Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu.

Nawatakieni nyote heri ya mwaka mpya.Mungu akaufanye mwaka huu kuwa mwaka wenu wa kuvuna yote mnayomuomba.

Nikiwa kama mzazi mtarajiwa,nimeona sio mbaya sisi wazazi tukikumbushana au kufunguana macho ktk mambo mbalimbali yatakayozidisha usalama wa watoto wetu.

Ni kawaida sana sisi watanzania kuishi na ndugu zetu wengi ktk nyumba zetu,utakuta mfano mtu una watoto wako lkn pia una ndugu zako na ndugu wa mkeo mnaishi nao pamoja kwa lengo la kuwasaidia ili siku moja nao wawe na maisha yao.Hii inasababisha watoto wetu wa kiume washee vyumba na ndugu zetu wa kiume yaani baba zao wadogo au wajomba zao na watoto wetu wa kike washee vyumba na mama zao wadogo/wakubwa au shangazi zao na housegirl.

Ni jambo zuri kuishi na ndugu zetu lakini naombeni mniamini kuwa sio vizuri watoto wetu walale na ndugu zetu watu wazima hasa wa kiume,nina uhakika na ninachokiongea,nina shuhuda nyingi juu ya watoto wengi wa kiume walivyokua sexualy abused na ndugu wa kiume wa wazazi wao wanaolala nao pamoja.Na inakuwa vigumu kwa mtoto kusema maana hawa molesters wanajua jinsi ya kumtisha mtoto ili asiseme.

Hata watoto wa kike ni vizuri waachwe walale wenyewe maana pia nimeshashuhudia watoto wadogo wa kike wakifanyishwa vitu vya ajabu na ndugu wa kike wa wazazi wao.Kuna mtoto mmoja hivi tunavyoongea anatibiwa fungus mdomoni sababu alikua "analambishwa chumvi" na mama yake mdogo kila siku usiku wakilala.

Najua labda mtaniona mwehu sababu tunawapenda ndugu zetu hivyo hatuwezi kamwe kudhania kuwa wanaweza kufanya hivi,lakini laiti ungeshuhudia niliyoshuhudia ungechukua tahadhari.Dunia imeharibika sana.wanadamu hatuna tena woga,sijasema muwafukuze ndugu zenu,ila ningeshauri hasa kwa watoto wa kiume kuliko wakalala na ndugu wakubwa wa kiume ni bora ndugu hao walale sebuleni kwenye magodoro.

Vile vile kina mama wenzangu naomba niwaonye,kama una tabia ya kuwaambia ndugu zako wa kiume wamsafishe mtoto akiwa amejisaidia uache sio vizuri.Hii tabia ya kumwambia mjomba au baba mdogo wa mtoto akusafishie mtoto ni ya hatari sababu,mwanao anaweza chomekwa vidole sehemu sehemu na wewe ukiona wala usishitukie.Na kama uncle anamfanyia mtoto mambo haya wakati anamsafisha basi akipata upenyo wkt mwingine pia atafanya.

Vile vile najua JF ni kama msafara wa mamba ambao ndani yako kuna mijusi na kenge,najua kabisa wengi wa JF memberz ni watu wazuri sana na wenye hekima lakini nataka niongee na wale wachache wetu wenye tabia za kifataki.Nyie ambao ni watu wazima lakini kutwa kurubuni watoto wadogo,definition ya fataki ni mtu mzima anayewarubuni kimapenzi watoto wadogo.

Nina amini mtu yeyote mwenye tabia za kifataki anaweza kujirekebisha,hivyo naombeni muache tabia za kutuharibia watoto/wadogo zetu.Kama wewe ni mbaba unayefanya hivi hebu jiulize je mtu mzima wa umri wako akikaharibu kale katoto kako unakokapenda utafurahi?Jibu ni hutafurahi,vile vile na wazazi wa hao watoto mnaowarubuni hawafurahi.

Na nyie wanaume mnaotongoza watoto wetu wa kiume nawaombeni hofu ya Mungu iwaingie muache maana siku za hivi karibuni hiki kimchezo kimepamba moto.

Pia kuna kina mama wanaharibu watoto,na maanisha kuna mafataki wa kike pia,wengi tu,kuna mama mmoja amesababisha mtoto wa mwenzake aache shule,huyu mama alikua anamfata mtoto shule ya bording anakosoma anamtorosha wanakwenda kupanga hotel mwishowe mtoto akashindwa masomo na ameambukizwa ukimwi japo huyo mama anadai yeye mzima lkn muda si mrefu na yeye atachekiwa.

Pia kuna kina mama wasagaji wanaharibu watoto wa kike,labda hili ni geni kwetu lakini wapo na hivi vitendo vipo na shuhuda ninazo.Hivyo naomba mwaka huu ili Mungu awaondolee mikosi na mabalaa na aweze kuwapatia yale mnayohitaji hebu nyie mnaofanya hivi vitendo vichafu amueni kubadilika maana inawezekana.

