Tz Hip-Hop Emcees na 'vipini/heleni' masikioni. Ni nani kawaroga?

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,127
8,155
Binafsi, mimi ni shabiki mkubwa sana wa muziki huu pendwa wa hip-hop. Nime-develop mahaba makubwa na hip-hop since back in days kitambo nikiwa mdogo until to-date, and I will always be in true love with HIP HOP ever! I really enjoy and relax to the fullest whenever I listen to hip hop flovour. During my leisure moments, hip hop comes into my mind forefront!

Lakini kadri siku zinavyosonga na mziki huu kukua ndani ya bongo and beyond, emcees wetu nao wanazidi kwa kasi kudondokea kwenye hii tabia chafu ya uvaaji heleni masikioni utadhani wanawake, na tunakoelekea huko mbeleni nahisi wataanza kubandika na vipini puani.

Frankly speaking, siku ambayo nilikuwa shocked na kugundua kwamba the situation is now getting worse, ni pale nilipomuona PROF JAY (the hip-hop legend mwenye legacy kubwa bongo) nae eti kaanza kuvaa kipini sikioni. Nilishtushwa sana and I was: ''W.T.F. huyu mkongwe nae kaanza swagga hizi???!!!''. Nilishangaa sana coz sikutarajia hip-hop icons wa bongo kama Prof Jay and others waliodumu kwenye game muda mrefu wakicomply with hip-hop code of conduct, leo hii waanze kubana vipini masikioni kama hawa upcoming hip-hop emcees tunaowaona au hawa wabana pua. It is a big shame and very unethical as regards to hip-hop basics!!!

Binafsi, tabia hii inanichefua sana, hasa ninapoona real hip-hop emcee kapigilia vipini masikioni. Wabana pua wao wavae tu kwani sinaga muda wa kuwatazama wala kusikiliza nyimbo zao. But my primary concern ni hawa wasanii wa hip-hop. Na nimekuwa nikijiuliza ni kitu gani kinachowafanya emcees wetu waambukizane hii tabia so rapidly, je ni ulimbukeni wa kuendana na usasa in the entire music industry? au ndo modern hip-hop hiyo? au ni behavioral-change conspiracy yenye back-up from western countries (''the first world'') ili kupenyeza na ku-internalize slowly mikakati yao ya ushoga in Africa? au ni anguko tu la maadili na kuiga mambo yasiyofaa? Mind you that hawa hawa emcees wanaovaa heleni/vipini masikioni, makusudi kabisa jinzi/suruali zao wanazishusha 'kata K' then boxer/chu.pi nje nje (hasa wakati waki-perform kwenye stage). Achilia mbali suala la 'kusuka'.

Tabia hii inatukera sana mafans wa muziki wa hip-hop Tz. Personally inanikera to the fullest.
I genuinely wish something affirmative should be done so that to clear such fishy behavioral atmosphere in hip-hop community ya bongo. Please, hip-hop emcees mnaovaa vipini/heleni, STOP STOP SOTP such d.ump-a.ss swag. Kama hamuwezi kuacha kuvaa heleni, basi just quit the game. Ebu DON'T contaminate our hip-hop music na u-cameroon wenu. HIP HOP is all about community potentials & stability, na sio vinginevyo. Gadem it!!!!

Ila pamoja na hiyo moral decay inayosambaa kwa kasi currently, angalau bado kuna hip-hop emcees baadhi ambao kwakweli sijawahi (mimi binafsi) kuwaona wamevaa heleni/vipini masikioni. Emcees kama SALU-T, BONTA, G-NAKO, NASH MC (na most of wenzake wa Tamaduni), FID Q, CHINDO, KIMBUNGA, KALAPINA (na most of wenzake wa kikosi), IZZO B, etc. Hawa sijawahi kuwaona na heleni/vipini masikioni. I STAND TO BE CORRECTED if proved otherwise!


-Kaveli-
 
umagharibi mwing mpaka tunaharibu,ndo tatzo letu wa tz

upo sahihi mkuu. kwakweli huu 'umagharibi' unaozesha akili zetu waafrika. Tunaiga kila jambo kutoka magharibi (hata liwe bovu). dizaini kama bado 'wametawala' akili zetu
 
keveli nipe mchano ya hip-hop ili tuelewe kweli wewe ni mwa sisi mwezetu.

keveli tupe mchano
ukishidwa tutakupe kibano,

hahahaa kaka Bush, bado hujalala tu mpaka mishale hii? au ndo umedhamiria kumsaka 'demu mwenye mwanya' kwa udi na uvumba.

