Tuweni waangalifu na wageni, awekewa dawa kwenye maji, watoto wawa vilema wengine wapoteza maisha

THT

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
737
869
Habari zenu wapendwa,

Kuna kisa kilimtokea jirani yangu nikaona si vyema kukaanacho kimya, nikaona ni vyema niwashirikishe nanyi wenzangu ili mpate kujifunza pia kuchukua tahadhari kuna jirani yangu alibarikiwa kupata watoto nane, wakiume watano wa kike watatu na wote walikuwa na uwezo mzuri tu darasani.

Mji wao ulikuwa ni mji usio isha wageni kwasababu baba yao alifanikiwa kimaisha na alikuwa na ndugu wengi waliokuwa wakimtegemea kijijini kwa hiyo mara kwa mara ndugu walikuwa wakipishana kwa safari za kuja kumsalimia. Mara watoto wanne waliugua kwa pamoja, mara waishiwe damu mara washindwe kutembea watembelee fimbo wakapelekwa mara BUGANDO mara DDH BUNDA tatizo halikuisha.

Wakajaribu kwa waganga lakini wapi, mwishowe wakaenda kumwona shehe mmoja aliyeaminika hapo mkoani kwao, akawaambia ni ndugu yao mmoja aliwawekea dawa kwenye maji ya kunywa, akawambia atawatibu ila watabaki kuwa vilema maisha yao yote baada ya muda watano walifariki wakabaki watatu na wazazi pia walifariki. Wawili ni wale ambao hawakuugua kabisa na ni wazima mpaka leo, mmoja ni trafiki na mwingine ni waziri mkubwa kabisa katika serikali ya Magufuli. Watatu ni kilema mpaka leo nae ndiye mwalimu aliyenifundisha mimi.

FUNZO: Tuwe waangalifu tusimwamini mtu yeyote kupita kiasi hii inaweza kuathiri mlolongo mzima wa maisha yetu na familia zetu kwani si kila mtu anafurahia mafanikio tuliyonayo, tutabaki kufirisika kwa kumalizia pesa zetu kwenye kutibu magonjwa.

Nawasilisha
 
1470311046478.jpg
 
Kwa kifupi hakuna watu hatari kama ndugu...Mara nyingi watu waliofanikiwa kimaisha huwakwepa sana binadamu,na pia huonekana wana roho mbaya,hawa nawaunga mkono manake wanaepuka mengi.
tena wengine ukiwasaidia pesa kidogo tu wanaenda kuzichezea utashangaa kila kitu kinagoma biashara zinapata majanga na hasara kila siku. ni kumtegemea mungu tu maana bila yeye hatuwezi
 
tena wengine ukiwasaidia pesa kidogo tu wanaenda kuzichezea utashangaa kila kitu kinagoma biashara zinapata majanga na hasara kila siku. ni kumtegemea mungu tu maana bila yeye hatuwezi
umegusa penyewe.
 
  • Thanks
Reactions: THT
tena wengine ukiwasaidia pesa kidogo tu wanaenda kuzichezea utashangaa kila kitu kinagoma biashara zinapata majanga na hasara kila siku. ni kumtegemea mungu tu maana bila yeye hatuwezi
Umeongea ukweli kabisa ndugu yangu. Wanakuchezea. Watu wabaya. Mimi naunga mkono kujitenga na watu kwa kiasi fulani yaani tuwe na mipaka usiwaamini asilimia mia moja.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Nina ushuhuda wa kweli na mkubwa sana kuhusu Uzi huu nikisema mengi naweza onekana muongo.... Ila katika yote tumuweke Mungu mbele daima hasa tukiwa na wageni majumbani kwetu.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom