Twamuomba Mengi arudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Twamuomba Mengi arudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 29, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Baada ya Mengi kuwatosa wananchi wanyonge waliokuwa wanamuona ni alama (symbol) ya kupambana na mafisadi, hasa baada ya ujasiri wake wa kuwataja mafisadi papa, sasa wanyonge tutampata wapi mwingine kama yeye?

  Kwa umiliki wake wa vyombo muhimu vya habari – radio, TV na magazeti – Mengi alikuwa ni mtu muafaka sana katika kazi hiyo, na wengi tuliona jinsi mafisadi walivyokuwa wakipata kiwewe kutoka kwake. Lakini ghafla ameamua kuwatosa, na vyombo vyake vya habari havigusii kabisa masuala ya ufisadi.

  Alipowataja mafisadi papa, CCM na serikali yake walimpa msukosuko mkubwa sana lakini alipata faraja kutoka kwa wananchi ambao walikuwa nyuma yake. What went wrong?

  Hata katika kipindi cha ITV cha mapitio ya magazeti, hayasomwi magazeti yale yenye habari kuu ukurasa wa mbele kama inahusu ufisadi wa viongozi wa chama tawala.

  Tunajua yeye ni CCM na anapenda kuona chama hicho kinashinda – ingawa twashangaa ni kitu gani kinamfanya aamini kama CCM inaweza kupambana kweli na ufisadi, kama tunavyoona sasa hivi jinsi JK anavyowakumbatia waziwazi mafisadi.

  Lakini kupambana katika vita vya haki ilipasa kuwa muongozo wake, hata kama vita hiyo ni ajenda kuu ya chama cha upinzani – Chadema. Kwa nini anawaona Chadema adui – na hivyo kuyatelekeza mapambano yenye lengo jema – na hivyo kuwatosa mashabiki wake?

  Tunaomba Mzee Mengi ajifikirie tena kuhusu hili. Kuna hatari naye ataambiwa ni fisadi kama vile wale aliowatuhumu miaka miwili iliyopita.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hata mimi limenishangaza hilo hazungumzii kabisaaa ufisadi kuchagua viongozi waadilifu
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kumuomba mengi kupambana si vizuri kwani mwanamapinduzi wa kweli haombwi bali hujitoa mhanga
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,285
  Trophy Points: 280
  Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji wakweli wanaoumizwa na umasikini wa Watanzania, hivyo hupigania maslahi ya taifa.
  Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wachumia tumbo, wakiwemo baadhi ya wale makamanda, waliokuwa wanapigania nafsi zao.
  Na kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji maslahi, miongoni mwao ni wafanya biashara, ambao wanapambana na ufisadi sio kwa chuki za ufisadi, bali kwa maslahi ya biashara zao. Hawa ndio hutaja majina ya watu, huku wakiisifia CCM na kuisuport kwa hali na mali.
   
 5. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  :confused2:
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ndo maana daima namuunga mkono mzee Pengo , kadinali. aliposema kuwa kuna watu wanapiga kelele za ufisadi kwa kuwa wao wamekosa fursa za kufisadi katika serikali .
  Pengo aliongea jambo ziito sana, ndo hawa Kina Mengi na makuwadi wenzao akina Sitta. woote ni Genge na Mafisadi, Huwezi kuupinga Ufisadi ukiwa ndani ya ccm, haiwezekani, ni unafiki, bora ukanyamaza kimya.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  ....Mpambanaji maslahi!
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mbona mi naye namwona fisadi tuu, uwekezaji wote huu si ufisadi? mimi siku zote huwa naamini msemo wa kiswahili usemao matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. maneno ya watu majukwaani hayanitatizi kabisa.
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe Pasco una kesi ya kujibu hapa JF, kuna wakati ulisema hivi:

  Bado unasimamia analysis yako?
   
 10. simon41

  simon41 Senior Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Always rich people use poor as commodity,everyone should have to wakeup:eek2:
   
 11. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Taasisi isiyo ya kiserikali, hivi karibuni imelitaja gazeti la Mwananchi kuwa ndio Gazeti pekee lililoandika habari za kweli na za bila upendeleo. Huu ni moja ya ushaidi juu ya kutokuwepo kwa fairness katika kuripoti habari hasa nyakati hizi za kampeni.

