Tuwe tunawahi

Tuwe tunawahi

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
438
Reaction score
67
Padri mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia sherehe kubwa. Katika sherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba ya shukurani ya kumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya, mbunge alichelewa kufika, Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri mweshimiwa mbunge. Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi, aliongea. "Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara ya kwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha. Mtu wa kwanza kabisa kumuungamisha alinishangaza sana. kwani alisema amemwibia bosi wake TV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, amezini na jirani yake, na pia katembea na house girl wake. Nilidhani watu wote wa kanisa hili wanatabia kama hizi, kumbe baadaye nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawana dhambi za ajabu ajabu". Mara mheshimiwa mbunge akawasili, padri akakatisha maongezi na mbunge akaanza kuhutubia. "Ndugu wapendwa, ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana kwani padri huyu alipokuja hapa, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kwenda na kuungama kwake... (Fundisho-tuwe tunawahi)
 
kwani umesahau kuwa tupo AFRIKA tena TANZANIA ambako watu wake hawajali muda? NB:No hurry in TANZANIA.
 
hahahaaaaa, hii kali, padre kamwanika msela wa mjengoni bila kukusudia lol
 
hahahaha!
MBUNGE ataona watu wanamwangalia sana na atadhani wamevutiwa na hotuba yake wanamckiliza kwa makini..kumbe loh!
 
Back
Top Bottom