Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Habari zenu marafiki,
Leo ningependelea tuzungumzie kuhusu ulezi wa watoto wetu,taifa lijalo na majukumu yetu kama wazazi.Mzazi ni mfano wa kuigwa kwa mtoto.Kile anachofanya mzazi kiwe kizuri au kibaya ndicho mtoto anaona ni mfano maridhawa kwake.Tulio wengi tunawadharau watoto,kwamba wana uelewa mdogo,lakini si kweli watoto wanauelewa wa hali ya juu na wanakumbukumbu maridhawa.Watoto walio wengi wapo very manipulative.Katika umri mdogo kabisa atajaribu kukufanyia kila visa kukujaribu na kukupima.Lakini wewe kama mzazi unatakiwa uwe na msimamo juu ya maamuzi yako na kanuni unazomuwekea.Na anakujaribu wewe kama mzazi kwasababu wewe ndio mtu alokuzoea na anaekuamini kuliko wote.Na ndio maana mtoto huyohuyo ambae anakufanyia vituko wewe akiwa na wengine anakuwa na adabu na hekima ya hali ya juu.Jinsi mtoto unavyomlea ndivyo jinsi anavyokuwa,tuwalee watoto katika misingi bora kwa manufaa yao ya baadae,wakati huohuo tusiwanyime haki zao za kuwa watoto.
Nafurahishwa sana na uhalisia/ukweli(honesty) na innocence ya watoto,their curiosty to learn and discover new things,its amazing.
Inanishangaza na kunisikitisha mno ninaposikia mzazi anamuadhibu au kumchapa mtoto wa miaka 3 au 5?Haswa kwa makosa ambayo ukifikiria ni wewe mzazi wa kujilaumu na kujihukumu.Kama una stress zako za maisha tafadhali tafuta suluhu ya kuzimaliza bila kuhusisha watoto.Hivi nyinyi wenzangu mnalichukuliaje suala hili?mnaona ni sahihi mtoto mwenye umri huo kuadhibiwa kwa viboko?na wewe kama mzazi mtoto wako wa miaka 5 akileta utovu wa adabu unachukulia hatua gani?utampa adhabu gani?Utamkanya?
Karibuni wapendwa tujadili suala hili!