Twanga Pepeta yapata 'silaha' mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Twanga Pepeta yapata 'silaha' mpya

Discussion in 'Entertainment' started by Lutala, Feb 8, 2011.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, itawatambulisha wanamuziki wake wapya kwenye onesho lao litakalofanyika Februari 14, mwaka huu kwenye ukumbi wa Da’ West Park Tabata, Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, amesema, siku hiyo ya Februari 14 ambayo huadhimishwa na wapendanao duniani kote, watatumia kutambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni wakiwemo wanenguaji.

  Lakini hakuwataja wanamuziki wala wanenguaji hao, ingawa alisema wanatoka kwenye bendi mbalimbali maarufu hapa nchini.

  “African Stars Entertainment (ASET) ni taasisi ya muziki ambayo kazi yake ni kuandaa na kukuza wanamuziki.

  “Ninawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili waone silaha zetu mpya pamoja na rapu zetu mpya,” alisema Asha.

  Mratibu wa onesho hilo Joseph Kapinga alisema kutakuwa na zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba na staili yake ya Kisigino.

  Alisema watapiga nyimbo zilizomo kwenye albamu yao waliyorekodi na mwanamuziki nguli kutoka Congo, Bozi Boziana.

  Nyimbo nyingine zinazotamba ni Mwana Dar es Salaam , Shida ni Darasa, Rafiki Adui, Mwisho wa Ubaya ni Aibu, Nazi Haivunji Jiwe na Sitaki Tena.
   
Loading...