu tutagundua ni bora wangeendelea "kusikilizia".

2. Tatizo la umeme - Wananchi "wanasikilizia" serikali itasema na kuamua nini, Tanesco "wanaisikilizia" wizara na wizara nayo "inasikilizia".

3. Ubadhirifu katika ununuzi wa rada - Pamoja na ushahidi woteunaooonyesha jinsi akina Chenge walivyohusika lakini polisi wetu hawawezi hata kuanza uchunguzi kwa sababu "wanasikilizia", Takukuru wanendelea "kusikilizia" kwa kisingizio walishafanya uchunguzi, DPP "anasikilizia" na sisi wananchi "tunasikilizia".

4. Sakata la Dowans ndiyo usiseme maana hilo hata mkulu alikuwa "anasikilizia"

5. EPA, MEREMETA, KAGODA, DEEP GREEN etc., wahalifu wake "wanasikilizia", Takukuru, DPP wanaendelea "kusikilizia" hata Pinda na JK wanatusikilizia sisi wananchi huku nasi tukiwa "tunaisikilizia" serikali.

Kifupi tumekuwa taifa la kusikilizia, mawaziri wetu wanasikilizia, watendaji wa wizara "wanasikilizia" mamlaka husika "zinasikilizia", wananchi "tunasikilizia". Just for your homework show me a country inayoendesha mambo kwa kusikilizia halafu"ikaendelea". Anywayz watanzania tumeamua kuwa watu wa "kusikilizia" basi tuendelee "kusikilizia" hatustahili kumlaumu mtu kwa sababu "NDIVYO TULIVYO" watu wa "kusikilizia".
 
watanzania na hasa viongozi wetu tumekumbwaa na ka ugonjwa kabaya sana "kusikilizia". Ule msemo maarufu "tafakari chukua hatua" is just for jokes kwenye pombe, au kwenye sherehe na sometimes mikwala ili mtoa mkwala aonekane yuko siriaz!

hebu fikiria:

1. Tuhuma za wiki hii kuhusu jairo na wizara yake - jairo "anasikilizia" nini say raisi ataamua, polisi pia "wanasikilizia" wataamrishwa lini ili nao wafanye uchunguzi, takukuru baada ya kusikilizia kwa mara ya kwanza eti wanachukua hatua ambazo muda si mrefu tutagundua ni bora wangeendelea "kusikilizia".

2. Tatizo la umeme - wananchi "wanasikilizia" serikali itasema na kuamua nini, tanesco "wanaisikilizia" wizara na wizara nayo "inasikilizia".

3. Ubadhirifu katika ununuzi wa rada - pamoja na ushahidi woteunaooonyesha jinsi akina chenge walivyohusika lakini polisi wetu hawawezi hata kuanza uchunguzi kwa sababu "wanasikilizia", takukuru wanendelea "kusikilizia" kwa kisingizio walishafanya uchunguzi, dpp "anasikilizia" na sisi wananchi "tunasikilizia".

4. Sakata la dowans ndiyo usiseme maana hilo hata mkulu alikuwa "anasikilizia"

5. Epa, meremeta, kagoda, deep green etc., wahalifu wake "wanasikilizia", takukuru, dpp wanaendelea "kusikilizia" hata pinda na jk wanatusikilizia sisi wananchi huku nasi tukiwa "tunaisikilizia" serikali.

Kifupi tumekuwa taifa la kusikilizia, mawaziri wetu wanasikilizia, watendaji wa wizara "wanasikilizia" mamlaka husika "zinasikilizia", wananchi "tunasikilizia". Just for your homework show me a country inayoendesha mambo kwa kusikilizia halafu"ikaendelea". Anywayz watanzania tumeamua kuwa watu wa "kusikilizia" basi tuendelee "kusikilizia" hatustahili kumlaumu mtu kwa sababu "ndivyo tulivyo" watu wa "kusikilizia".

kusikiliza pia ndio kulikokufikisha hapo ulipo,bila kusikiliza usingekuwa hapo na kutumia internet na kujiunga jamii forum kujadili mada mbali mbali..hivyo basi kusikiliza muhimu...
 
kusikiliza pia ndio kulikokufikisha hapo ulipo,bila kusikiliza usingekuwa hapo na kutumia internet na kujiunga jamii forum kujadili mada mbali mbali..hivyo basi kusikiliza muhimu...

