Tuzike maiti kaburini au tuchome? Changamoto

Tuzike maiti kaburini au tuchome? Changamoto

Hizi hapa faida nyingine;
Maiti ikichomwa hautapata adhabu ya kaburini

Maiti ikichomwa watu hawata pata usumbufu wa kuja kufagilia kaburi lako

Maiti ikichoma wachawi hawata pata msukule kama ulikufa kwa ushirikina
Umetisha Brother Kaka.

Kitendawili kingine ni Ufufuo wa Wafu,

Kipindi cha nyuma miaka ya Elfumbili Mwanzoni kulikuwa na filamu moja ya kinaijeria Maudhui yake Makubwa ilikuwa ni Namba 666 au Mpinga kristo/Chapa 666.

Huwezi Uza wala nunua bidhaa bila ya kupokea chapa 666,Mambo ya Ufunuo Wa Yohane Agano Jipya.

Sasa hiyo filamu Mwanzoni kabisa anaanza Pastor ananyakuliwa akiwa anahubiri na baadhi ya waamuni na wengine wakibaki wakiduwaa,

Ghafla pia inaonekana Wafu wanafufuliwa katika Makaburi Wanapanda hewani na mavazi Meupe kama Theluji.

Sasa swali la kizushi linapanda hewani vipi Jamiizile zichomazo Maiti kisha jivu kutupiwa baharini..? ?
 
Kipindi nikiwa Mdogo Tulikuwa Tunakwenda kushuhudia Mazishi ya baadhi ya Jamii za kihindi wao walikuwa wanachoma Moto Maiti hapa nazungumzia Tabora barabara ya kwenda Skonge.

Tulikuwa Tunakwenda kutazama bure kabisa na wao walikuwa wanaruhusu,Unasikia Mifupa na kichwa vinapasuka kwa Wingi wa Moto,Kama ushawahi kushuhudia filamu za Bollywood Zile scene za Mazishi unaweza pata picha kwa mbali basi sisi tulikuwa tunashuhudia live bila chenga.

Kusema kweli huu utamaduni unanivutia sana...Kuchoma Maiti safi sana, labda changamoto kubwa itakuwa katika Vitendea kazi vya shughuli hii.

Nadhani hili Nalitafakari katika Wosia Wangu nikikata Pumzi nitiwe kiberiti.

Kwangu wazo hili Naunga Mkono hoja.
 
Ni vizuri maiti ikachomwa alafu majivu yakazikwa hii itasaidia sana katika utunzaji wa maeneo ya ardhi
 
Kama ni kuogopa kumaliza ardhi basi tufanye moja katika mawili
Aidha tuchimbe gorofa kwenda chini ya ardhi au tuzike kwa kusimama Lakini kuchoma Hapana tuwaachie wahindu tu
 
Hakuna ubishi kwamba Watanzania tunaongezeka kwa kasi sana. Wakati tunapata Uhuru ilikadiriwa kuwa nchi ilikuwa na watu milioni tisa. Sasa tupo karibu milioni 60. Sawa na population ya Uingereza ingawa wao wana eneo dogo.

Katika mambo tuliyofanikiwa ndani ya miaka 57 ya Uhuru ni kuzaliana!! Watu hawazai kama njiwa ama mbuzi.....

Ni wazi kwamba wakati watu wakiongezeka kila kuficha, ardhi imebaki kuwa ileile sq km 945000 na ushei hivi. Ongezeko la watu weeengi vs ardhi isiyoongezeka imekuja na matatizo mengi ikiwemo mtihani kuhusu mahala pa kuzika wafu.

Maeneo ya kuzika yamekuwa yakimalizika kwa kasi na hili nalo ni time bomb ambalo litalipuka kama tusipopata suluhisho mbadala.

Upo mjadala duniani na hapa nchini hivi sasa juu ya kuopt kuchoma marehemu wetu kama njia ya kutunza mazingira.

Kuzika na kuchoma kote ni mjadala mzito. Kuchoma maiti kunatisha na kunaweza kuwa a weird kind of burying wapendwa wetu. Lakini kumbuka huyo ameshakufa hatarudi tena. Ukifa huna tofauti na gogo ambalo hatma yake ni kuchomwa.

Kuchoma kunaweza kusaidia sana kupunguza madhila yanayotokana na ugomvi wa maeneo hasa Serikali inapobadilisha matumizi ya ardhi na wafiwa kulazimika kuhamisha makaburi!!

It's so painful kuhamisha mifupa ya ndugu yenu mliyemzika miaka mingi iliyopita. Ni sawa na msiba kuanza upya.

Adha hii ingeweza kuepukwa kama maiti ingechomwa, majivu yake kutupwa baharini au mtoni na mengine kiasi familia ikabaki nayo kabatini kwa kumbukukumbu. Shrine?

Kuzika kaburini kuna gharama kubwa na watu wanashindana kwa hili. Kuchoma ingeweza kuwa suluhisho.

