big banana
Member
- Jan 23, 2021
- 44
- 83
Nitajaribu kuwaza kuhusu hoja za kupinga akina Mdee na wenzake kuwa wabunge. Watu wanachambua na kujenga hoja kuwa wamevunja katiba ya chama na ya nchi.
Kwa kifupi mimi niweke wazi kuwa niko tofauti na watu wengi wanaopinga akina Mdee kuwa wabunge. Naona kama tunapoteza muda kujadili hoja zisizo na tija kwa nchi yetu na kuongea hoja zinazowafaidisha watu wachache sana kwa faida ya matumbo yao.
Kwan akina Mdee na wenzake 19 wakiendelea kuwa wabunge kuna shida gan. Chadema wao si wamewafukuza. Wale ni wanawake na wanasifa zote za kuwa wabunge, wa viti maalum. Kosa lao ni kuwa chama kinadai hakikuwapendekeza au kuwa waliopendekezwa ni wengine na wala sio Mdee na wenzake?
Kama sio akina Mdee basi ni akina nani hao. Mbona hatujui majina Yao.
Kama hakuna waliopendekezwa na chama, kuna tatizo gan akina Mdee wenye sifa na haki zote kuwa wabunge. Kosa lao la pengine barua kutosainiwa na katibu, nasema pengine.
Niseme hivi Kwan ni lazima Katibu asain barua au mtu yeyote kwa niaba ya Katibu wa chama anaweza kusain.
Mdee yeye alikuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake. Wawakilishi wa wanawake huwa wanachaguliwa na wanawake wenyewe, wala sio baraza kuu. Je Mdee kuandika barua na kuisain kwa niaba ya Katibu mkuu wa chama kuna tatizo gani la kuweza kufukuzwa uanachama?
Kama kuna mtu alikosea taratibu pale ufipa si ni mambo ya kuambizana na kupeana elimu ndan ya chama. Hizi ni siasa, na kwenye siasa kuna rafu nyingi. Hivi ni kweli kuwa tatizo ni akina Mdee kuwa wabunge au tatizo ni wanawake fulan walio karibu na watu fulan kukosa hizo nafasi. Je ni kweli kuwa kama akina Joyce Mukya na wenzake wangekuwa kwenye kundi la akina Mdee na wenzake, hatua kama hizi zingechukuliwa na akina Mbowe?
Heb tuwe serious na issue serious. Haya mambo ya akina Mdee yanatutoa kwenye reli. Wale ni wanawake waliokuwa viongozi wa wanawake katika ngazi mbalimbali ndani ya chadema na walikuwa na sifa zote za kuwa wabunge wa viti maalum na hawakupokonya haki yoyote ya mwanamke mwingine kuwa mbunge. Waliendesha mchakato wa kuteua wabunge wa viti maalum wakapeleka tume ya uchaguzi. Kama chama kilikuwa hakitaki wapeleke, hilo ni Jambo la ndan ya chama, lakin katiba ya nchi ilikuwa inataka idadi fulan ya wanawake kutoka chadema kuwa wabunge baada ya matokeo Yale ya uchaguzi.
Sasa jaji ataamua kipi cha kuheshimu , katiba ya nchi au maamuzi ya chama yanayoenda kinyume na katiba.
Wale wataendelea kuwa wabunge mpaka uchaguzi ujao. Kujadili suala lao ni kukosa kazi za kufanya. Wana haki na sifa zote za kuendelea kuwa wabunge na hakuna mtu wa kuwatoa bungeni.
Atokee mtu mmoja basi mwenye uchungu na uvunjaji wa katiba akafungue Kesi mahakama kuu au mahakama ya katiba kuhoji kama ni halali kwa mzanzibari kuongoza au kuteua mtu wa kuongoza wizara zisizo za muungano.
Apeleke hoja mahakaman kuhoji kama ni halali kuagiza wizara zisizo za muungano kutekeleza projects mbalimbali sehem nyingine ya muungano. Wakaiombe mahakama iamuru na itamke kuwa mzanzibari hawezi kuongoza wizara au kuteua mtu kuongoza wizara zisizo za muungano.
Tuache kuhoji vitu visivyo na tija na vilivyo wazi, tuanze kuhoji vitu vikubwa vyenye kufikirisha na vyenye kuonyesha matatizo makubwa ya katiba yetu.
Alamsiki