Twite adaiwa 600,000 za Kodi-agomea mazoezi

Twite adaiwa 600,000 za Kodi-agomea mazoezi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
WACHEZAJI wa kigeni wa Yanga wametangaza mgomo mkali kwenye timu hiyo, kutokana na uongozi wa timu hiyo kushindwa kumlipia kodi ya nyumba, beki Mbuyu Twite.
Twite, ambaye ni raia wa Rwanda, amekuwa akidaiwa kodi ya nyumba anayokaa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kwa mwezi anatakiwa kulipa shilingi 600,000, lakini uongozi wa timu hiyo ambao kwa mujibu wa mkataba wake ndiyo unatakiwa kumlipia, umekuwa ukimzungusha.
Beki huyo kisiki alianza mgomo wa kutotokea mazoezini kuanzia juzi Jumatatu na viongozi wa timu hiyo wamekuwa wakitupiana mpira kulizungumzia suala hilo.
Championi ambalo jana lilitinga kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika katika Uwanja wa Loyola jijini Dar es Salaam, lilishangaa kuona kiungo mahiri wa timu hiyo, Haruna Niyonzima naye akikosekana kwenye mazoezi hayo, lakini lilipouliza kwa uongozi, bado halikupata jibu sahihi.
Chanzo cha ndani cha uhakika ambacho kilizungumza na gazeti hili jana, kilisema kuwa kiungo huyo naye amejiunga kwenye mgomo na Mnyarwanda mwenzake, huku Didier Kavumbagu raia wa Burundi na Hamis Kiiza nao wakitajwa kuungana nao siku zijazo.
“Amewaambia anaumwa, kawadanganya, yupo sawa tu, sema hafurahishwi na jinsi viongozi wa klabu wanavyompa ahadi ambazo kwake anaona kama ni dharau,” kilisema chanzo chetu.
“Mimi nimezungumza naye leo (juzi asubuhi), ameniambia kuwa hana tatizo lakini hili suala lake la nyumba anaona kama ghasia kutoka kwa mwenye nyumba, ambapo kila siku wanamuona anaamka na kwenda mazoezini huku kodi akishindwa kulipa, hivyo amekasirika sana.
“Unajua hapa sasa wanachofanya viongozi ni kumweka kocha (Ernie Brandts) katika wakati mgumu, anawakosa wachezaji kama hao katika mazoezi anawezaje kuandaa timu tayari kwa mechi na ratiba inaonyesha Yanga ina michezo migumu hivi karibuni?
“Timu ina wachezaji wengi lakini lazima tukubali Yanga ikiwakosa hao inaweza kuwa katika wakati mgumu kwenye mechi zake na hapo ikitokea timu ikafungwa viongozi watamgeukia kocha na kuwa wakali wakati wao ndiyo wanaomkwamisha.
“Hivi sasa Mbuyu na Huruna wameonyesha kutokukubaliana na hili kwa kujiweka kando lakini wakati wowote usishangae kusikia kuwa hata Kiiza na Kavumbagu nao wakiungana na wenzao, kwa nilivyofuatilia nimeambiwa kuwa kwa upande wa Haruna kodi yake inaisha leo (jana), sasa sijui itakuwaje.”
 
Akilimali alisema ana milioni 750 za usajili, za kodi hana?
 
Ina maana anatakiwa kulipwa mshahara na kulipiwa pango? Kweli Afrika kuna mambo. Afu bado tunakuwa maskini nani anayeandika hii mikataba mtu ulipwe mshahara na ulipiwe kodi ya nyumba?Kweli Bongo kuna mambo.
 
ina maana anatakiwa kulipwa mshahara na kulipiwa pango? Kweli afrika kuna mambo. Afu bado tunakuwa maskini nani anayeandika hii mikataba mtu ulipwe mshahara na ulipiwe kodi ya nyumba?kweli bongo kuna mambo.

ndiyo hivyo pia kwa akina kavumbagu na niyo
 
Ina maana anatakiwa kulipwa mshahara na kulipiwa pango? Kweli Afrika kuna mambo. Afu bado tunakuwa maskini nani anayeandika hii mikataba mtu ulipwe mshahara na ulipiwe kodi ya nyumba?Kweli Bongo kuna mambo.

Manji ajifanya mjuaji sana
 
Manji ajifanya mjuaji sana
moja kati ya watu wajinga katika mpira wa Tanzania anayeungwa mkono na wana Yanga basi ni huyo Manji........hana lololote kulegeza macho tu, hawezi kuiinua Yanga kufikia ngazi ya kimataifa hana tofauti na akili za Mzee Akilimali
 
ina maana anatakiwa kulipwa mshahara na kulipiwa pango? Kweli afrika kuna mambo. Afu bado tunakuwa maskini nani anayeandika hii mikataba mtu ulipwe mshahara na ulipiwe kodi ya nyumba?kweli bongo kuna mambo.

mi so kijan lakin mfanyakazi c ajabu kulipiwa nyumba. Je unafahamu kitu kinaitwa housing benefit
 
moja kati ya watu wajinga katika mpira wa Tanzania anayeungwa mkono na wana Yanga basi ni huyo Manji........hana lololote kulegeza macho tu, hawezi kuiinua Yanga kufikia ngazi ya kimataifa hana tofauti na akili za Mzee Akilimali
muhindi hawezi kuwekeza mahali bila ya masilahi fulani
 
Ina maana anatakiwa kulipwa mshahara na kulipiwa pango? Kweli Afrika kuna mambo. Afu bado tunakuwa maskini nani anayeandika hii mikataba mtu ulipwe mshahara na ulipiwe kodi ya nyumba?Kweli Bongo kuna mambo.

kwani hilo ni tatizo kaka?hayo ni makubaliano ya mkataba tu?hujawahi kuckia mchezaji anapewa nyumba ya kuishi,gari la kutembelea na ulinzi vyote hivyo nje ya mshahara tena hukohuko majuu,hata katika hali ya kawaida mbona wafanyakazi wanaepewa mshahara pia wanapewa na housing allowance every moth...
 
Sijawahi kusikia huu upuuzi... Nachojua majuu hakuna kitu cha kupewa wala bure kila senti unayotengeneza ina mahali pa kutokea. Wachezaji wanagharamia hizo luxury toka katika mishahara yao kama wafanyakazi wengine.
 
mkuu tatizo huku hivyo vitu haitoi klabu wanato watu, mtu akikorofishana na klabu inakua jumba bovu kwa klabu
 
Sijawahi kusikia huu upuuzi... Nachojua majuu hakuna kitu cha kupewa wala bure kila senti unayotengeneza ina mahali pa kutokea. Wachezaji wanagharamia hizo luxury toka katika mishahara yao kama wafanyakazi wengine.

tatizo hata wakitoa wanatoa chini ya uwezo wao matokeo yake mchezaji anaingia fedheha
 
Back
Top Bottom