Basi tuendelee kusikilizia!!!!!
 
Pinda alishindwa kuamua suala la Jairo akisikilizia kwanza kama mkuu wake atambeba au la... Na amegundua mwelekeo ni kumbeba hivyo anasikilizia upepo wa wabunge...
 
Na sisi tunasikilizia nani ataanzisha mapambano ya kumng'oa.

na hata akijitokeza wakuanza hayo mapambano tutaendelea kuomba update kwenye key board za computer ili tuendelee kusikiliza kinachoendelea huko kwenye mapambano, looh! TAIFA LA KUSIKILIZA.
 
Acheni tuendelee kusikilizia maana wote watanzania tunasikiliziana tu akuna wa kulianzisha. na hata akija wakulianzisha tutamsikilizia polisi wana sema fanya nini. TAIFA LA KUSIKILIZIA TANZANIA JAMANI WATU WA KUSIKILIZIA
 
na hata akijitokeza wakuanza hayo mapambano tutaendelea kuomba update kwenye key board za computer ili tuendelee kusikiliza kinachoendelea huko kwenye mapambano, looh! TAIFA LA KUSIKILIZA.

Ndiyo hivyo mkuu!!!!
 
Kupanga ni kuchagua, kama tumechoka kusikilizia haya yote basi tuamue kufanya kama Misri, Libya n.k na ili tusikilizie ladha ya mabomu ya machozi na risasi za moto kwa ajili ya kukifanya kizazi kijacho kusikilizia matunda ya tutakachokisilizia !!!
 
Nchi makini inayofanya maamuzi magumu ndio hii
kweli nimeamini kweli kama watu wanaiba halafu mpaka leo bado watu wapo ofisini
 
Nchi makini inayofanya maamuzi magumu ndio hii
kweli nimeamini kweli kama watu wanaiba halafu mpaka leo bado watu wapo ofisini

Mkuu si unaona Ikulu sasa inasikilizia kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu Jairo, anayesikiliziwa ni JK naye atarudi hapa kusikilizia kwanza kabla ya kupiga propaganda kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi!
 
Nyambala, ndiyo maana hawaishi kutuletea hadithi na misemo. Wanajua tutawasikiliaza tu.Ukiachilia mambo mengi uliyoorodhesha si unaona ngonjera za Jairo, yaani kiongozi mwendamizi wa serikali ana tuhuma za kutoa rushwa kwa watunga sheria bado anapewa likizo ili uchunguzi wa katibu mkuu Luhanjo ufanyike. Lini CAG amewahi kwafikisha wala mapesa au watoa rushwa mahakamani? Luhanjo anasema ametoa siku 10, halafu siku za Jairo kujibu hazijulikani, wa TZ watakuwa wanasikiliza. Mbona Mwakalebela alikamatwa hapo hapo. Luhanjo anataka tumsikilize ili adanganye umma kwa vifungu vya ajabu vya sheria, ili kulindana tu.

Maneno yanayotupumbaza; Mkakati, mchanganuo, tunalifanyia kazi, sheria zifuatwe, mamlaka ya juu, tahmini, uchunguzi wa kina.
Tunatakiwa tuanze na wanaoficha uvundo kama katibu mkuu kiongozi, DPP, DCI, PCCB,IGP.

Hawa ndio wanatumika kuficha uhalifu kwa maneno ya kuudhi.Badala ya kuwasikiliza tuwaambie hatudanganyiki, na hili naanza na katibu mkuu kiongozi.
Tusiposema basi kusikiliza tutaendelea kuwa masikini na wanyonge kila siku. Kwanini tusiazamie kuwa hakuna kuwasikiliza tena? Maamuzi magumu hayaishii kwenye vyama, sisi wananchi ni wakati sasa tuchukue maamuzi magumu dhidi ya wadanganyifu.
 
Mkuu hii ya Jairo nadhani bado wanaendelea kusikilizia na ukizingatia upepo sasa unavumia kule kwenye trilioni na bilini kadhaa Arusha usije shangaa kusikilizia ikawa mpaka mwakani. Bongo tambararereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
Back
Top Bottom