Tuwashauri waandishi wachanga wa riwaya!

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
13,363
31,505
Habari waungwana!
Nianze kwa kuwapongeza sana watunzi wa riwaya kwa kazi zao nzuri ambazo huelimisha,huonya,huhamasisha na kuburudisha jamii.Binafsi ni mpenzi wa riwaya hivyo nafurahi sana ninapoona waandishi wapya wakichipukia kuendeleza fasihi ya kiswahili.Pamoja na kazi zao kuwa nzuri ni vyema kuwapa ushauri ili kuboresha kazi zao.

Nikianza na mwandishi PATRICK C.K, kazi zake ni nzuri na hapo baadae atakuja kuwa mwandishi bora,nashauri mtunzi huyu arekebishe mtazamo wake wa kuona kuwa mwisho wa waovu ni kifo. Kwa nchi inayofuata utawala wa sheria kama Tanzania,anapaswa aonesha jinsi waovu wanavyoshughulikiwa na sheria kuliko kuishia kufa,kuuwawa au kukimbilia nje ya nchi. Mfano katika riwaya za QUEEN MONICA na PENIELA tumeona viongozi wengi waovu,wasaliti na wauza madawa ya kulevya wakiishia kuuwawa au kukimbia nchi. Ina maana anafundisha jamii kuwa waovu wauawe na sio kufikishwa kwenye vyombo vya sheria? Au anafundisha jamii kuwa mtu anaweza kufanya uovu na mwisho wa siku akakimbia nchi na ikawa ndo mwisho wa stori? Hapana jamii inapaswa kufundishwa kutii sheria na aioneshe jamii jinsi sheria inavyoweza kumaliza uovu katika jamii.

Karibuni waungwana muendeleze ushauri kwa waandishi wetu ili tuboreshe na kuendeleza fasihi ya kiswahili!
 
Watunge vitabu vyenye direct effects kwa msomaji,
Wengine ni just mere stories, you gain nathing at the end.
Alafu wapunguze kuwa too theoretical, watunge mambo yenye uhalisia kwenye jamii, yanayoigusa jamii moja kwa moja.

Mf, mtunzi wa watoto wa mama Ntilie, takadini etc , hawa waliigusa jamiii direct.
Sio unatujazia mambo ya kufikirika ya usalama wa Taifa kibao kuanzia mwanzo wa kitabu hadi mwisho, sasa sisi raiya inatusaidia kitu gani.?
 
Unachokisema ni kweli kabisa, wakati mwingine wanatuletea habari za kufikirika zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom