Tuwe na mjadala wa wazi leo

Tuwe na mjadala wa wazi leo

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,664
Reaction score
8,285
Kipindi cha awamu ya 5 cha mhe hayati Rais Magufuli tuliona ukosoaji mkubwa kutoka kwa viongozi wa upinzani dhidi ya utawala wa awamu ya 5 licha ya magumu yaliowakuta wapinzani.

Ni kinyume na sasa katika utawala wa awamu ya 6 ya Samia suluhu.

Wakuu huu ukimya uliopo wa ukosoaji kwa viongozi wa upinzani dhidi ya utawala wa awamu ya 6 je, ukimya wao viongozi wakuu wa wa vyama vya upinzani utakua unaashiria nini?

Na kuna nini kimechojificha nyuma ya pazia?

KARIBUNI TUJADILI PAMOJA
 
Unaishi sayari gani? Acha unafiki. Wampigie kondoo gitaa ili iweje?
 
Kuna wachungaji sasa wamechukua nafasi ya vyama vya siasa... Chadema wako bize mahakamani
 
Angalau utawala huu na sisi wapinzani tunapata deals na michongo flani flani. Kuna tuvitengo twa kupiga pesa tunapewa.

Magufuli alikuwa katili sana kwetu. Alitubana kila angle. Lakini sasa tutakosoa nini kama mambo yetu yapo mswano? Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Mjadala Mzuri sana mkuu.
Sema kwasababu ya watu kutokuwa serious wanauchukulia mzaha hii hoja.

Nikijikita kwenye Mada Moja kwa Moja kwanini magufuli Alikuwa anakosolowe wazi wazi.

1. Magufuli Alikuwa anaamka Kila siku na jambo jipya..

2. Alitaka awe anaandikwa yeye anasomwa yeye anatangazwa yeye tu kwa mazuri.

Alipigwa vita kwa sababu.

À. Nchi ilikuwa imekumbwa na wimbi la
1. UTEKAJI.
2.UUAJI.
3. MADAWA YA KULEVYA.
4. UTUMBUAJI HOLELA.
5. KUFUKUZA WANAFUNZI VYUO.
6. KUPIGA WANASIASA RISASI HADHARANI.
7.WANASIASA KUFYATA MKIA NA KUUNGA JUHUDI.
8.MAPAMBANO YA HOVYO YA COVID
9. MAKINIKIA YA MCHONGO.
10. KUKAMATWA MALA KWA MALA KWA NDEGE NK.

N.B.
Nimeweka mambo kumi kwa haraka ila ni mengi zaidi ya hapo.
 
Uhuru wa kidemokrasia kidogo awamu hii upo kuliko kipindi cha awamu ya 5 ,awamu ya giza, unafiki, uongo, kumsifia binadamu mwenzako mpaka kumwita Mungu, kuna mabadiliko mengi mno including humu, awamu ya 5 tuliwapoteza members wengi including Saanane,jeshi la police linasukwa upya na ninaimani within 90days tutaona maboresho mengi tu, President Samia amebonyeza ile RESET BUTTON 🔳
 
Magufuli alibana sana hadi wanasiasa wakakosa pesa za kula. Walilia njaa, pesa zote zilienda kwenye maendeleo.
 
Kipindi cha awamu ya 5 cha mhe hayati Rais Magufuli tuliona ukosoaji mkubwa kutoka kwa viongozi wa upinzani dhidi ya utawala wa awamu ya 5 licha ya magumu yaliowakuta wapinzani..
Hao huwa wanatetea mabeberu na si wananchi wa kawaida. Kwa sasa wanaoteseka zaidi ni wananchi wa hali za nchi.

Ambao kiuhalisia hakuna wa kuwasemea maana wasemaji hawana wanachoweza kupata toka kwao zaidi ya kuwatumia wakati wa uchaguzi.

Na huo ndio UKWELI! Kama kuna mtu haamini basi asubiri aje kiongozi anayetetea tabaka la nchi kama ilivyokuwa kwa hayati JPM, halafu utaona hao upinzani watakavyojitokeza!
 
Mjadala Mzuri sana mkuu.
Sema kwasababu ya watu kutokuwa serious wanauchukulia mzaha hii hoja.

Nikijikita kwenye Mada Moja kwa Moja kwanini magufuli Alikuwa anakosolowe wazi wazi.

1. Magufuli Alikuwa anaamka Kila siku na jambo jipya..

2. Alitaka awe anaandikwa yeye anasomwa yeye anatangazwa yeye tu kwa mazuri.

Alipigwa vita kwa sababu.

À. Nchi ilikuwa imekumbwa na wimbi la
1. UTEKAJI.
2.UUAJI.
3. MADAWA YA KULEVYA.
4. UTUMBUAJI HOLELA.
5. KUFUKUZA WANAFUNZI VYUO.
6. KUPIGA WANASIASA RISASI HADHARANI.
7.WANASIASA KUFYATA MKIA NA KUUNGA JUHUDI.
8.MAPAMBANO YA HOVYO YA COVID
9. MAKINIKIA YA MCHONGO.
10. KUKAMATWA MALA KWA MALA KWA NDEGE NK.

N.B.
Nimeweka mambo kumi kwa haraka ila ni mengi zaidi ya hapo.
sio kweli hamna hata moja hapo acha ngonjera. kifupi maslahi na madeal yao yalibanwa, sasa wanalamba asali na pia kupewa pesa ili wakae kimya. huwezi ongea kama mtu unalamba asali
 
Ukiumizwa una haja ya kuambiwa ulie kwa sauti au uanzishe kilio weye mwenyewe?Ni muda sasa umefika,Watanzania mjitetee wenyewe.Msiwasukumie mizigo yenu wakinzani hasa CHADEMA.Pambaneni wenyewe.Kwanza hamna shukrani.
 
Back
Top Bottom