Elections 2010 TV stations na Blogs zina ubia na CCM?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Wadau,

Kampeni ndio zimeshaanza rasmi.

Lakini nashangazwa na baadhi ya Tv stations na blogs maarufu hapa nchini kuonyesha habari za CCM tu kana kwamba ndio chama pekee cha Siasa hapa nchini.

Kwa mfano ukitembelea Blogs maarufu za Michuzi, Mjengwa nk zimepambwa na picha za kijani.

Na kwa TV stations nazo ukiachilia mbali TBC1 ambayo ilishamtangaza JK kuwa ni Mshindi kabla hata ya Kampeni kuanza (Haina sauti kwa CCM).

Chanel Ten ndio kama ya CCM.

Radio stations nazo ndio kabisa.

CCM imeingia Ubia na vyombo hivi? Au hivi vyombo ni vinajipendekeza tu kwa chama tawala?
Hivi ni haki kwa vipasha habari hivi kuelemea chama kimoja tu?
 
Mkuu,

Kama CCM wanatuma info zaidi kuliko vyama vingine (naongelea blogs) unatarajia nini? Wasiziweke simply kwakuwa wataonekana wanaipendelea CCM?

Let's be fair; vyama vya upinzani vinakalia habari sana, hata sielewi kwanini havitoi ushirikiano kwa blogs; wanataka wafuatwe ilhali CCM wanakuwa na waandishi wanaofuatilia na kutuma habari haraka kwa vyombo vyote vya habari.

Tarajia makubwa zaidi; CCM watalipia matangazo kwenye blogs, sasa wasiweke kwakuwa wapinzani watalalamika? Kwanini upinzani wasilipie japo kidogo? Hivi kweli hawana ruzuku ya kuweza kumudu kutangaza japo kwenye tovuti/blog nne au tano tu?
 
Mkuu
Mhhh! Jibu hili limekaa kisanii kidogo. Umeongelea upande mmoja wa chama kupeleka au kununua muda na nafasi kwenye chombo cha habari. Hilo mimi sina tatizo nalo.

Tatizo linakuja pale vyombo vyenyewe vinapoongelea CCM tu kama habari ya kawaida: news or report. Coverage yao ni unproportionately and unfairly huge.
 
kwani waadnishi wa habari ndo wanafuata /wanatafuta habari au CCM ndio inayowapelekea habari??? sihitaji kufanya analysis ya kisomi katika hili kwa kuwa jibu ni rahisi sana,blogs na TV zimenunuliwa na CCM.....
 
Back
Top Bottom