TWAWEZA: Wananchi 8/10 wanapinga uamuzi wa serikali kusitisha matangazo LIVE ya Bunge

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
15 Juni 2016

Wananchi 8 kati ya 10 wanapinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Wananchi 9 kati ya 10 wanasema gharama za kuyarusha matangazo hayo si hoja

15 Juni 2016, Dar es Salaam: Watanzania walio wengi (79%) hawakubaliani na maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kupitia runinga na redio. Karibu wananchi wote (92%) wanaamini kuwa ni muhimu vikao hivyo virushwe moja kwa moja.

Takwimu hizi zimetolewa na Twaweza kupitia muhtasari wa matokeo ya utafiti wake: #BungeLive.

Muhtasari huo unahusisha takwimu zilizokusanywa na Sauti za Wananchi, Utafiti wa kwanza barani Afrika unaotumia simu za mkononi na wenye uwakilishi wa kitaifa. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,815 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 29 Machi na tarehe 12 Aprili 2016.

Miongoni mwa watanzania waliokua wakitazama na kusikiliza vipindi vya Bunge asilimia 42 walikuwa wakiangalia vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja kupitia runinga na asilimia 60 walikuwa wakisikiliza vikao hivyo kupitia redio. Kati ya hawa, asilimia 59 waliangalia vipindi vya Bunge kupitia runinga miezi miwili kabla ya utafiti huu kufanyika, na asilimia 57% walisikiliza vipindi vya Bunge kupitia redio.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa wananchi walikuwa wafuatiliaji wazuri wa vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja. Sababu zao za msingi ni kama zifuatavyo:

Asilimia 46 ya wananchi wanataka kuwafuatilia wabunge wao ili kuona kama wanawawakilisha
ipasavyo.

Asilimia 44 ya wananchi wanasema ni haki yao kufahamu kile kinachoendelea bungeni

Asilimia 29 ya wananchi wanaamini zaidi matangazo ya moja kwa moja kwa sababu wanawaona na kuwasikia wabunge kwa macho na masikio yao wenyewe.

Walipoulizwa na kama ni sahihi kutumia fedha za umma kugharamia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, asilimia 80 ya wananchi wamesisitiza kuwa matangazo hayo yana umuhimu sambamba na huduma nyingine za jamii.

Wananchi walio wengi (88%) wanasema matangazo ya vikao vya Bunge yarushwe moja kwa moja
bila kujali gharama.

Watanzania wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa (asimilia 75) suala la kuruhusiwa kwa
vyombo binafsi vya habari kurusha matangazo ya moja kwa moja ya viako vya Bunge iwapo serikali imeshindwa kuyagharamia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, anasema: “Suala la kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Tanzania limezua mjadala mzito miongoni mwa watanzania.

Kupitia Sauti za Wananchi, tunaona wazi kabisa shauku kubwa ya wananchi ya kutaka kuwaona na kuwasikia wawakilishi wao bungeni kwa macho na masikio yao wenyewe. Je, serikali iko tayari kuyapokea matakwa ya watanzania walio wengi katika jambo hili? Ikibadilisha maamuzi yake na kurudisha matangazo haya itakua ishara nzuri ya nia yake ya kuimarisha uhusiano wa karibu zaidi kati ya wananchi na wabunge wao.”

TWAWEZA 1.png

tWAWWEZA.png

Kawaida ya CCM wakipitisha jambo huwa hawana tabia ya kubadilisha uamuzi!

Maamuzi ya kusitisha #bungelive limeridhiwa na vikao vya juu vya CCM!

CCM wanafahamu hizi kelele za kutaka #bungelive niza muda mfupi hasa ikichukuliwa kuwa bunge la Tanzania halikai kwa muda wote kama yalivyo mabunge kama la Westminster-UK.

CCM wanafahamu baada ya kikao cha bajeti kuisha, hata hizi kelele za #bungelive litaisha na kwa maana hiyo, hata hoja za #bungelive sitasahaulika.

CCM wanafahamu #bungelive siyo hoja ya msingi kwa wapiga kura pamoja na kwamba wapiga kura wangependa kuwepo na #bungelive.

Siasa ni sayansi na sayansi inataka tafiti.
 
Wananchi 8 kati ya 10 wanapinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa
moja ya vikao vya Bunge

Tafiti zingine ni za kijinga.Lengo lake wanataka liwe nini?
Wangefanya utafiti kuwa watu 8 kati ya 10 wasema wabunge hawaongelei matatizo ya wananchi yaliyoko majimboni kwao wawapo bungeni ungekuwa utafiti wa maana ambao ungeamsha wabunge kuanza kuhoji serikali kwa mambo mbali mbali ili kuletelea maendeleo majimboni mwao.

