johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,149
Ameenda kulalamikia sehemu isiyo sahihi!Kama binaadamu mwenye sifa ya kukasirika,kufurahi,kuridhika,kuhuzunika,kulalamika,kuona umepuuzwa au kudharauliwa au kutengwa na kunyimwa haki zako,UNGEKUWA NI LISSU usingefanya au kusema kama yeye?
- Ni Mbunge wa Upinzani na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni
- Alishatoa taarifa ya 'kufuatiliwa' na kutishiwa uhai wake
- Akashambuliwa akiwa kazini maeneo ya Bunge yenye ulinzi wa kutosha.
- Kwa mujibu wake na familia yake,Bunge halijawahi kugharamia matibabu yake nje ya nchi kwa kile kinachotajwa kama kutofuata utaratibu unaohusu matibabu ya Wabunge.
- Kwa mujibu wake,hakuna kiongozi yeyote wa Bunge aliyemtembelea hospitalini kuanzia Nairobi hadi Ubelgiji pamoja na kuwa yeye ni 'mgonjwa wa Bunge'
- Kwa mujibu wake,hadi Sasa,hakuna yeyote aliyekamatwa,kushikiliwa au kushtakiwa kwa 'shambulio' lake.
- Kwa mujibu wake,mipango ya kumvua Ubunge wake kwa 'utoro' inasukwa ili kutekelezwa.
- Lissu ni Mwanasheria anayejua haki na wajibu,hasa haki na wajibu wake.
- Alishambuliwa akiwa ni Rais wa TLS,Mbunge wa Singida Mashariki-CHADEMA,Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA.
- Yeye na familia yake wamekuwa wakifuatilia stahiki zake,za kimatibabu,kwa Mamlaka husika kama Bunge bila mafanikio.