Twiga stars updates

Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,476
4,250
Jamani leo dada zetu wanacheza na Ethiopia kuwania nafasi ya kushiriki fainali za AWC. Tafadhali tunomba updates kwa wale mlio uwanjani au mnaosikiliza radio....:amen:
 
Sasa ni mapumziko, bao ni bila bila. Hata hivyo Twiga wameonesha kuelemewa kwa kiasi fulani. Tuendelee kuomba dua tupate ushindi.
 
Kocha Boniface Mkwasa alisema kule Ethiopia walifanyiwa hujuma ndio maana wakafungwa.Vipi leo kunani tena?
 
Dua zimekataliwa, tumepigwa 1-0.

Kama ni kweli bac ni muda muafaka kwa Boniface Kuachia wengine wafanye hiyo kazi, maana kwa miaka mingi kaangaika na hiyo timu na inaonekana keshamaliza ujuzi wake wote na hakuna Jipya, hivyo awapishe wengine
 
Nasikitika kusema ngoma ya kitoto haikeshi warudishee majeshi nyuma mwakani tuanze upya na uongozi mpya
 
Nyie TFF, mpeni KAIJAGE hii twiga staz. Mkwasa hana jipya. watoto hawana hata stamina!. Walielemewa muda mwingi yeye anashika kiuno tu!. ile fullbeki yetu ya kulia leo ilipwaya sana. Nawashauri Tuanzishe ligi za soka la kinadada huko mikoani ili hawa wachezaji wawe fiti muda mwingi na sio kufanya mazoezi ya wiki mbili kwa kushiriki mashindano makubwa kama haya.
 
Kama ni kweli bac ni muda muafaka kwa Boniface Kuachia wengine wafanye hiyo kazi, maana kwa miaka mingi kaangaika na hiyo timu na inaonekana keshamaliza ujuzi wake wote na hakuna Jipya, hivyo awapishe wengine

weye wajua boniface ana miaka mingapi na hii timu ambayo kwako unaona ni mingi. Tusiwe na mazoea yta kutaka kufukuzana kwa mitindo ya kushindwa kufuzu tu. Una kumbukumbu nzuri kwamba mwaka jana ni huyuhuyu boniface ndo alitupeleka afrika kusini? Unafikiri kwamba kocha anafukuzwa kwa kuzingatia kigezo cha muda aliokaa na timu? Think twice man. Mi niko disappointed na matokeo tu lakini boniface na vijana wake si wabaya kama unavyotaka watu waamini
 
Nyie TFF, mpeni KAIJAGE hii twiga staz. Mkwasa hana jipya. watoto hawana hata stamina!. Walielemewa muda mwingi yeye anashika kiuno tu!. ile fullbeki yetu ya kulia leo ilipwaya sana. Nawashauri Tuanzishe ligi za soka la kinadada huko mikoani ili hawa wachezaji wawe fiti muda mwingi na sio kufanya mazoezi ya wiki mbili kwa kushiriki mashindano makubwa kama haya.

hata kaijage akipewa hiyo timu kwa maandalizi ya wiki mbili atafanya nini. nakubaliana na wewe kwamba lengo liwe ni kuijenga zaidi timu kitu ambacho matokeo yake hayawezi kuonekana ndani ya muda mfupi tu
 
hata tukibadirisha makocha mala 1000000000,hakuna jipya

kama hamuamini tumleta kocha wa man city ama man u hakuna jipya kama hatutawekeza ktk soka kuanzia chini
 
Back
Top Bottom