Huu utafiti wa kuonyesha bunge live umekula pesa za watu bure na ni wa kijinga.Nani aliyeidhinisha mali na raslimali zitumike kwa utafiti wa kipuuzi kama huo? Anatakiwa atimuliwe kazini.
 
Hili wala halikuhitaji utafiti wowote bali inaeleweka kuwa huu ulikuwa ni uamuzi wa kujihami wa serikali tokana udhaifu wake na udhaifu wa Rais aliyeingia madarakani kwa njia ya wizi wa kura!!
 
Hivi Urafiki wao na JM umeishia kwenye propaganda za uchaguzi? Naona sasa wanaenda against chama kitavyotaka kusikia! Au ukute hel yake hajalipwa...si wajua matapeli ki JM wamedhulumu wengi sana kipindi cha uvhaguzi.......uliza Prof Lumumba(Lipumba)
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
15 Juni 2016

Wananchi 8 kati ya 10 wanapinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa
moja ya vikao vya Bunge

Wananchi 9 kati ya 10 wanasema gharama za kuyarusha matangazo hayo si hoja

15 Juni 2016, Dar es Salaam: Watanzania walio wengi (79%) hawakubaliani na maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kupitia runinga na redio. Karibu wananchi wote (92%) wanaamini kuwa ni muhimu vikao hivyo virushwe moja kwa moja.

Takwimu hizi zimetolewa na Twaweza kupitia muhtasari wa matokeo ya utafiti wake: #BungeLive.

Muhtasari huo unahusisha takwimu zilizokusanywa na Sauti za Wananchi, Utafiti wa kwanza barani Afrika unaotumia simu za mkononi na wenye uwakilishi wa kitaifa. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,815 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 29 Machi na tarehe 12 Aprili 2016.

Miongoni mwa watanzania waliokua wakitazama na kusikiliza vipindi vya Bunge asilimia 42 walikuwa wakiangalia vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja kupitia runinga na asilimia 60 walikuwa wakisikiliza vikao hivyo kupitia redio. Kati ya hawa, asilimia 59 waliangalia vipindi vya Bunge kupitia runinga miezi miwili kabla ya utafiti huu kufanyika, na asilimia 57% walisikiliza vipindi vya Bunge kupitia redio.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa wananchi walikuwa wafuatiliaji wazuri wa vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja. Sababu zao za msingi ni kama zifuatavyo:

Asilimia 46 ya wananchi wanataka kuwafuatilia wabunge wao ili kuona kama wanawawakilisha
ipasavyo.

Asilimia 44 ya wananchi wanasema ni haki yao kufahamu kile kinachoendelea bungeni

Asilimia 29 ya wananchi wanaamini zaidi matangazo ya moja kwa moja kwa sababu wanawaona na kuwasikia wabunge kwa macho na masikio yao wenyewe.

Walipoulizwa na kama ni sahihi kutumia fedha za umma kugharamia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, asilimia 80 ya wananchi wamesisitiza kuwa matangazo hayo yana umuhimu sambamba na huduma nyingine za jamii.

Wananchi walio wengi (88%) wanasema matangazo ya vikao vya Bunge yarushwe moja kwa moja
bila kujali gharama.

Watanzania wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa (asimilia 75) suala la kuruhusiwa kwa
vyombo binafsi vya habari kurusha matangazo ya moja kwa moja ya viako vya Bunge iwapo serikali imeshindwa kuyagharamia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, anasema: “Suala la kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Tanzania limezua mjadala mzito miongoni mwa watanzania.

Kupitia Sauti za Wananchi, tunaona wazi kabisa shauku kubwa ya wananchi ya kutaka kuwaona na kuwasikia wawakilishi wao bungeni kwa macho na masikio yao wenyewe. Je, serikali iko tayari kuyapokea matakwa ya watanzania walio wengi katika jambo hili? Ikibadilisha maamuzi yake na kurudisha matangazo haya itakua ishara nzuri ya nia yake ya kuimarisha uhusiano wa karibu zaidi kati ya wananchi na wabunge wao.”
 
