Twitter verification/blue tick sio issue tena, mluga luga nimekuwa verified

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Huko nyuma kupata blue tick ilikua ni ishu, lazima uwe maarufu sana ama uwe na followers wa kutosha ana kiongozi wa siasa ndio ulikua unapata blue tick. Kipindi hicho kupata blue tick ilihitajika hadi Dollar 6,000 kupata blue tick.

Musk kabadisha huo utaratibu, sasa mtu yoyote anaweza kua na blue tick ikiwa tu atakua tayari kulipia Dollar 11 kwa mwezi.

Musk kasema zile blue tick za huko nyuma zote anazipiga chini maana zilipatikana kwa mtindo wa rushwa na ufisadi mkubwa.

Jana na mimi mluga luga wa huku Makete nimelipia Dollar 11 sawa na Elfu 29 kupata blue tick. Hivyo niwasihi kwamba kama unataka Blue tick wewe lipia tu. Mimi nina mpango wa kuitumia kwa miezi 3 tu kisha naachana nayo.

Karibuni kwenye blue tick wakuu.

Screenshot_20230215_214739_Gmail.jpg
 
Sawa sawa, ngoja tuone za IG, FB na whatsapp green tick verification maana zinachanganya sana watu.
 
Back
Top Bottom