Najua watu watasema huu sio utamaduni wetu. Hata hivyo sio mbaya kuiga. Tunaiga mambo mengi ya hovyo. Hebu tujaribu kuiga yenye tija pia.

Sijui dini zinasemaje juu ya hili. Lakini tunajua mitume wengi walizikwa kaburini. Hata hivyo haina maana kwamba na sisi lazima tuzikwe kaburini.

Kumbuka mitume waliishi zamani sana na wakati wao ardhi haikuwa shida. Hivi sasa mambo ni tofauti sana. Sio kila kitu kilichofanywa au kusemwa na mitume ni applicable leo. No.

Kuna haja ya kufikiria kuchoma sasa kama namna bora zaidi ya kuwasitiri maiti na au kuhifadhi mazingira.

Ukichomwa hakuna atakayefukua kaburi lako.
Ukichomwa hakuna atakayekojolea kaburi lako. Hakuna atakayewanga juu ya kaburi lako.

Hakuna gharama za jeneza kama alivyochomwa Wangari Mathai wa Kenya na Margaret Thatcher wa Uingereza.
Ardhi bado ipo ya kutosha, ukitaka kuchoma unaongeza uharibifu wa mazingira kwa maana ya kukata kuni, hafu sisi idadi ya vifo ni kubwa.
 
Nawaza hapa kama tungekua tuna choma moto wafu tangu miaka ya 1900 saivi tungekua na misitu kias gani?
Je kama tusingekua tunalima, tungekua na misitu kiasi gani.

Maana ukienda kijijini tangu wanze kuzikana hata ekari kumi hazijatimia, ila kilimo kimekula sana misitu.
 
mleta mada umeeleza vizuri, na nmewahi kushirikisha jamaa zangu juu ya hili nami ningependa kufanyiwa aina hiyo ya mazishi, ni nzuri na inatusahaulisha maumivu ya kuachwa na wapendwa wetu kwa haraka, inapunguza ushirikina na imani ya mizim, misukule, ibada za wafu na kuokoa ardhi hasa mijini, usumbufu wa kufanyia usafi na ghalama za jeneza na ujenzi wa makaburi na uhifadhi wake,
Unaweza kuwapo utaratibu mzuri tu wa uchomaji ama ziwepo taasisi maalum kwa hilo, hasa hospital.
 
mleta mada umeeleza vizuri, na nmewahi kushirikisha jamaa zangu juu ya hili nami ningependa kufanyiwa aina hiyo ya mazishi, ni nzuri na inatusahaulisha maumivu ya kuachwa na wapendwa wetu kwa haraka, inapunguza ushirikina na imani ya mizim, misukule, ibada za wafu na kuokoa ardhi hasa mijini, usumbufu wa kufanyia usafi na ghalama za jeneza na ujenzi wa makaburi na uhifadhi wake,
Unaweza kuwapo utaratibu mzuri tu wa uchomaji ama ziwepo taasisi maalum kwa hilo, hasa hospital.
Hili swala kuchoma mwili, marehemu, sheria ya nchi haikatazi, wewe unaweza andika usia ukifa uchomwe na ukachomwa.

Kumbuka Serikali, haingilii imani za watu, Hapa Tanzania watu hivi leo unajua watu wanachomana.

Mkitaka iwe Sheria, inamaana Serikali, itakua inavunja haki ya kuabudu.
Hili la Ambaruty, mataifa yametushupalia, alafu tuanzishe lingine Tena.
 
Kwahiyo wanaochoma hawana mafundisho ya Mungu? (india, China, Banladeshi, Korea, Japan nk)
Unajui imani, imani yao, inwaelekeza hivyo, ya kwangu hainielekezi kuchomwa.
Tena ikibidi nikazikwe kijijini kwetu.
 
Mimi nadhani ni vyema maiti zikapelekwa kwa vyuo vya afya kama muhas, kairuki n.k ili ziweze kutumiwa ktk kujifunza kwa vitendo. Nchi za mbele kuna body donation program, mtu willingly anajaza form ya kudonate mwili wake utumike kwa medical training anapofariki. Hii pia itasaidia kupunguza usumbufu wa kuzikana lakini pia itakuza medical fields.
Empty set kabisa
 
Tanzania bado kubwa sana hata tukiwa milioni 100 bado panatutosha hata 200.
 
kwa nchi masikini wacha tuendelee kuzika, tukianza kuchoma moto itakua uchochoro wa kupotezea ushahidi, hususani polisi
Hata nchi tajiri wanaendelea kuzika, nadhani kuna madhehebu matano yanayofuata utaratibu wa kuchoma miili ya waliofariki (Sio wakristo na waislamu). Lakini pia namna tunavyowaaga wapendwa wetu waliotangulia ni sehemu ya utamaduni wa jamii husika.
 
Tuna ardhi kubwa sana, tatizo ni watu kujenga maeneo ya makaburi na kutaka kuzika katikati ya mji
 
Back
Top Bottom