Ccm wameishiwa siasa wamegawanyika,wamechanganyikiwa,wana depression, sio kwamba hawaoni au hawajui kama wanatunyima haki yakikatiba but wanamuogopa rais wanabakisha siku sio nyingi wamwapishe kuwa mungu wao,

wamesahau when the tough gets going the going gets tough we r not slaves tutawakimbiza na polisi mda sio mrefu we r patient untill we soon gonna loose that patience then waje na maji yao ya washawasha tutawafanya kama kinjeketile this is too much wanazidi kutupima
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hao watafiti wanapoteza hela zao bure,hilo swala lipo wazi sana,halihitaji utafiti,bali utashi wa watawala.Bunge live ni la muhimu.Sisi walipa kodi ndio tunalihitaji,hao wanao lizuia ni kwa maslahi ya nani?
Unaweza kuwafanya watu wajinga kwa mda fulani,si wakati wote
 
Twaweza ni waharibifu wa fedha za wafadhili, hili linahitaji utafiti kujua kama wananchi wanapinga?, na sio kupinga tu tumechukizwa sana na udikteta huu
 
Leo Twaweza watasifiwa sana kwakuwa wamefanya kinachopendwa na UKAWA!
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
15 Juni 2016

Wananchi 8 kati ya 10 wanapinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa
moja ya vikao vya Bunge

Wananchi 9 kati ya 10 wanasema gharama za kuyarusha matangazo hayo si hoja

15 Juni 2016, Dar es Salaam: Watanzania walio wengi (79%) hawakubaliani na maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kupitia runinga na redio. Karibu wananchi wote (92%) wanaamini kuwa ni muhimu vikao hivyo virushwe moja kwa moja.

Takwimu hizi zimetolewa na Twaweza kupitia muhtasari wa matokeo ya utafiti wake: #BungeLive.

Muhtasari huo unahusisha takwimu zilizokusanywa na Sauti za Wananchi, Utafiti wa kwanza barani Afrika unaotumia simu za mkononi na wenye uwakilishi wa kitaifa. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,815 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 29 Machi na tarehe 12 Aprili 2016.

Miongoni mwa watanzania waliokua wakitazama na kusikiliza vipindi vya Bunge asilimia 42 walikuwa wakiangalia vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja kupitia runinga na asilimia 60 walikuwa wakisikiliza vikao hivyo kupitia redio. Kati ya hawa, asilimia 59 waliangalia vipindi vya Bunge kupitia runinga miezi miwili kabla ya utafiti huu kufanyika, na asilimia 57% walisikiliza vipindi vya Bunge kupitia redio.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa wananchi walikuwa wafuatiliaji wazuri wa vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa moja kwa moja. Sababu zao za msingi ni kama zifuatavyo:

Asilimia 46 ya wananchi wanataka kuwafuatilia wabunge wao ili kuona kama wanawawakilisha
ipasavyo.

Asilimia 44 ya wananchi wanasema ni haki yao kufahamu kile kinachoendelea bungeni

Asilimia 29 ya wananchi wanaamini zaidi matangazo ya moja kwa moja kwa sababu wanawaona na kuwasikia wabunge kwa macho na masikio yao wenyewe.

Walipoulizwa na kama ni sahihi kutumia fedha za umma kugharamia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, asilimia 80 ya wananchi wamesisitiza kuwa matangazo hayo yana umuhimu sambamba na huduma nyingine za jamii.

Wananchi walio wengi (88%) wanasema matangazo ya vikao vya Bunge yarushwe moja kwa moja
bila kujali gharama.

Watanzania wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa (asimilia 75) suala la kuruhusiwa kwa
vyombo binafsi vya habari kurusha matangazo ya moja kwa moja ya viako vya Bunge iwapo serikali imeshindwa kuyagharamia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, anasema: “Suala la kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Tanzania limezua mjadala mzito miongoni mwa watanzania.

Kupitia Sauti za Wananchi, tunaona wazi kabisa shauku kubwa ya wananchi ya kutaka kuwaona na kuwasikia wawakilishi wao bungeni kwa macho na masikio yao wenyewe. Je, serikali iko tayari kuyapokea matakwa ya watanzania walio wengi katika jambo hili? Ikibadilisha maamuzi yake na kurudisha matangazo haya itakua ishara nzuri ya nia yake ya kuimarisha uhusiano wa karibu zaidi kati ya wananchi na wabunge wao.”
Utafiti huu hauna maana kwa watawala. Kama ungesema wananchi wanaunga mkono uamuzi wa serikali wa kutonesha bunge " live" vyomba vyote vya habari ndio ingekuwa habari kuu.

Twaweza utafiti wenu ni sawa kumpigia mbuzi gitaa. Kwa vile "mshavuta" tafuteni fitna nyengine muifanyie utafiti mpate " kuvuta" tena. Tafiti aina hii Afrika hususan kusini mwa jangwa la sahara, zinakuwa hazina maana.
 
Back
Top Bottom