Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,695
- 149,921
Nakubaliana kabisa kuwa wafanyakazi hewa wanatia hasara kubwa sana Taifa hili ambapo kwa miaka 5 tu serikali inapoteza zaidi ya bilioni 600 kwa kulipa wafanyakazi hewa kama alivyobainisha Raisi leo hii.
Lakini tujiulize kwenye swala la malipo ya sitting allowance za wabunge kwa kipindi hicho hicho cha miaka 5, serikali inalipa fedha kiasi gani?
Sitting allowance kwa mbunge mmoja kwa siku ni shilingi 200,000.Sasa tufanye hesabu kwa wabunge wote ambao jumla yao ni wabunge 397 kama sikosei (niko tayari kurekebishwa hiyo figure) kwa siku tu wanalipwa kiasi gani.
200,000 x 397=79,400,000(milioni sabini na tisa na laki nne kwa siku)!!
Hii ni hela wanayolipwa wabunge hawa kwa siku moja tu.Sasa piga mahesabu kwa jumla ya vikao vyote vya bunge kwa mwaka mmoja wanalipwa shilingi ngapi hawa watu alafu uzidishe hiyo figure utayopata kwa miaka 5.
Kumbuka Bunge la Bajeti tu kwa kila mwaka huchukua karibu miezi mitatu.Pia kama sikoei, kuna Bunge la wiki mbili ambalo huanza mwezi January mwishoni na lingine kama hilo ambalo hukaa mwezi November kila mwaka.
Anaetetea sitting allowance za wabunge atupe na justification ya malipo haya ambayo binafsi nayaona hayana tofauti na malipo ya watumishi hewa.