PreGE2025 Tuzo za Samia Kalamu Awards Superdome Mawaziri washindana kutoa zawadi kwa washindi, mmoja apewa boti ya milioni 50

PreGE2025 Tuzo za Samia Kalamu Awards Superdome Mawaziri washindana kutoa zawadi kwa washindi, mmoja apewa boti ya milioni 50

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo May 05,2025 ameongoza Wadau mbalimbali kwenye ugawaji wa Tuzo za umahiri kwa Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari Tanzania, zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam.

Tuzo hizo zimepewa jina la ‘Samia Kalamu Awards’ na zinaendelewa kutolewa muda huu ambapo Viongozi, Wageni waalikwa na Wanahabari mbalimbali wamehudhuria

Kazi 1,131 za kihabari ziliwasilishwa katika Tuzo za SamiaJumla ya kazi 1,131 za kihabari ziliwasilishwa na wanahabari ili kushindania tuzo 38 zinazotolewa katika vipengele mbalimbali kwenye tuzo mpya za Samia Kalamu Awards kwa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Joyce Shebe amesema, kazi hizo zimechujwa na Majaji wabobezi wa Tasnia ya Habari na kupatikana kazi 85 zilizoingia fainali.

Akitoa taarifa ya TAMWA kwenye hafla ya utoaji Tuzo hizo, Shebe amesema, kati ya kazi hizo 85 zilizoingia fainali ni kazi 38 tu ndio zitashinda tuzo ya Samia Kamalu Awards.

Shebe amesema, tuzo hizo pia zinakuwa na kipenge mahsusi ya Tuzo ya Habari za Nishati Safi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kampeni ya kitaifa na kimataifa ya matumizi ya Nishati safi.

Kituo cha Redio cha Taifa 'TBC Taifa' na kituo cha Runinga cha TBC1 wachaguliwa kama vituo bora vya maudhui ya Redio na Televisheni kama washindi wa tuzo za Samia Kalamu Awards mwaka 2025.

Wanahabari 254 wamepatiwa mafunzo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amesema mchakato wa maandalizi ya tuzo za Samia Kalamu Awards yamewezesha Waandishi wa Habari 254 kupata elimu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi na ubora wa kazi za waandishi.

Akitoa taarifa ya TCRA kama Muandaaji mwenza wa Tuzo hizo, Dkt. Jabiri amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) walifanya utafiti na kugundua kuwa wanahabari wengi wanakosa sifa ya kutambua habari muhimu zinazohusiana na maendeleo na ndio maana wakaanzisha mafunzo hayo.

Amesema mafunzo hayo yalifanyika kwa waandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na baada ya mafunzo hayo wameona mabadiliko makubwa katika kazi za Uandishi na taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya Habari.

WASHINDI

  • Mwandishi Bora Sekta ya Elimu - Agnes Mbapu, TBC (Kashinda Milioni 5, kiwanja chenye hati na Cheti cha ushindi huo)

  • Mwandishi Bora Wa Mazingira - Vitus Audax, Nipashe - Amezawadiwa Tsh Milioni 5 na ziara ya mafunzo nchini Ufaransa na kutazama mechi za Ligi Kuu kwenye jukwaa la VVIP

  • Mwandishi mahiri wa Habari za Elimu - Silvano Kayera, Mlimani TV (Silvano amekabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni Tano,laptop,vitabu na cheti ambavyo amekabidhiwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda.

  • Mwandishi Bora wa Habari za fedha na uchumi - Francis Kajubi, The Guardian (Kashinda milioni 5, atalipiwa masomo katika fani ya fedha na uandishi wa habari za fedha,na yeye na chombo chake watapata fursa ya kuandika habari za bajeti ya serikali mwezi ujao, ataandikiwa bondi iliyoandikwa kwa jina lake ya Sh.milioni 10, na katika taasisi za wizara ya fedha kuna nafasi ya ajira atapelekwa kwenye mchakato wa kupata nafasi ya ajira.

  • Chombo cha habari mtandaoni kinachoongoza kuripoti matukio - Millard Ayo

  • Mwandishi Bora Habari za Uchukuzi - Abela Msikula, TSN (Kashinda Milioni 5, Laptop Mpya na Tiketi 10 za SGR atakazotumia ndani ya mwaka 1

  • Mwandishi Bora Habari za Afya - Ismail Kawambwa , TSN

  • Mwandishi Bora wa Habari Sekta ya Ardhi na Makazi - Agnes Mbapu, TBC

  • Mwandishi Bora wa Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum - Samson Paskal Mgelwa, Muungwana Blog

  • Mwandishi Bora Habari za Kilimo - Issa Kwisa Njole Mbyale, Highland FM (Ameshinda Milioni 5 na kupewa kiwanja cha Ekari 10 Dodoma)

