Tuzike maiti kaburini au tuchome? Changamoto

Tuzike maiti kaburini au tuchome? Changamoto

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Hakuna ubishi kwamba Watanzania tunaongezeka kwa kasi sana. Wakati tunapata Uhuru ilikadiriwa kuwa nchi ilikuwa na watu milioni tisa. Sasa tupo karibu milioni 60. Sawa na population ya Uingereza ingawa wao wana eneo dogo.

Katika mambo tuliyofanikiwa ndani ya miaka 57 ya Uhuru ni kuzaliana!! Watu hawazai kama njiwa ama mbuzi.....

Ni wazi kwamba wakati watu wakiongezeka kila kuficha, ardhi imebaki kuwa ileile sq km 945000 na ushei hivi. Ongezeko la watu weeengi vs ardhi isiyoongezeka imekuja na matatizo mengi ikiwemo mtihani kuhusu mahala pa kuzika wafu.

Maeneo ya kuzika yamekuwa yakimalizika kwa kasi na hili nalo ni time bomb ambalo litalipuka kama tusipopata suluhisho mbadala.

Upo mjadala duniani na hapa nchini hivi sasa juu ya kuopt kuchoma marehemu wetu kama njia ya kutunza mazingira.

Kuzika na kuchoma kote ni mjadala mzito. Kuchoma maiti kunatisha na kunaweza kuwa a weird kind of burying wapendwa wetu. Lakini kumbuka huyo ameshakufa hatarudi tena. Ukifa huna tofauti na gogo ambalo hatma yake ni kuchomwa.

Kuchoma kunaweza kusaidia sana kupunguza madhila yanayotokana na ugomvi wa maeneo hasa Serikali inapobadilisha matumizi ya ardhi na wafiwa kulazimika kuhamisha makaburi!!

It's so painful kuhamisha mifupa ya ndugu yenu mliyemzika miaka mingi iliyopita. Ni sawa na msiba kuanza upya.

Adha hii ingeweza kuepukwa kama maiti ingechomwa, majivu yake kutupwa baharini au mtoni na mengine kiasi familia ikabaki nayo kabatini kwa kumbukukumbu. Shrine?

Kuzika kaburini kuna gharama kubwa na watu wanashindana kwa hili. Kuchoma ingeweza kuwa suluhisho.

Najua watu watasema huu sio utamaduni wetu. Hata hivyo sio mbaya kuiga. Tunaiga mambo mengi ya hovyo. Hebu tujaribu kuiga yenye tija pia.

Sijui dini zinasemaje juu ya hili. Lakini tunajua mitume wengi walizikwa kaburini. Hata hivyo haina maana kwamba na sisi lazima tuzikwe kaburini.

Kumbuka mitume waliishi zamani sana na wakati wao ardhi haikuwa shida. Hivi sasa mambo ni tofauti sana. Sio kila kitu kilichofanywa au kusemwa na mitume ni applicable leo. No.

Kuna haja ya kufikiria kuchoma sasa kama namna bora zaidi ya kuwasitiri maiti na au kuhifadhi mazingira.

Ukichomwa hakuna atakayefukua kaburi lako.
Ukichomwa hakuna atakayekojolea kaburi lako. Hakuna atakayewanga juu ya kaburi lako.

Hakuna gharama za jeneza kama alivyochomwa Wangari Mathai wa Kenya na Margaret Thatcher wa Uingereza.
 
Tamaduni nyingi zinaheshimu Sana mwili wa marehemu..na hata hivyo sio utu kumchoma marehemu..Mimi nadhani bado tuendelee na taratibu zile zile ila makaburi yakifikisha miaka Mia tunaweza kupasafisha tukaendelea na shughuli
 
Ila hili ni wazo zuri sana. Kila kata ingejenga Tanuri maalumu, mtu akidanja anapigwa kiberiti mchezo umeisha.
 
Mi mwenyewe natamani nikifa wanichome moto tuu maana wachawi hawakawii hata kubeba viungo vyako buree ilihali nishakufa au watu kukojolea kaburi lang na vingine vingi tuu.... Nafikiri kuna haja ya hii hoja kuipeleka mbele zaidi ili kuwe na option mtu anapofariki aidha azikweau achomwe kulingana na mahitaji ya marehem aliyotaka pindi akiwa hai... [emoji41][emoji41]asante mtoa mada kwahili pia.
 
Nimeshawahi kusikia kwamba pamoja na kuwa na eneo kubwa la ardhi kiasi hicho ni 20% tu Ndiyo linatumika. Tz mapori kibao
 
Duuuh sitamani kuona mwili wa mtu wangu wa karibu ukichomwa moto aheri kuzika tu
 
Nawaza hapa kama tungekua tuna choma moto wafu tangu miaka ya 1900 saivi tungekua na misitu kias gani?
 
Mimi nadhani ni vyema maiti zikapelekwa kwa vyuo vya afya kama muhas, kairuki n.k ili ziweze kutumiwa ktk kujifunza kwa vitendo. Nchi za mbele kuna body donation program, mtu willingly anajaza form ya kudonate mwili wake utumike kwa medical training anapofariki. Hii pia itasaidia kupunguza usumbufu wa kuzikana lakini pia itakuza medical fields.
 
Dah hili nalo ni wazo? Sasa mkuu hivi tuseme kwa siku moja watanzania 100 hufariki dunia kwa siku 10 tutakuwa na maiti 1000 huko Muhas na Kairuki wanaenda kula nyama za wafu?
Mimi nadhani ni vyema maiti zikapelekwa kwa vyuo vya afya kama muhas, kairuki n.k ili ziweze kutumiwa ktk kujifunza kwa vitendo. Nchi za mbele kuna body donation program, mtu willingly anajaza form ya kudonate mwili wake utumike kwa medical training anapofariki. Hii pia itasaidia kupunguza usumbufu wa kuzikana lakini pia itakuza medical fields.
 
Dah hili nalo ni wazo? Sasa mkuu hivi tuseme kwa siku moja watanzania 100 hufariki dunia kwa siku 10 tutakuwa na maiti 1000 huko Muhas na Kairuki wanaenda kula nyama za wafu?
Tuna vyuo vingi vya udaktari... ila hata kama maiti ni nyingi dead bodies can be preserved for future use.
 
kwa nchi masikini wacha tuendelee kuzika, tukianza kuchoma moto itakua uchochoro wa kupotezea ushahidi, hususani polisi
 
Back
Top Bottom