Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, Jan 3, 2012.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nawatakieni nyote heri ya mwaka mpya.Mungu akaufanye mwaka huu kuwa mwaka wenu wa kuvuna yote mnayomuomba.

  Nikiwa kama mzazi mtarajiwa,nimeona sio mbaya sisi wazazi tukikumbushana au kufunguana macho ktk mambo mbalimbali yatakayozidisha usalama wa watoto wetu.

  Ni kawaida sana sisi watanzania kuishi na ndugu zetu wengi ktk nyumba zetu,utakuta mfano mtu una watoto wako lkn pia una ndugu zako na ndugu wa mkeo mnaishi nao pamoja kwa lengo la kuwasaidia ili siku moja nao wawe na maisha yao.Hii inasababisha watoto wetu wa kiume washee vyumba na ndugu zetu wa kiume yaani baba zao wadogo au wajomba zao na watoto wetu wa kike washee vyumba na mama zao wadogo/wakubwa au shangazi zao na housegirl.

  Ni jambo zuri kuishi na ndugu zetu lakini naombeni mniamini kuwa sio vizuri watoto wetu walale na ndugu zetu watu wazima hasa wa kiume,nina uhakika na ninachokiongea,nina shuhuda nyingi juu ya watoto wengi wa kiume walivyokua sexualy abused na ndugu wa kiume wa wazazi wao wanaolala nao pamoja.Na inakuwa vigumu kwa mtoto kusema maana hawa molesters wanajua jinsi ya kumtisha mtoto ili asiseme.

  Hata watoto wa kike ni vizuri waachwe walale wenyewe maana pia nimeshashuhudia watoto wadogo wa kike wakifanyishwa vitu vya ajabu na ndugu wa kike wa wazazi wao.Kuna mtoto mmoja hivi tunavyoongea anatibiwa fungus mdomoni sababu alikua "analambishwa chumvi" na mama yake mdogo kila siku usiku wakilala.

  Najua labda mtaniona mwehu sababu tunawapenda ndugu zetu hivyo hatuwezi kamwe kudhania kuwa wanaweza kufanya hivi,lakini laiti ungeshuhudia niliyoshuhudia ungechukua tahadhari.Dunia imeharibika sana.wanadamu hatuna tena woga,sijasema muwafukuze ndugu zenu,ila ningeshauri hasa kwa watoto wa kiume kuliko wakalala na ndugu wakubwa wa kiume ni bora ndugu hao walale sebuleni kwenye magodoro.

  Vile vile kina mama wenzangu naomba niwaonye,kama una tabia ya kuwaambia ndugu zako wa kiume wamsafishe mtoto akiwa amejisaidia uache sio vizuri.Hii tabia ya kumwambia mjomba au baba mdogo wa mtoto akusafishie mtoto ni ya hatari sababu,mwanao anaweza chomekwa vidole sehemu sehemu na wewe ukiona wala usishitukie.Na kama uncle anamfanyia mtoto mambo haya wakati anamsafisha basi akipata upenyo wkt mwingine pia atafanya.

  Vile vile najua JF ni kama msafara wa mamba ambao ndani yako kuna mijusi na kenge,najua kabisa wengi wa JF memberz ni watu wazuri sana na wenye hekima lakini nataka niongee na wale wachache wetu wenye tabia za kifataki.Nyie ambao ni watu wazima lakini kutwa kurubuni watoto wadogo,definition ya fataki ni mtu mzima anayewarubuni kimapenzi watoto wadogo.

  Nina amini mtu yeyote mwenye tabia za kifataki anaweza kujirekebisha,hivyo naombeni muache tabia za kutuharibia watoto/wadogo zetu.Kama wewe ni mbaba unayefanya hivi hebu jiulize je mtu mzima wa umri wako akikaharibu kale katoto kako unakokapenda utafurahi?Jibu ni hutafurahi,vile vile na wazazi wa hao watoto mnaowarubuni hawafurahi.

  Na nyie wanaume mnaotongoza watoto wetu wa kiume nawaombeni hofu ya Mungu iwaingie muache maana siku za hivi karibuni hiki kimchezo kimepamba moto.