  Tatizo ni uwoga kwamba kama sinta kuwepo upande wao watanigeuka. lakini kwa kufanya hivyo ni kuwanyima fursa na Haki wananchi wa Tanzanaia, na pia ni kukiuka misingi ya kazi za kiuandishi wa habari ambayo husisitiza Fairness, Haki na Ukweli katika kuhabarisha.

  Nashangaa ni kwanini mtu ujipendekeze! Huko nyuma aliwahi kulala mika sana amechezewa rafu katika kuinunua iliyokuwa inaitwa Kilimanjaro Hotel, na alilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha umma kwa kutokuandika ukweli juu ya sakata lile. Leo ameshasahau.. ukweli hataki kuundika, amerudi kulekule alikokuwa anakupinga, huu ni unafiki katika media.
   
 12. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Kwa definition yako ya ufisadi, wafanyabishara wote ni mafisadi?
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mnategemea MENGI awakubalie ombi lenu?
  alipoonesha msimamo wake against mafisadi, serikali walipiga za utosi mpaka akawa anakosa za kulipia mshahara watu wake. ameamua kulegeza mkanda na anapiga hesabu zake vizuri ili oktoba atoke vipi.

  Lakini ni huyu huyu aliyetuonesha picha za rwanda na burundi siku moja kabla ya kupiga kura mwaka 1995 ili tuuchukie upinzani. He is not in favor of sauti ya wengi he is in favor with making more cash and reputation
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mengi na ITV yake pamoja na magazeti yake ni wakuogopwa kama ukoma, anzeni kukumbuka sakata lake la uuzwaji wa Kilimanjaro Hotel jinsi alivyozidiwa kete halafu akapiga kelele saaaaaana watu tukamwonea huruma weeee kumbe mafisadi wenzie walimzidia kwa kuweka cha pembeni kwa dau kubwa kuliko lake, mzee mbaya sana yule jamani amulikwe sana ingawa anatumia media zake kujionyesha kuwa yu pamoja na walalahoi
   
 15. m

  magee Senior Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  i wonder ni lini tutaachakunyosheana vidole na kuchukua hatua wenyewe,ni lini tutaacha laumiana na kusubiri mpaka mtu afanyekitu kwaajili ya ukombozi wetu wenyewe,you are likely sailing in the same boat with mengi cause what i see mengi si mwanamapinduzi wa kweli kama wewe ulivo na wengi kwenye jukwaa hili walivo maana daima tunaishia ongea tu na kutokuchukua hatua yoyote......mengi aliwataja mafisadi then what aliwapeleka mahakamani?hii ilitosha kuonesha kuwa si mwana mapinduzi huyu.its high time kwa kila mzalendo na mwana mapinduzi kusimama katika zamu yake mwenyewe.
  I love tanzania!!!!!
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Siku ile RA anajibu mapigo alitoa na ushahidi wa maandishi wa jinsi Mzee Mengi alivyo fisadi nyangumi na akawapa PCCB. Nini kilifuata?
   
 17. M

  Msavila JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mengi ni mfanyabiashara na kwa sasa kula iko CCM
   
 18. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  By 2015. Hairuhusiwi m2 kumiliki vyombo vya habari zaidi ya kimoja. Mnalijua hili??
  Nafikiri Kikwete akishinda itabidi huu mkakati ufutwe ili kumpa Favaour Mengi. Ni mwana ccm Mwenzetu na ametoa Mchango mkubwa sana katika kufanikisha ushindi wa JK.
  Slaa akishinda watalia wengi!! Simaanishi wengi relative to TZ population, namaanisha wengi relative to Mafisadi Percentage.
   
 19. M

  Malembeka Shija Member

  #19
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona mnadanganyana sana hapa....kwanza kabisa hii jamiiforum inaonekana ni ya chadema kila ukisoma ni hadithi za DK SLAA...hamna kingine...na mnafanya watu wapumbavu sana wakati dunia nzima inajua R.a. mengi chadema...kwenye msafara wa mamba na chadema wamo...hapa kwakweli haki haitendeki kila kitu kibaya mnachosema nyinyi ni ccm...mbona hamuyataji mazuri walioya fanya ccm?.naona hapa kinacho fanyika ni brainwashing..hahaha mtu mzima hatishiwi nyau...HATUDANGANYIKI...CCM OYEEE,KIKWETE OYEEE
   
 20. D

  Dash Member

  #20
  Oct 13, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
Loading...