Twende wapi kulalamika kuhusu hili?

Twende wapi kulalamika kuhusu hili?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,480
Reaction score
7,443
Mkuu wa nchi analia mbele ya kipaza sauti kuwa wananchi wake wanabambikiwa kodi. Je, waende wapi kudai haki zao?

Wanaoonewa na mahakimu, polisi na watendaji kata waende wapi?

Je, ni lini Tanzania itakuwa taifa lenye kutoa haki?
 
Twende tukalalamike kwa kaka zetu Mabeberu 🐐

Watatusaidia hata kuwaondoa hawa miungu watu wote kwenye jamii yetu.
 
Kanuni ni ile ile tengeneza tatizo halafu uje ulitatue!
 
Si umeshaanzisha mada kama hii hii na ile id yako ya zamani? Acha kujaza server bana.
 
Jamaa ni master wa ku-manipulate watu. Analia ili aonekane yuko upande wa wananchi. Mbona hafanyi mabadiliko kuondoa hayo anayolalamikia kila siku?

Sasa hivi watu ni waelewa wamebaki wanamchora tu, ila watu wanakosa ujasiri wa kumwambia ukweli kwa kuogopa lile kundi lake la watu wasiojulikana.
 
Kanuni ni ile ile tengeneza tatizo halafu uje ulitatue!
Hapana, kwanza siyo kanuni wala hatengenezi tatizo ili aje alitatue bali hayo ni matokeo ya udhaifu wake wa kutambua lipi lifanyike, wakati gani na nani afanye kwa hiyo anaishia kufanya kwa makosa kila analogusa na kuanza kulalamika na kulaumu Wapinzani kuwa wanachelewesha maendeleo mambo yakienda vibaya.

Kutegemea alivyoamka, anatoa agizo linayemfikia analipeleka mbele wateule wake wakipokezana mpaka ngazi ya chini kabisa ya uongozi wa Nchi yetu basi, hapa kazi tu, wote wanafurahi agizo toka juu limefika watangoja lingine. Huwa haandai utaratibu wa mrejesho wa kupokewa na utekelezaji wa maagizo yake bali wananchi wakianza kulalamikia tatizo husika hakumbuki tena alimuagiza nani na anaanza kulalamika mwenyewe na kutengua teuzi za wasiohusika.

Kiongozi ukivibana vyombo vya Habari hata habari nzuri za kukusaidia wewe kutoa uamuzi sahihi utazikosa na wananchi watalalamika na wewe utalalamika na mambo yatabaki palepale.

Mfano: Ile Shule ya Ubungo iliyokuwa na hali mbaya sana Rais akaingilia kati baada ya Chombo cha Habari kuibua, je kweli Mkuu wa Kamkoa kadogo, Mkuu na DED wa Kawilaya kadogo kale hawakuona hali ya Shule ile? Agizo lilipowafikia, wakawa wanaolala wanajenga Shule, lakini kuna Shule ngapi nchini zenye hali mbaya kama ile au zaidi?
 
Ile ni technic wewe jiongeze. Kwa akili yako fikiria vzr
 
Muigizaji mzuri matatizo MENGI yanatokana na maagizo yake na kabadili walio chini yake kufanya kazi kimihemko ili kumfurahisha yeye matokeo yake raia wanaumia na kuanza kulalamika
 
Raisi hajalalamika ,bali aliwaonya TRA kuacha hiyo tabia yakukadiria kodi kubwa
 
Back
Top Bottom