  Pia kuna kina mama wanaharibu watoto,na maanisha kuna mafataki wa kike pia,wengi tu,kuna mama mmoja amesababisha mtoto wa mwenzake aache shule,huyu mama alikua anamfata mtoto shule ya boarding anakosoma anamtorosha wanakwenda kupanga hotel mwishowe mtoto akashindwa masomo na ameambukizwa ukimwi japo huyo mama anadai yeye mzima lkn muda si mrefu na yeye atachekiwa.

  Pia kuna kina mama wasagaji wanaharibu watoto wa kike,labda hili ni geni kwetu lakini wapo na hivi vitendo vipo na shuhuda ninazo.Hivyo naomba mwaka huu ili Mungu awaondolee mikosi na mabalaa na aweze kuwapatia yale mnayohitaji hebu nyie mnaofanya hivi vitendo vichafu amueni kubadilika maana inawezekana.

  Amini usiamini kama unafanya hivi vitendo lazima tu Mungu anakuadhibu lakini wewe hujui,unaweza kuwa tajiri una kila kitu lakini ukapewa ugonjwa utakaofanya hata usifurahie hizo mali zako.

  Okay wazazi wenzangu najua labda sio wote mtakaonielewa hasa ktk kipengele cha ndugu lakini hata kama kuna mmoja atanielewa post hii itakuwa imefanikiwa.

  Wimbo huu wazazi nasindikizia huu ujumbe wangu,ni wimbo mzuri sana,kama una watoto wanaosoma ni vizuri uwawekee wausikilize,una ujumbe ambao Tanzania inahitaji kwa sasa.

  WITH LOVE ,CHEUSIE.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante kwa uzi mzuri CM.

  Nnachoweza kuongezea ni wazazi wajenge tabia na mazoea ya kuongea na watoto wao kujua hua wanafanya nini na nani wao wakiwa hawapo, wakiwa wanacheza nje, wakiwa shule n.k . Kwasababu pedofiles sio lazima wawe karibu kiasi cha kushea chumba. Hata walimu, majirani, wavulana wengine mitaani wanaweza wakafanya hayo.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nilipo:flypig:kutana na YESU historia ya maisha yangu yote ilibadilika.
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Yani malezi siku hizi ni very tricky aisee.. mungu atusaidie tu
  Asante kwa mada hii
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Umeongea maneno ya busara sana. Ujumbe umefika cheusie. Ila kwa ujenzi wetu wa kimaskini unakuta nyumba inavyumba 3 vya kulala. Cha wazazi, watoto wa kike na watoto wa kiume. Kwahiyo kama umepata wageni wakike na wa kiume, wote kwa pamoja utawalaza sebuleni au?
   
 6. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante Lizzy kwa kuappreciate.Ni kweli kuongea na watoto ni jambo zuri sana,kwanza linajenga urafiki kati ya mtoto na mzazi kiasi kwamba anakua huru kukueleza lolote.Na hao wengine ndo hao sasa mafataki niliowakemea na kuwaomba wabadili tabia zao.Ubarikiwe.
   
 7. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  yes yes, before and after jesus is not the same.
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, wazazi tuwe makini! Asante kwa meseji nzuri.
   
 9. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni kweli,wazazi wanatakiwa wawe makini sana,mtu unatakiwa kuchunguza kuona kama mtoto ana mabadiliko kidogo,ujue kwa nini amebadilika,inabidi tuwe na muda wa kuwa karibu na waoto wetu pia,sio mtu uko busy kuwatafutia ada hata hujui jana wameamka saa ngapi na leo wamelala saa ngapi,kumbe mtoto yuko kwenye dilema anajiuliza sijui nimkubali yule baba anayeniahidi blackberry,kumbe tungekua na muda wa kukaa nao ungegundua mtoto kuna kitu kinamsubua kichwani ungempeleleza angesema.
   
 10. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante kwa kuappreaciate.
  kwa kweli mm watoto wangu kutokana na mambo ninayoyajua sitawachanganya na ndugu zangu watu wazima,nitaangalia jinsi nyumba yangu ilivyo then hao wageni nitajua jinsi ya kuwalaza,kama ni wageni wa kuondoka kesho au keshokutwa,basi watoto wangu naweza kuwawekea godoro chini wao ndio walale sebuleni wawapishe wageni chumbani,ila kama ni wale ndugu tunaoishi nao hawaondoki kesho wala kesho kutwa wao ndio watalala sebuleni au huko dining au jikon,kuna majiko mengine ni makubwa tu kama vyumba,mtu anaweza kulala huko.
   