Amini usiamini kama unafanya hivi vitendo lazima tu Mungu anakuadhibu lakini wewe hujui,unaweza kuwa tajiri una kila kitu lakini ukapewa ugonjwa utakaofanya hata usifurahie hizo mali zako.

Okay wazazi wenzangu najua labda sio wote mtakaonielewa hasa ktk kipengele cha ndugu lakini hata kama kuna mmoja atanielewa post hii itakuwa imefanikiwa.

Wimbo huu wazazi nasindikizia huu ujumbe wangu,ni wimbo mzuri sana,kama una watoto wanaosoma ni vizuri uwawekee wausikilize,una ujumbe ambao Tanzania inahitaji kwa sasa.

WITH LOVE ,CHEUSIE.

Nakushukuru kwa post yako kwani imenifungua macho na kuamini hivi vitu vipo na vina madhara makubwa kwa watoto wetu Mungu akubariki kwani najua hii post itaokoa watoto wengi na wazazi kuchukua tahadhari
 
Last edited by a moderator:
Umeongea maneno ya busara sana. Ujumbe umefika cheusie. Ila kwa ujenzi wetu wa kimaskini unakuta nyumba inavyumba 3 vya kulala. Cha wazazi, watoto wa kike na watoto wa kiume. Kwahiyo kama umepata wageni wakike na wa kiume, wote kwa pamoja utawalaza sebuleni au?

Hilo nalo ni suala la kujipanga kabla ya kufanya maamuzi ya kuwa na familia
 
cheusie are you.......pregnant..............................??

kama ndivyo basi imekula kwangu......................!mizawadi yote ile niliyokupa xmas hlf jamaa wameshajaza upepe.....................????
cheusie what do u mean by `Nikiwa kama mzazi mtarajiwa`.....................................???? u must be kiding..............................!............................lol...............................!

back to the topic................................asante kwa kuongelea hili jambo.....................ukifikiria kwa makini...................hatari nyingi zipo majumbani mwetu..........................hawa hawa tunaowapa ugali wa bure....................ndio hawa hawa wanageuka sumu kwetu..............................take care murembo.....................!kuna mdingi fulani.........................yeye ndiye aliyewafataki watoto wake wa kiume...............ishu ilibumburuka baada ya watoto kuanza kuoneana wivu kumshare baba..............................yaani kila mmoja alikua anataka baba awaache wengi abaki naye peke yake..........................sasa hapa napo mtu unalindaje wakuu..............................................???
 
Cheusi hizo pande unazoishi ni zipi, maana kuwa shuhuda wa huu uchafu wote ulioelezea hapa ni ngumu kidogo katika mazingira ya kawaida. Naomba nieleweke kuwa sio kwamba nasema haya mambo hayatokei ila napata shida kidogo kuelewa mazingira yanayokuwezesha wewe kushuhudia mambo yote haya.

Haya mambo hutokea sana na ni rahisi kuyajua kutoka kwa ndugu, majirani au kama unafanya kazi polisi, ni daktari au unafanya mashirika ya kutetea haki za binadamu au watoto.
Binafsi nilifanya utafiti unaohusu mambo ya Child Abuse. Nilienda mpaka vituo vya Polisi kupitia reported cases, pia nilienda hospitali kuwaona ambao wamebakwa/wamelawitiwa na wanapata matibabu. Pia nilipitia tafiti mbalimbali zilizoandika juu ya Child Sex Abuse.

Utafiti mmoja ambao ni thesis ulihoji watoto waliokuwa sexually abused na kufuatilia ni kina nani walikua first abusers. Utafiti huo wa kama miaka nane iliyopita ulionyesha kuwa asilimia 70 ya watoto wamebakwa au kulawitiwa na baba mdogo, uncle, babu,houseboy au watoto kwa watoto wenyewe. Baadhi ya respondents walikua gays tayari.

Niliapa sitaki ndugu kwangu. Kila la kheri wanaopenda kukusanya utitiri wa ndugu wasio na sababu majumbani kwao. Same is for housegirls.

Wazazi ni kutafuta hela na kujirusha. Watoto wanaonana jmosi asubuhi halafu wanaishia. Anyway, kila mtu na maisha yake lakini tusilalamike watoto wameharibika na mabwabwa wamezidi, au watoto hawashikiki.
 
mjasiria,mm naishi maeneo ya kaiwada tena yenye utulivu,sema tu sijui niseme ni bahat nzur au mbaya lkn Mungu amenipa nafasi yakuweza kushuhudia haya mbaya.Nataman kukushawishi usipuuzie ujumbe wangu sbb ni rahisi kudhani how come lkn haya mambo yapo,tena kwa kiwango kikubwa,yanaweza kutokea ktk familia yeyote ile iwe iko mbezi beach au uwanja wa fisi tandika.Hata wazazi waliopatwa na haya ninayoeleza walipata shida kualewa na kuamini kuwa haya yalitokea ndani ya nyumba zao bila wao kuhisi kama kuna kinachoendelea.
 
