TV yangu jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV yangu jamani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Straight corner, Apr 8, 2011.

 1. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari za siku wana JF?
  Leo asubuhi tulikuwa tunaangalia kipindi cha 'Tuongee Asubuhi' kinachorushwa Star TV, mada ilikuwa MSWADA WA SHERIA YA KUTUNGA KATIBA MPYA. Mojawapo ya wageni alikuwa Simbachawene (Mb) na Bw. Marcos kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadam.

  Katika majadiliano huyu Bw. Marcos akasema mswada unazuia kuongelea mambo kadhaa kama muungano, urais n.k. lakini huyu mbunge akakanusha na kusema watu wanaelewa vibaya kwani hawajazuiwa kujadili mambo ya muungano, urais ... na hapo ndo ulikuwa mwisho wa kuangalia mjadala kwani rafiki yangu aliyekuwa pembeni akinywa chai alirusha kikombe kwenye screen upande wa yule mbunge na kuvunja screen!

  Nilipomuuliza kulikoni alisonya na kuuliza kwamba inamaana Majaji na wanasheria woote wanaosema mswada unazuia kujadili mambo hayo ni wajinga? Hatimaye akaishia kuniomba radhi na kusema Viongozi wanatuona wapumbavu mno!

  My take:
  Kama sikosei Madaktari wana chama chao ambapo akitokea dactari amekiuka maadili yao wanamchukulia hatua, hivi hawa wanasheria wenyewe hawana cha kuwawajibisha wanapowahadaa wananchi makusudi? Maana inadaiwa huyu mbunge naye ni mwanasheria.
   
 2. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama ni kweli, that was too far nashauri umpeleke huyo ndugu yako aliyevunja tv hospitali akapimwe akili. unaweza kuchukulia kwamba ni hasira lakini huo ni ugonjwa na umefikia kiwango kibaya. Please act very soon, akiwa na silaha huyo anaweza kukudhuru wewe mwenyewe siku ukisema jambo ambalo hakubaliani nalo
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mmmh!! chijana....screen ya TV kuvunjwa na kikombe cha chai???? Ni TV gani hiyo na imetengenezwa wapi? Isijekuwa ya Kinyanambwa B

  BTW, pole sana kwa machungu yote...hii ndiyo TZ zaidi ya uidhanivyo
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  akimpeleka hospitali wote wawili hawatarudi ila watapelekwa mirembe maana huwezi kumpima akili mtu anayegombana na TV kwa sababu majibu yake tayari yanajulikana.
   
Loading...