 11. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Cheusi, kwanini uwalaze watoto sebuleni ka wageni walale chumbani? Sio haki kwa watoto. Pia ujue mbakaji akiwepo ndani hata sebuleni atamfuata tu mtoto wako au mchana kweupeee anambaka baada ya kushiba dona ulilompikia anacheua mdomoni na chini.

  Swali kuu ni kwamba - kwanini tukaribishe wageni na wewe huna servant quarter au guest room? Hili nalo linataka uzi wake.
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  au unawapa hela wageni wakishakula wakalale zao guest house. Lol.
   
 13. n

  ngwana ongwa doi Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cheusi mangala umetoa wosia mzuri sana na unaonekana unahekima sana,but nakushauri badilisha avatar yako busara ulizotoa haziendani na avatar hiyo.
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni kweli mbakaji anaweza kuwafuata watoto sebuleni lkn haitakua rahisi kama akiwa amelala naye kitanda kimoja.
  sion kama ni shida watoto kulala sebuleni kwa siku mbili hadi wageni waondoke,hata mm nilivyokua mtoto wakija wageni tulikua tunatandikiwa chini sometimes halafu wageni wanalala kitandani.
  kuwa na wageni ni neema,ni jambo zuri,sio lazima tuwe na servant quarter au vyumba maalum vya wageni ndio tuweze kupokea wageni majumbani kwetu,hiyo itakua ni ajabu na watz wengi nyumba zao hazina hivi vitu,nyumba nyingi ni vyumba vitatu vya kulala sebule jiko choo imekamilka.wageni wanakaribishwa hata kama nyumba ni ndogo cha msingi ni kujua tu utafanyaje ili uwatenge watoto wako hadi wageni wakiondoka.
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hongera "mzazi mtarajiwa"!

  Nilimiss harusi yako!
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hii hapana,nikija kwako ukanifanyia hivi nitakutangaza ukoo mzima na sitarudi tena kwako,huwezi kufanya hivyo,ukiwa kama mama utajua tu ufanyaje bila kuwafanya wageni wajisikie vibaya.
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  cheusie hata kitendo cha kumlaza mtu mzima jikoni au sebuleni wakati chumbani kamelala katoto kadogo unafikiri huyo mtu hatojisikia vibaya? Ni bora kama hutaki alale na watoto basi utafute mazingira mazuri ya mgeni wako kulala na si jikoni au sebuleni. Halafu hicho kinachoogopwa hakiwezi kufanyika mchana wakati haupo? Watoto wako hawatotembelea ndugu na kulala huko huko?
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mi napendekeza mtu ujikakamue umpe hela mgeni akalale gesti iwapo hutaki alale na watoto na wewe hauna vyumba vya kutosha. Utakapompa hela mara ya kwanza utakuwa ushafikisha ujumbe kuwa hutaki wageni walale nyumbani kwako hivyo kwa mtu mwenye akili hatorudia tena. Kuna mzee mmoja yeye akiombwa lifti huwa anawauliza wanaomuomba nauli ya kutoka pale hadi wanapoenda ni sh ngapi, akishatajiwa anawapa hela. Watu wameshamsoma huyo mzee, sahv yupo huru na gari lake maana hakuna anayemuomba lift.
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante kwa kupenda wosia,naomba uniahidi kutenda kile ninachoshauri,maana kitasaidia kuwaepusha watoto wetu ktk kufanyiwa vitendo wasivyostahili na vinavyoweza kuharibu mfumo mzima wa maisha yao.Kumbuka ni muhimu kuwalinda maana hawana mlinzi mwingine zaidi ya sisi tuliowaleta duniani,baya unaloweza kulikinga likiwapata wakulaumiwa sio aliowadhuru bali ni wewe maana ungechukua tahadhari labda pedofile asingefanikiwa japo wakati mwingine tunaweza kulinda sana na bado mapedofile wakatuharibia watoto ndio maana ni vyema tukawalinda lkn tujue tukiwalinda bila kuwakabidhi kwa Mungu tutakua tunalinda bure.

  Avatar isikudistruct,ipuuzie tu,ubarikiwe.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Au unalala na watoto wako chumbani kama sio mijibaba.
   
Loading...