Back to topic: (though hoja yako ipo off-topic kidogo)

Mkuu kwanza kabisa hakuna mahala popote nimesema kuwa mimi ni muasisi (nadhani ndo hiyo 'mwasisi' uliyomaanisha wewe) wa hip-hop.

Pili, upenzi wa music waweza kuwa KUIMBA/KUCHANA, KUTUNGA MASHAIRI, KUSIKILIZA, au KUCHEZA. So to clear the shadow of doubt, mimi upenzi wangu kwenye HIP-HOP ni KUSIKILIZA tu mkuu. Hata andiko langu lina-portray openly kabisa kwamba I am just a FAN (SHABIKI) of hip-hop music.

Otherwise, wewe ndo utupe mistari hapa ili ku-justify uasisi wako. Mwaga wino kaka, tupe ladha. :becky:

-Kaveli-
 
Yo yo yo nakuja kama najamba kumbe naharisha,harisha na hapo katikati kumbe nmemzungusha!! Twende nigga nipe michano......

yeah, nakouna unavyojamba,

lakn ujue kujamba

maswala ya kishamba

nakona kama ni wakutoka shamba
 
Mtoa Mada hujielewi nawish siku tembelea Bronx Brooklyn Queens jamaica compton utajua HIP HOP SIO KUTOA MADA HAZINA KICHWA WALA MIGUU.
 
Mtoa Mada hujielewi nawish siku tembelea Bronx Brooklyn Queens jamaica compton utajua HIP HOP SIO KUTOA MADA HAZINA KICHWA WALA MIGUU.

Mtoa mada kazungumzia wana HIP HOP wa Bongo..na sio huko ulipopataja....vile vile si kila yanayofanyika huko unayaona yanafaa...mengine tuyaache.....inawezekana wewe ndiye hujielewi au umeshindwa kumuelewa mtoa mada....
 
Mtoa mada kazungumzia wana HIP HOP wa Bongo..na sio huko ulipopataja....vile vile si kila yanayofanyika huko unayaona yanafaa...mengine tuyaache.....inawezekana wewe ndiye hujielewi au umeshindwa kumuelewa mtoa mada....

Sasa hyo hip hop ya bongo n Ipi me najua kuna Hip Hop tu sijajua kama kuna hip hop ya Bongo hyo mtu kuvaa vipini n uhuru wa mtu yeyote.
 
Sasa hyo hip hop ya bongo n Ipi me najua kuna Hip Hop tu sijajua kama kuna hip hop ya Bongo hyo mtu kuvaa vipini n uhuru wa mtu yeyote.

Kiasili muziki wa hip hop huko ndiko ulipoasisiwa na sisi huku tumeupokea kutokana na kuukubali kutokana na uzuri wa maudhui.....lakini wakati huo huo tumeupokea huku tukiwa na tamaduni zetu...na kuvaa vipini kwa watoto wa kiume si sehemu ya utamaduni wetu....ingawa ni uhuru wa mtu binafsi...tunayapenda maudhui yake lakini so kigezo cha kuiga kila wafanyalo wana hip hop hata kama linapingana na tamaduni zetu..na hatimaye kuonekana vituko mbele ya jamii iliyostaarabika...
 
Sasa hyo hip hop ya bongo n Ipi me najua kuna Hip Hop tu sijajua kama kuna hip hop ya Bongo hyo mtu kuvaa vipini n uhuru wa mtu yeyote.

nilishawahi kuandika hivi

Hip hop inatafsirika au unaweza kuiita ni maisha halisi haijalishi wapi ulipo jinsia yako wala rangi yako.

Chimbuko la Hip hop linaweza
kufafanuliwa kwa kifupi kama ‘juhudi za wasiojiweza’. Hili
lilionekana dhahiri wakati Wamarekani
weusi walipokuwa wakipigania haki zao za kijamii, wakati huo wa civil rights movement. Hapa kwa haraka tunaona uhusiano wa Hip Hop na jamii.
Hip Hop ikiwa upande wa wanyonge, ikitumika kama sauti ya wakandamizwaji.

Miaka hiyo imekwishapita na
muziki huu umekua na kuwa ni
utamaduni. Lakini bado umebaki na damu ya uanaharakati. Hip Hop
imebadilika kama tamaduni yeyote ile, na mpaka kuvuka mipaka. Mipaka hiyo ilivuka hadi kufika Tanzania ambako ilikaribishwa.

