Kingine, biography ya Balozi imemtaja Mkapa mara saba, haijatulia. Sio kwamba ina mapungufu ya kitaaluma au uzoefu, ila imejaa uhusiano wake wa karibu na Mkapa, mshutumiwa wa high crimes in high places. Hawa watu kuna vitu fulani vya public relations hawajaamka kuvijua bado. Mkapa sasa hivi ni persona non grata. Hata kama ni ndugu yako inabidi hadharani usimtaje taje Rais Mstaafu anayetaka kushtakiwa kwa kujiuzia migodi. Barabarani Mkapa kazomewa. Vivyo hivyo, mitandaoni Mkapa sio popular, kama Uswahilini ambako akijichanganya bila ulinzi atapigwa matofali!
Bio inasema Balozi alikuwa "personal assistant with added responsibilities" wa Mkapa (wanajua wenyewe hayo majukumu ya ziada). Sasa unafikiri Rais alipokuwa anafanya dili za kununua migodi alikuwa anaenda mwenyewe kwenye minada? Ni hawa "personal assistant with added responsibilities" zisizo julikana ndio walikuwa wanatumwa labda.
Hiyo ni labda. Cha uhakika ni kwamba hata kama walikuwa hawaendi kwenye minada kwa niaba ya Mkapa, at the very least, walijua madili yake. Hawa ndio wanabeba brief case la Mkapa, ndio wanatoa photocopy ma document ya Rais, ndio ma liaison wa idara ya Usalama Ikulu. Hata wasipoenda nae kwenye dili, wanajua amelalia wapi, ameamkia wapi. Kwa hiyo, kama we ni mjanja, huwezi ku advertise kwenye Bio yako hicho ki wasifu cha kubeba mkoba wa master key ya mwizi, kama anavyo shutumiwa. Ni kirekodi kichafu. Huyu balozi lazima atakuwa hana public relations/political savvy masikini. Labda ni mtupu huyu.
Viongozi wetu, masikini weeee!