Philipo Mwakibinga
Senior Member
- May 13, 2013
- 111
- 175
DIPLOMASIA YA KIUCHUMI BAINA YA CHINA NA AFRIKA
Tarehe 14/12/2020.
Mahusiano ya China na Nchi za Kiafrika yanarejewa kwanzia karne ya 7 bk (baada ya Kristu) hadi sasa. Kwasasa China imekua na uhitaji mkubwa wa malighafi na masoko kwaajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko yake. Wakati huo Afrika imekua na mahitaji makubwa ya fedha za kuendeleza na kujenga miundombinu mbalimbali.
China inatoa kipaombele cha utoaji mikopo yenye masharti nafuu, China wanafanya Uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu kwa nchi za Afrika ambazo zinautajiri mkubwa wa malighafi na eneo kubwa lenye soko kwaajili ya bidhaa za viwandani kwa maana ya eneo lenye idadi kubwa ya Watu kupewa kipaombele zaidi. Pamoja na unafuu huo China kama nchi nyingine kubwa Duniani imekua ikinyonya nchi za Afrika kwa kusaini mikataba mibovu hasa pale ambapo VIONGOZI wa TAIFA HILO NI LEGELEGE.
Wakati mwingi China wamejikita kwenye ujenzi wa miundombinu mikubwa katika nchi za Afrika kwa kubadilishana na madini, mafuta kwa mikataba ya ujenzi wa miundombinu.
Mahusiano haya yamekuwa ya kichagizwa na kuimarishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia, biashara, misaada ya kijeshi kama vile silaha na vifaa vingine.
Ndani ya Bara la Afrika China amekua na ushindani mkubwa na mataifa mbalimbali ya Ulaya na Amerika kama vile Uingereza, Ufaransa na Amerika.
Kwa Mwaka 2009 pekee China alikuwa mdau mkubwa wa Biashara baina yake na Nchi za Afrika huku akimuacha Amerika mbali zaidi kwani alisaini mikataba na mataifa takribani arobaini (40) ya Afrika.
Taarifa zinaonesha kuwa Mwaka 2000 Biashara ya China na Afrika ilikuwa kwa thamani ya dolla za kimarekani Bilioni kumi ($10 Bilioni) ambapo kufikia Mwaka 2014 ilikuwa hadi kufikia dolla za Kimarekani miambili ishirini bilioni ($ 220 Bilioni).
Nilazima tuendelee kuwa na Rais Dkt Magufuli ili Tanzania iendelee kunufaika na Diplomasia ya Kiuchumi kuliko kuwa Miongoni mwa mataifa yanayoibiwa. Uwekezaji huu wa miundombinu ya barabara, umeme, Afya, Elimu, Usafiri wa Aga na mengine mengi unaofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano ni wazi kuwa tunaenda kuwa Taifa kubwa litakaolo weza kuvuka mipaka katika Duru za kiuchumi Afrika na Duniani kwa Ujuma. Tujenge uzalendo.
Philipo Mwakibinga.
0758-910403.