Boardman anajenga hoja kuwa,
Hip Hop ilifanikiwa kuvuka mipaka ya Tanzania kutokana na kuanguka kwa Siasa ya Ujamaa. Mwanzo ulikuwa mgumu, na bado safari ni ndefu, lakini mafanikio yanaonekana; kama kukubalika na jamii.

Muziki huu hata hivyo bado
unaonekana kama ni tamaduni ya
Kimarekani zaidi, huku kuna baadhi ya watu kwenye jamii zetu ambao wanaona Hip Hop ya nyumbani ‘ina- recycle’ tu yale yanayofanywa na wasanii wa Marekani. Kwenye hilo natumaini kuwa kila mtu atakuwa na mawazo yake, lakini ili kupata jibu lililo karibu na sahihi, ni vizuri kurudi kwenye chimbuko la tamaduni wa muziki huu wa Hip Hop. Muziki huu ulikuwa unaitwa “muziki wa
kufokafoka” kipindi hicho. Nadhani hilo jina halikuwa sahihi, na uliupa mziki huu taswira mbaya. Lakini kwa kuwa ulikuwa ni muziki
mpya, inawezekana hatukujua
jina gani litakuwa sahihi. Hata hivyo, ukiangalia kwa karibu labda neno kufoka halikukosea sana,
kwani kurap ni kama kufoka — lakini neno sahihi la Kiswahili ni kughani.


Muziki huu ulileta mgongano kati ya kizazi chetu na kizazi cha Tabora Jazz kwani muziki huu uliangaliwa kwa tafsiri tofauti Muziki huu ulionekana ukiwa na hiyo dhana ya kufokafoka, na kawaida ya tamaduni zetu, mtoto hamfokei mzazi. Hivyo inawezekana Hip Hop ikaonekana ni muziki unaochochea uasi dhihi ya tamaduni zetu za ndio mzee au zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.
Lakini kwa upande mwingine, hasa ukiangalia katika chimbuko, huu ni
muziki wa watu wanaokandamizwa. Hivyo kipindi kile cha akina II Proud na Wapi Tunakwenda, vijana tulikuwa na madukuduku mengi.

Hip Hop ikafanya vile vile kama ilichofanya Marekani kipindi cha miaka ya sitini na sabini kuwapa wanyonge sauti. Tofauti ilikuwa, huko Marekani iliwapa watu weusi
(hasa vijana) sauti dhidi ya
ubaguzi wa rangi. Hapa Tanzania, suala halikuwa ubaguzi wa rangi, lakini kupigania haki za vijana, dhidi ya uonevu wa polisi, dhidi ya
maisha magumu kwa vijana n.k.

Hivyo ni kweli, mwanzoni kwenye hip hop watu walikuwa wanafoka vilivyo, kwani matatizo yalikuwa mengi na hakuna aliyewasilisha
matatizo hayo ya vijana, au hata kuyapa nafasi ya kusikilizwa. Hilo
linafanana na makundi kama N.W.A. huko Marekani. N.W.A walikuwa wakali, kwani hali halisi yao
ilikuwa ni ngumu sana kipindi hicho, ukilinganisha na sasa.
Sasa kama tamaduni nyingine, Hip Hop imekuwa inakwenda na wakati, pamoja na kuwa kwenda na wakati huko hakujasaidia
sanaa hii moja kwa moja.

Maisha yamebadilika, vijana wa juzi waliokuwa wanapigania haki zao, leo baadhi wamefanikiwa Hivyo maudhui ya mashairi
yamebadilika kwa namna moja
au nyingine.

Kama marekani, vijana wengi wametajirika kupitia mgongo wa Hip Hop, hivyo kuanza kughani kuhusu utajiri wao, kwasababu hawaishi tena kwenye ghettos kama awali.