Nakushukuru kwa post yako kwani imenifungua macho na kuamini hivi vitu vipo na vina madhara makubwa kwa watoto wetu Mungu akubariki kwani najua hii post itaokoa watoto wengi na wazazi kuchukua tahadhari

asante kwa kushukuru,nafuraahi post yangu imekufungua macho,sbb haya mambo yapo hivyo kuchukua tahadhari ni lazima,Nawe pia ubarikiwe.
 
asante kwa ujumbe.
Unachosema ni kweli kbs!
Ndugu tunaowaamini ndio wanaotuharibi.
Maadili hakuna kabisa

kuna ule msemo kuwa adui wa kwanza ni yule wa nyumbani kwako,kwa sbb tunawapenda ndugu zetu,hata kama kuna dalili za uharibifu unaoendelea nyumban huwa hatuzion sbb upendo wetu kwao unatufanya tupuuzie hata pale dalili zinapokua za wazi wazi kabisa sbb mtoto anayefanyiwa hivi vitu hawezi kubehave normaly,anabadilika,mzazi akiwa makini ndio anaweza kuona kuwa mtoto hayuko sawa.
 
cheusie are you.......pregnant..............................??

kama ndivyo basi imekula kwangu......................!mizawadi yote ile niliyokupa xmas hlf jamaa wameshajaza upepe.....................????
cheusie what do u mean by `Nikiwa kama mzazi mtarajiwa`.....................................???? u must be kiding..............................!............................lol...............................!

back to the topic................................asante kwa kuongelea hili jambo.....................ukifikiria kwa makini...................hatari nyingi zipo majumbani mwetu..........................hawa hawa tunaowapa ugali wa bure....................ndio hawa hawa wanageuka sumu kwetu..............................take care murembo.....................!kuna mdingi fulani.........................yeye ndiye aliyewafataki watoto wake wa kiume...............ishu ilibumburuka baada ya watoto kuanza kuoneana wivu kumshare baba..............................yaani kila mmoja alikua anataka baba awaache wengi abaki naye peke yake..........................sasa hapa napo mtu unalindaje wakuu..............................................???

leo niko kimama zaidi sitaki masihara.Hiyo ya wababa dizaini hiyo nayo ipo sana,hata wababa kwa mabinti zao pia ipo,ila huyu shetan akishamwingia baba mama hutaweza kulinda,maana baba ni mlinzi mwenzake na mama lkn akigeuka kuwa zimwi mama huna jinsi labda kama watoto wawe na uwezo wa kukataa na kumweleza mama.Ila kuna mahala nimesema hata tuwalinde vipi watoto wetu kama familia haina ulinzi wa Mungu yote ni kazi bure.Mungu ndiye anayeweza kuipesha vitu kama hivi vya baba kwa mwanae.God forbid.
 
Haya mambo hutokea sana na ni rahisi kuyajua kutoka kwa ndugu, majirani au kama unafanya kazi polisi, ni daktari au unafanya mashirika ya kutetea haki za binadamu au watoto.
Binafsi nilifanya utafiti unaohusu mambo ya Child Abuse. Nilienda mpaka vituo vya Polisi kupitia reported cases, pia nilienda hospitali kuwaona ambao wamebakwa/wamelawitiwa na wanapata matibabu. Pia nilipitia tafiti mbalimbali zilizoandika juu ya Child Sex Abuse.

Utafiti mmoja ambao ni thesis ulihoji watoto waliokuwa sexually abused na kufuatilia ni kina nani walikua first abusers. Utafiti huo wa kama miaka nane iliyopita ulionyesha kuwa asilimia 70 ya watoto wamebakwa au kulawitiwa na baba mdogo, uncle, babu,houseboy au watoto kwa watoto wenyewe. Baadhi ya respondents walikua gays tayari.

Niliapa sitaki ndugu kwangu. Kila la kheri wanaopenda kukusanya utitiri wa ndugu wasio na sababu majumbani kwao. Same is for housegirls.

Wazazi ni kutafuta hela na kujirusha. Watoto wanaonana jmosi asubuhi halafu wanaishia. Anyway, kila mtu na maisha yake lakini tusilalamike watoto wameharibika na mabwabwa wamezidi, au watoto hawashikiki.

nashukuru kwa ulichoandika maana watu wengi tukiongea kama hivi itasaidia wale wanaodhani nyumaban kuko salama wapadili jinsi ya kufikiri.Nashukuru unanielewa ninachoongea sababu ni rahisi mtu ambaye hajashuhudia haya kudhani labda mim ni mwehu.Haya mambo ni ya kawaida sana ila si rahisi mtu kuamin kuwa inawezekana hadi limfike.Pia mara nyingi,hizi kesi hata maredion na magazetini sio mara kwa mara kuzisikia sbb unakuta aliyefanya kitendo ni ndoo basi,na wazazi kuficha aibu wanayamaliza kindugu,yanaisha kimya kimya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom