Tuweni makini sana na ulimi/ndimi

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,101
34,050
ULIMI, ni kiungo katika miili ya wanyama na ndege, kwa binadamu ulimi mbali na kazi zingine kama kuonja ladha pia humwezesha kutamka maneno au kuimba nyimbo.

Ulimi una madhara makubwa sanaaa kuliko kiungo chochote kile kwa mwanadamu.

Dhambi ya kwanza ya uasi ilisababishwa na ulimi.

Dhambi nyingi sana huanzia kwenye macho (kutamani) kisha ULIMI (kushawishi).

Mfano: Rushwa, Wizi, Zinaa, Dhulma,vifo, Utapeli, uonevu, kusababisha uchochezi, Kuvunja Urafiki, kuvunja Ndoa, Mauaji ya halaiki n.k

KUMBUKA: Mtu mpumbavu sana akikaa kimya mbele ya halaiki, kamwe upumbavu wake hautofahamika na ataonekana mwenye hekima.

LAKINI
Mwerevu au tumwite Msomi akiwa mropokaji/muongea hovyo mbele ya watu anaonekana na kueleweka ni Mpumbavu au kichaa kabisa.

Biblia imeonya sanaa zaidi ya mara 40 kuhusu kuwa makini sana na ULIMI na Maneno ya Vinywa vyetu.

Kukaa kimya ni silaha kubwa sana hata kwa maadui wa wazi au wanaokusema vibaya, hasa pale unapojua makosa yao kisha huwaulizi, wakija kugundua kuwa unajua maovu yao watasurrender kwako. Take it from me.

Mara nyingi kukaa kimya hata kwa wanaojua mengi ila wakatulia (Introverts) ni BUSARA na HEKIMA.

Ipo mifano mingi tu ya watu maarufu waliotamka mabaya juu ya binadamu wenzao baadaye wakaathirika wao.

Pia wapo wanaojitamkia wenyewe maneno yenye kukatisha tamaa na kuvunja moyo kisha wanaathirika nayo seriously.

Lakini pia ulimi ukitumika kiusahihi unasaidia kuonya na kubariki

Kuna makala na vitabu vya "Power of the tongue" vinaeleza pia mengi zaidi kuhusu matamshi yetu.

Tuwe makini sana na ndimi zetu.
 
Back
Top Bottom