Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Tunapenda kutoa mwaliko kwa wageni 20 tu watakaohudhuria katika kipindi kipya kitakachorushwa TBC1. Wageni lazima wawe wameguswa sana na tatizo la madawa ya kulevya na wawe tayari kuleta changamoto katika kipindi au kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo. Tafadhali thibitisha kuhudhuria kwako kupitia barua pepe: Mtsimbe@micronet.co.tz
Kipindi cha kwanza kitarushwa tarehe 24-11-2013 na Mada itakayoongelewa na "Tatizo la Madawa ya Kulevya na Ufumbuzi Wake"
Wageni wa kipindi wanaotarajia kuwepo ni:
Wale wote wenye michango ya msingi au maoni au ufumbuzi au maswali mnayopenda wahusika waulizwe pia mnaweza kuniandikia mapema.
TV Talk Show itajulikana kama "Wake Up & Change" au "Amka na Badilika" na ni kipindi kitakachorushwa kila wiki siku ya jumapili usiku.
1. Madhumuni ya Kipindi
a) Kubadilisha mitazamo ya watazamaji ili iwe mitazamo chanya zaidi kwa mambo mbalimbali pamoja na kuwahamasisha kubadili tabia na kuchukua hatua katika kukabiliana na matatizo.
b) Kutafuta na kutoa majibu kwa masuala muhimu yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi au utatuzi wa matatizo na pia kujibu maswali yanayohusiana na mada husika kutoka kwa watazamaji waalikwa.
c) Kukifanya kipindi kama jukwaa la majadiliano katika mambo muhimu ya kijamii na kitaifa na kuhamasisha mabadiliko chanya.
2. Ubunifu wa Kipindi
Kipindi kimebuniwa ili kuleta majadiliano yatakayoleta hisia kwa wote watakaohusika katika mjadala na pia watazamaji. Jambo hili ni muhimu zaidi ili kuleta matokeo chanya kwa wote wanaoangalia kipindi. Kwa ujumla kipindi kimebuniwa kutatua matatizo mbalimbali ya watu binafsi, familia, jumuiya, jamii na taifa kwa ujumla huku kikitoa mikakati na mipango ya kutatua matatizo na kuwahamasisha watazamaji kubadilika. Studio itakoyorekodi vipindi hivyo pia imetengenezwa katika hali ya ubunifu na kupendezesha kipindi.
3. Mada Zitakazoongelewa
Kutakuwa na mada mbalimbali na mpya ambazo zitaongelewa kila wiki. Mada hizi zitategemea utafiti utakaofanywa na mamombi ya watazamaji ili mradi tu liwe ni tatizo ambalo linaigusa jamii au watu wengi. Mfano wa mada hizi ni pamoja na biashara; mahusiano; kazi na ajira; kilimo; Wanawake, rushwa; madawa ya kulevya nk.
4. Mpangilio wa Kipindi:
a) Kuwakilisha mada husika na kuitambulisha huku takwimu zikitolewa toka chanzo cha kuaminika.
b) Kulielezea tatizo husika katika uhalisia wake na kuwafanya watazamaji waone ukubwa wa tatizo
c) Kulijadili tatizo na kulichambua kwa kina huku maswali yakijibiwa
d) Kuwakilisha majibu na ufumbuzi wa tatizo
e) Kuhamasisha watazamaji wazinduke/waamke, kubadilika na kuchukua hatua ya kutatua tatizo kama lilivyo ainishwa.
f) Kipindi kitaendeshwa kwa mtindo wa majadiliano yenye hisia kali na hivyo kupeleka hisia kwa watazamaji pia.
5. Wageni wa Kipindi na Waalikwa Watazamaji:
a) Mwakilishi wa walioathirika jambo linaloongelewa
b) Mwakilishi aliyeweza kushinda tatizo linaloongelewa
c) Mwakilishi kutoka chombo au vyombo vya serikali vinavyotakiwa kushughulikia tatizo
d) Mwakilishi wa asasi inayojihusisha na tatizo
e) Mwanataaluma anyeweza kuchambua jambo husika na kuleta ufumbuzi
f) Waendesha kipindi wawili wa kike na wa kiume
g) Msanii atakeyetumbuiza siku husika kuwakilisha ujumbe husika
h) Wageni watakaoalikwa kutazama kipindi na kuuliza maswali kama wawailishi wa watazamaji wa TV
6. Walengwa wa Kipindi:
a) Vijana
b) Wanafunzi
c) Wafanyabiashra
d) Wanandoa
e) Na wananchi wote kwa ujumla.
7. Urushaji wa Kipindi na Upatikanaji katika DVD
a) Kipindi kitakuwa kinarekodiwa na kurushwa katika Luninga siku ya Jumapili saa 3 hadi saa nne usiku kwa muda wa saa moja. TBC1.
b) Baadhi ya vipindi vitavyoonekano kama ni mafunzo muhimu na adimu kwa watu na jamii vitarekodiwa katika DVD na kusambazwa na kuuzwa kwa bei nafuu kwa walengwa.
c) Wasambazaji watakaopenda kuuza DVD hizi wanakaribishwa pia kutuandikia.
8. Wadhamini wa Kipindi
Makampuni au mtu atakayependa kukidhamini kipindi na kuleta matangazo au kununua airtime anakaribishwa awasiliane nasi kupitia mtsimbe@micronet.co.tz

- Kamishna wa tume ya Madawa ya Kulevya
- Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Madawa ya Kulevya
- Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali DPP
- Mkemia Mkuu wa Serikali
- Daktari anayetibu waathirika
- Mh. Esther Bulayo mbunge aliyewakilisha mada husika Bungeni
- Ray C – Msanii na Balozi wa Madawa ya kulevya. Atatumbuiza pia.
- Kitale: Msanii anayeigiza kama teja
- Asasi inayojihusisha na kusaidia walioathirika na madawa ya kulevya