  • Mwandishi Bora Habari za Madini - Dotto Dosca Kwilasa, Malunde Media (Ameshinda Milioni 5 na amepewa madini aina ya Ruby)

  • Mwandishi Bora Habari za Maji - Adam Gabriel Hando (Kashinda Milioni 5, Laptop Mpya, Bili ya maji ya miezi 3 na atachimbiwa kisima na serikali)

  • Mwandishi Bora Habari za Maliasili na Utalii - Innocent John Anselemi ( Kashinda Dola 2500, Ubalozi wa Utalii Kwa Mwaka 1 na trip ya Utalii kwa mwaka mmoja)

  • Mwandishi Bora Habari za Mifugo na Uvuvi - Mussa Yusuph Musa (Kashinda Milioni 5, Mtamba 1 mwenye mimba, Kizimba kwenye ziwa Victoria)

  • Mwandishi Bora Sekta ya Nishati - Nyamguma Mahamud, Mlimani FM (Kashinda Milioni 5, Jiko la Umeme la Induction Cooker, Umeme bure sehemu anayoishi kwa mwaka 1)

  • Mwandishi Bora Sekta ya TEHAMA na Ubunifu - Mariam Maulid Matundu, Dodoma FM (Kashinda Milioni 5, Laptop Aina ya HP, Fiber ya bure ya TTCL kwa mwaka mmoja, mafunzo ya wiki moja ya taarifa binafsi, atafunguliwa sanduku la posta, kama atapenda kuanzisha Online Media atapewa leseni ya miaka 3, mafunzo ya AI atakayopata nchi Marekani)

  • Mwandishi Bora sekta ya Uchumi wa Bluu - Mackriner Siyovelwa, Crown FM (Kashinda Milioni 5, atapewa Boti ya Uvuvi ya Milioni 50, trip ya kwenda Zanzibar ndani ya siku 10)

  • Mwandishi Bora Sekta ya Ujenzi - Mathias Canal Said, Wazohuru Media (Kashinda Milioni 5, atazunguka nchi nzima kufanya coverage ya Miradi ya Ujenzi)

  • Mwandishi Bora Sekta ya Utamaduni na Michezo- Sanura Renatus Athanas, Nipashe (Kashinda Milioni 5, Laptop Mpya, safari ya kutembelea vyombo vya habari nchini Ufaransa, tiketi ya kutazama msimu mzima wa Ligi Kuu Uwanja wa Benjamini kwa ngazi ya VVIP)

  • Mwandishi Bora sekta ya uwekezaji - Evans Rehema Mwaikyema, Azam Media (Kashinda Milioni 5, Ushauri wa Bure TIC kuhusu namna ya kuwekeza, safari 3 na Waziri nje ya nchi zinazohusu Uwekezaji, safari na Waziri ndani ya nchi kwa mwaka mmoja)

  • Mwandishi Bora Sekta ya Vijana - Gilfred Arnold Msengezi, Azam Media (Kashinda Milioni 5, Laptop Mpya, Atafanya kazi kwenye shughuli mbalimbali za Wizara ya Vijana)

  • Mwandishi Bora Sekta ya Viwanda na Biashara - Rehema Amri, Azam Media (Kashinda Milioni 5, Ofa ya kusoma CBE, ataenda kwenye Japan Expo, Smartphone ya kisasa, Mafunzo ya SIDO)

  • Afisa Habari Mahiri wa Serikali - Joshua Alinanuswe Sengo, Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Kashinda Milioni 5, Nafasi ya kuhudhuria kongamano la Kiswahili Ufaransa, Tiketi za Mwaka mzima kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Ubalozi wa Yanga au Simba)

  • Chombo Cha Habari Mahiri (Magazeti) - Nipashe (Kimeshinda Milioni 5, Watahudhuria Kongamano la Kiswahili Ufaransa, Safari ya Mafunzo Marekani)

  • Chombo cha Habari Mahiri cha Kijamii (Bara) - Dodoma FM (Redio imeshinda Laptop, Milioni 5 na pikipiki)

  • Chombo cha Habari Mahiri cha Kijamii (Zanzibar) - Tumbatu FM ( Kipando, Tsh Milioni 5 na Computer)

  • Chombo cha Habari Mahiri Mtandaoni - Wazohuru Media (Wameshinda Milioni 5 na mfanyakazi mmoja ataenda Japan kuhudhuria Japan Expo)

  • Redio Bora Kitaifa - TBC Taifa
  • Kituo Bora Cha Runinga - TBC 1
  • Gazeti Linalopatikana Kwa Uhakika - Mwananchi
  • Mwandishi bora wa habari za kutetea watu wenye ulemavu - Zungu kelvin Raphael
 
Inawezekana kabisa huyu wa Tanzania ndio anayehudhuria Matamasha ya wasanii Kila kukicha.

Mfalme apatapo Wafitini na Washaurí wabaya , Taifa hua katika Majonzi.

Fikiria MTU kama Kikwete, ambaye mtoto wake ni Waziri, Mke Mbunge, atamshauri nn Samia zaidi ya kumwambia 'Unaupiga mwingi?'
 
Nasubiria hafla uzawadia wale wenye ubunifu wa kisayansi uliofanyika hapa nchini na umeleta tija kwa Taifa kiuchumi na kiteknolojia.
 
Taifa lenye furaha
1000032984.jpg
 
Sisi tuna majonzi ya ndugu zetu wanaopotea kila uchao huku Tanganyika/Bara...
Nyie endeleeni na sherehe zenu.Mungu ni wa wote!
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo May 05,2025 ameongoza Wadau mbalimbali kwenye ugawaji wa Tuzo za umahiri kwa Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari Tanzania, zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam.

Tuzo hizo zimepewa jina la ‘Samia Kalamu Awards’ na zinaendelewa kutolewa muda huu ambapo Viongozi, Wageni waalikwa na Wanahabari mbalimbali wamehudhuria

Kazi 1,131 za kihabari ziliwasilishwa katika Tuzo za SamiaJumla ya kazi 1,131 za kihabari ziliwasilishwa na wanahabari ili kushindania tuzo 38 zinazotolewa katika vipengele mbalimbali kwenye tuzo mpya za Samia Kalamu Awards kwa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Joyce Shebe amesema, kazi hizo zimechujwa na Majaji wabobezi wa Tasnia ya Habari na kupatikana kazi 85 zilizoingia fainali.

Akitoa taarifa ya TAMWA kwenye hafla ya utoaji Tuzo hizo, Shebe amesema, kati ya kazi hizo 85 zilizoingia fainali ni kazi 38 tu ndio zitashinda tuzo ya Samia Kamalu Awards.

Shebe amesema, tuzo hizo pia zinakuwa na kipenge mahsusi ya Tuzo ya Habari za Nishati Safi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kampeni ya kitaifa na kimataifa ya matumizi ya Nishati safi.

Kituo cha Redio cha Taifa 'TBC Taifa' na kituo cha Runinga cha TBC1 wachaguliwa kama vituo bora vya maudhui ya Redio na Televisheni kama washindi wa tuzo za Samia Kalamu Awards mwaka 2025.

Wanahabari 254 wamepatiwa mafunzo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amesema mchakato wa maandalizi ya tuzo za Samia Kalamu Awards yamewezesha Waandishi wa Habari 254 kupata elimu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi na ubora wa kazi za waandishi.

Akitoa taarifa ya TCRA kama Muandaaji mwenza wa Tuzo hizo, Dkt. Jabiri amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) walifanya utafiti na kugundua kuwa wanahabari wengi wanakosa sifa ya kutambua habari muhimu zinazohusiana na maendeleo na ndio maana wakaanzisha mafunzo hayo.

Amesema mafunzo hayo yalifanyika kwa waandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na baada ya mafunzo hayo wameona mabadiliko makubwa katika kazi za Uandishi na taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya Habari.

Agnes Mbapu apata tuzo
Mtangazaji na Mhariri wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Agnes Mbapu ameshinda tuzo ya Samia Kalamu Awards katika kipengere cha Ardhi na Makazi ambapo Makala yake ya Anwani za Makazi imemwezesha kushinda tuzo hiyo.

Akikabidhi tuzo hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga amesema, Wizara hiyo imetoa fedha, shilingi Milioni 5, kiwanja chenye hati na Cheti cha ushindi huo.

Agnes Mbapu kupitia kipindi cha Kishindo cha Awamu ya 6 amekuwa akimulika na kutoa elimu kuhusiana na Matumizi ya Ardhi na Makazi.

Amesema, moja ya eneo ambalo wameligusia kwenye mafunzo hayo ni matumizi ya Akili unde (AI) na uandishi wa Habari zenye tija kwa manufaa ya Taifa.

Hadi mwaka uishe Zitatolewa tuzo nyingi sana
 
WAshamjulia mpenda misifa kila kutu sa100 sa100 sa100 sa100
Na yeye anaona diiili kumbe wanafki wanamchora hajui
sa100 akitoka madarakani hizo tuzo zitakuwa ndio mwisho

sijaona umuhimu wake zaidi ya kupeana zawadi kama rushwa, hao wanajipanga kwaajiri ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom