Tuwatajewalarushwa.co.tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwatajewalarushwa.co.tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAMMAMIA, Jul 8, 2011.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi tumekumbana na vitendo vya rushwa. Ingawaje kisheria "mla rushwa na mtoa rushwa wote ni wakosa, lakini mara nyingi tunalazimika kununua haki zetu kwa kutoa rushwa. Kuanzia kijijini kwa balozi hadi kufikia wizarani kwa waziri na walio chini yake, kumejaa wala rushwa na kunanuka. Tumefika pahala kutoa rushwa kumiekuwa mtindo wa maisha yetu na wametuweka kwenye ulingoni kwenye ringi hatuna pa kutokea.
  Lakini bado nafasi tunayo, angalau kwa kupunguza hasira zetu kwa kuwataja hapa.

  Umewahi kuombwa "kitu kidogo katika kudai haki yako au katika kufuatilia huduma? Polisi amekukamata na kosa, badala ya kukupeleka mahakamani akadai "chai"? Mdada, umelazimika kumridhisha bosi ili upate kazi au usitimuliwe kazini? Mzee wangu uliyekwisha staafu, hukupewa kiinua mgongo chako hadi ulipotoa chochote? Mwanafunzi, ilikubidi kuahidi na baadaye kutoa sehemu ya mkopo wako wa elimu, vyenginevyo usingelipata mkopo? Mwanakijiji, ulipotaka kujenga ilikulazimu kumgawia chai diwani ili upate kibali cha ujenzi? Mfukuza tonge, hukupewa leseni ya kuweka genge lako hadi ulipovaa "shati la mikono mirefu? Mifano ni visa ni vingi.
  Ninakuombeni kutaja hapa kila adha uliyopata kwa kudai haki yako.

  Nikianza kwa kutoa mfano, niliporejea toka masomoni, Wizara ya Fedha ilikuwa na wajibu wa kunirejeshea gharama za nauli. Nilipigwa tarehe siku nenda siku rudi, mpaka pale"msamaria mwema" mmoja pale wizarani aliponitonya kuwa ili nifanikiwe ingebidi "nile na watu". Kwa umasikini wangu, nilikubali na kutakiwa kutoa 25% ya pesa zile na kweli haikumaliza wiki nikafanikiwa. Siku ya makabidhiano, nilitakiwa kuweka saini kwenye vocha, baadaye "wakahukua chao mapema" kabla ya kuingia mikononi mwangu, yenginevyo tungelivutana mashati. Wewe je, ni mkasa gani wa rushwa uliokumbana nao?
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Zamani za Sokoine na Paul Sozigwa kulikuwa na kipindi RTD kinaitwa Mikingamo ambacho nia yake ilikuwa ni kufichua waovu wa aina hiyo, ila nadhani wengine waliki-abuse.
   
 3. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Badilisha katiba ili sheria ya wala rushwa na watoa rushwa ifanane kabisa na ile ya wa china. Kwa ufupi sheria inasema hivi.............afisa wa serikali akipokea rushwa kwa namna yoyote ile hukumu yake ni kitanzi. Najua hii sheria ni kali sana ila imewanyonga maafisa kadhaa watuhumiwa wa rushwa na matokeo yake mnaona china ya kikomunisti iloshamiri rushwa miaka ya sabini na themanini sasa hivi mambo mswano, maendeleo juu kwa juu mpaka inaitisha marekani na urusi.
   
 4. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwakweli hata demu nilienae nilimpata baada ya kumuhonga sana( yaani kumpa sana rushwa) ndo akanikubali,kilio changu mpaka sasa ni kuwa najua hanipendi na yupo kwangu after faranga!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nakikumbuka mkuu Tuambie ni nani yuko wapi na anafanya nini kuendeleza rushwa, kama unavyosema watu waliki abuse wakawa wanasingizia watu hovyo lakini kilisaidia kwa kiasi chake.
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tena walikusamehe hawajakumbushia kurudisha mkopo wao, nadhani wanagekukumbusha usingeondoka na kitu.
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,046
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Mpige chini!!
   
 8. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  rushwa ziko nyingi anzia nepotim, kickback(ten%), loyality(kupewa madaraka, kazi usiyostahili kwa kulipwa fadhila ya Ngono, ushemeji, kupiga watu mabomu,urafiki na kukiss your boss's ass')', takrima, fedha taslim ili upate huduma na nyingine nyingi RUSHWA IPI WE unataka tuwataje wahusika?
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,850
  Likes Received: 4,518
  Trophy Points: 280
  Hali kwa kweli ni mbaya sana...kiasi kwamba watu wanaona kumpa mfanyakazi wa umma au wa sekta binafsi asante baada ya kutoa huduma nzuri kama ni sawa. Yaani unaenda hospitali, muuguzi anakuhudumia vizuri, na wewe kuonyesha umeridhika na huduma yake, unampa pesa kama asante. Hii ni rushwa tena mbaya sana...kwanini apewe asante wakati ametimiza wajibu wake?!? Hii nayo ni sawa na serikali ya CCM inavyojisifia kujenga barabara n.k. (tena hadi inataka iwe inasifiwa kwa hayo) wakati huo ni wajibu wake kama serikali.

  Kwa hiyo mkuu tatizo lipo kila sehemu siku hizi....kuna na adhabu kali zenye fundisho kwa wengine ni moja ya suluhisho..ila kutoa elimu ya masuala ya rushwa kuanzia shule za msingi pia ni suluhisho jingine...pia kuboresha maslahi ya watumishi wa umma katika kupunguza tofauti ya walio nacho na wasion nacho kutasaidia kwa kiasi kikubwa..
   
 10. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rushwa ni adui wa haki...sitatoa wala kupokea rushwa....hii ilikuwa amri ya ngapi ya TANU/CCM?
   
Loading...