Tuzo ya heshima kutoka kwa Sir Richard Turnbull, Gavana wa mwisho Tanganyika. Nimeona Tuzo hii na inabidi Serikali kufatilia

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Wanasema kuishi na watu kuona mengi. Kuna mzee wangu ambaye nilinunua shamba kanda ya ziwa kwa wasukuma. Kupiga stori naye na mda mrefu kunieleza kuwa babu yake alikuwa mtawala wa mwisho wa machifu kipindi hiko kanda ya ziwa ikiitawaliwa na Tabora kwa upande wa kahama anadai ilikuwa inaitwa West Tabora zone kama sijakosea.

Babu yake alikuwa anaitwa Chief Iphanda aliyetawala 1907-1963 na kufariki 1970.

Utawala huu ulikuwa 1946 maeneo yaa Ngogwa chiefdom.

Kuleta habari hii ni kwa sababu ya kuona medali hii na ana historia nyingi.

Mzee huyu baba yake alikuwa waziri wa fedha kipindi cha Nyerere marehemu Sazia.

Nikipata mda nitawaletea historia maana sehemu naliyopo kuna umbali


 
Interesting....tuzo ilitoka kwa Richard kwenda kwa nani?
Mzee kama ana khali mbya atakua kaukalia uchumi
 
Hiyo inaonekana ni dhahabu yenyewe
 
Unawapa mzee wa watu shida tu,wahuni wataenda kusaka hizo dhahabu zimjeruhi mzee wetu.
 
Bila shaka hii ni pure gold

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
Babu...
Sidhani kama hiyo ni dhahabu.

Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes niliziona medali alizotunukiwa na Waingereza - "War Medal," na "Burma Star," kwa ajili ya kupigana katika Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945).

Nimeiona vilevile medali aliyotunukiwa na Tanzania katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru.

Zote hizi si dhahabu.

Naweka picha ya Ally Sykes akiwa amevaa medali zake ambazo wote yeye na kaka yake walipata na nyingine yeye alipata lakini ndugu yake hakupata ya "marksman," yaani medali wanayotunukiwa askari wenye shabaha vitani yenye alama ya mkasi.

Naweka pia medali ya Mwenge wa Uhuru.



 
Asante sana kwa kuleta uzi huu.
Mtemi wa mwisho hapo alikua anaitwa Andrea Mhanda( sio Iphanda ulivoandika)
Mheshiwa Sazia hakuwahi kua Waziri wa Fedha, alikua Waziri wa Ujenzi.
 
Asante sana kwa kuleta uzi huu.
Mtemi wa mwisho hapo alikua anaitwa Andrea Mhanda( sio Iphanda ulivoandika)
Mheshiwa Sazia hakuwahi kua Waziri wa Fedha, alikua Waziri wa Ujenzi.
Vipi kuhusu huyu Mtemi omabala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…