Hapa Tanzania, kwenye nchi masikini, Hip Hop imekuwa bado
ikitegemewa katika kutetea haki za wanyonge na kuzungumzia
matatizo ambayo yanaendelea kukabili vijana wengi. Pamoja wapo
wachache, waliofanikiwa, wengi wa vijana bado wapo kwenye hali ngumu. Hapa ndipo neno “Hali Halisi” linapoingia katika kuchambua Hip Hop ya Tanzania. Wapo ambao wanahesabiwa kama si wana Hip Hop, kwani mashairi yao hayazungumzii hali halisi ya maisha ya kijana wa kila siku wa
Kitanzania. Hili linaendana na
picha zilizomo kwenye video nyimbo zao. Video nyingi
zinaonekana kushindwa kuakisi
yaliyomo katika tamaduni zetu, bali huakisi zaidi
yaliyomo katika mila na desturi
za tamaduni za Magharibi.
Hili suala la mila na desturi ni
mjadala mwingine, kwani video hizi huonekana kama zinakiuka maadili ya mila na desturi zetu. Mengi yamezungumzwa, bila
kufafanua nini maana ya mila na desturi zetu, kwani kama suala ni
mavazi ya uchi, basi kuna Wamasai ambao hutembea wamevaa lubega tu, bila kuwa na mavazi ya
ndani. Wapo wengine ambao wanaona picha za kwenye video za Hip Hop zinahamasisha maovu; kwa mfano ngono,
kama vile video nyingi za Hip Hop za Marekani. Kama hilo ni tatizo,
basi tunaweza kubadilishakituo cha runinga na
kuweka mduara, ambao naamini ni
tamaduni yetu.Hata hivyo, kuna machache ambayo wapinzani wa Hip Hop hawajakosea sana.

Am in love with hip hop
 
Sasa hyo hip hop ya bongo n Ipi me najua kuna Hip Hop tu sijajua kama kuna hip hop ya Bongo hyo mtu kuvaa vipini n uhuru wa mtu yeyote.
mbaya zaidi mtoa mada hajui kuwa hip hop ni utamaduni, pia izi hereni na kata k imekua ni sehemu ya utamaduni huo.
mtoa mada na wengine wengi wanashindwa kutofautisha 'rap' na 'hip hop'.
 
mbaya zaidi mtoa mada hajui kuwa hip hop ni utamaduni, pia izi hereni na kata k imekua ni sehemu ya utamaduni huo.
mtoa mada na wengine wengi wanashindwa kutofautisha 'rap' na 'hip hop'.

-mkuu, kwa ufahamu wako binafsi, nini maana ya neno ''UTAMADUNI''? na je UTAMADUNI ni universal? Labda tuanzie hapo kwanza. Please usitoe majibu rahisi rahisi.

-Hip-Hop imekuwepo tangu zamani, kwanini uvaaji wa heleni kwa wanaumu & kata K (chu.pi nje) unashamiri sana wakati huu kuliko miaka ya nyuma? na ndo maana kwenye andiko langu nikauliza kwamba je au ndo 'morden' hip-hop hiyo?

Pia kwa faida ya wengine, hebu tuelimishe TOFAUTI kati ya RAP na HIP-HOP, na utueleze ni kipi kati ya hivyo viwili kinaruhusu uvaaji wa heleni kwa wanaume na kata-K. Hapa utakuwa umenisaidia sana.

URGENT QUESTION: Kwa muktadha wa Kiafrika (hususani Kitanzania), wewe unaona ni SAWA kabisa wanaume wavae heleni, wabane vipini, na wavae kata-K (chu.pi nje)?? WEWE unafanya vitu hivi eeh, na kama huvifanyi ni kwanini hufanyi?

-Kaveli-
 
Kiasili muziki wa hip hop huko ndiko ulipoasisiwa na sisi huku tumeupokea kutokana na kuukubali kutokana na uzuri wa maudhui.....lakini wakati huo huo tumeupokea huku tukiwa na tamaduni zetu...na kuvaa vipini kwa watoto wa kiume si sehemu ya utamaduni wetu....ingawa ni uhuru wa mtu binafsi...tunayapenda maudhui yake lakini so kigezo cha kuiga kila wafanyalo wana hip hop hata kama linapingana na tamaduni zetu..na hatimaye kuonekana vituko mbele ya jamii iliyostaarabika...

mkuu umenena vyema sana, na asiye kuelewa hapo basi ana umaandazi kichwani mwake. HIP-HOP tuliipokea kwa misingi na nguzo zake pamoja na maudhui yake, but with ''reservation'' on baadhi ya mambo kama hayo ya uvaaji heleni na kata-K (chu.pi nje).

That's why miaka ya nyuma, ilikuwa ni vigumu sana kumuona mwana-hip hop (Tz) eti kavaa heleni au kata-K. Style hii imeanza kuenea Tanzania (na Africa) kuanzia miaka ya hivi karibuni, na sasa inazidi kushamiri kwa kasi. WHY now and not from the inception of HIP-HOP in Tz? Lazima kutakuwa na kitu behind the scene.

-Kaveli-
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom