Tuwape wakenya hongera, pole! Tz tujipange na kutumia fursa hiyo.

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu,
Sakata la uchaguzi Mkuu waKenya kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka limekamilika kwa Tumekumtangaza Uhuru Muigai Kenyatta kuwamshindi wa nafasi ya Urais. Uhuru Kenyatta kwa mujibu wa hesabu za Tumeameshinda kwa kujipatia takribaniasilimia 50.07 ya kura zilizopigwa na hivyo kumbwaga mpinzani wake mkuu Raila Amollo Odinga.

Pamoja na kutolewa kwataarifa hiyo ya ushindi wa Uhuru Kenyatta, muda mfupi baadae Raila Odingaalitoa taarifa yake kupinga matokeo hayo. Raila anasema hakubaliani na matokeahayo na hivyo yeye na wenzake wameamua kuyapinga kwa kufuata mkondo wa Mahakamahuku akionyesha kuwa na imani na mfumo wa Mahakama uliopo hivi sasa.

Katika miaka michacheiliyopita, baada ya kupitishwa kwa Katiba Mpya, mfumo wa Mahakama nchini Kenya umejijengeaheshima kwa kukubali na kufanya mabadiliko makubwa yenye lengo la kujenga imanikwa wananchi. Tume ya kuchuja utendaji na uadilifu wa majaji na mahakimuinayoongozwa na Jaji Rao imefanya kazi kubwa ikiwamo kuwaondoa katika nyadhifazao majaji kadhaa na mahakimu kwa maamuzi mabaya, rushwa, uadilifu, upendeleona mengineyo.

Aidha Jaji Mkuu wa Kenya,Dr. W. Mutunga amesimamia mageuzi makubwa yenye kujenga heshima na nidhamu yamahakama. Tukio mojawapo la hivi karibuni ni kuondolewa madarakani kwa NaibuJaji, Nancy Baraza, ambaye alituhumiwa kwa kutumia madaraka yake vibaya kwakumtisha na kujaribu kumdhuru mfanyakazi mmoja wa kike wa duka la huduma jijiniNairobi. Jaji huyu, baada ya uchunguzi,amefukuzwa kazi. Nafasi yake hivi sasa imefanyiwa usaili na Jaji aliyeshindamchujo huo mkali nambaye atajaza nafasi hiyo ni Jaji K. Rawal. Jaji Rawal, ni mamamtu mzima mwenye uzoefu wa takribani miaka 40 katika sheria. Mfumo unahitajikuwapo kwa jinsia mbili tofauti kati ya Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu.

Pamoja na Dr. Mutunga,yupo pia mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Githu Muigai ambaye naye amekuwa namchango mkubwa katika kujitahidi kusimamia na kutekeleza kwa haki na usawamajukumu ya kisheria kwa wananchi wa Kenya. Hawa wachache, ni baadhi yaviongozi katika muhimili huu ambao Raila anasema hivi sasa ana imani nao.

Katika Uchaguzi Mkuu wanyuma uliotawaliwa na vurugu, mapigano na mauaji, hakuna aliyeonyesha kuwa naimani na Mahakama. Watu wakaamua kuingia barabarani na hatimaye kupelekeakutokea kwa vurugu nyingi na mauaji ya kutisha. Wanaoshtakiwa kwa vurugu namauaji hayo ni Rais Mteule UhuruKenyatta, Makamu mteule W. Ruto, aliyekuwa mtangazaji wa maarufu Radio; J. ArapSang na aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa umma Balozi F. Muthaura. Hawa wana kesiya kujibu, ICC.

Nimetoa maelezo hayo marefukidogo ya utangulizi kwa makusudi kabisa ili kujenga uelewa wa pamoja wakinachoendelea Nchini Kenya kwa hivi sasa. Nimelenga pia kutoa tahadhari kutofanyaharaka kushangilia, kucheka, kupongezana na kukimbilia kutoa salamu za pongezikabla ya kutafakari kwa kina athari za maamuzi haya.

Katika maelezo yanayofuatanitazieleza athari hizo pamoja na fursa kwa Tanzania kujijenga kisiasa nakiuchumi.

1.Tishiokwa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kwa hali ilivyo hivi sasani vema kama Taifa tukajiepusha kuonyesha msimamo wa wazi na upendeleo kwamgombea yeyote kati ya hao wawili. Maamuzi yenye muelekeo mmoja yanaweza kuletaathari kubwa za kimahusiano na ushirikiano. Ni vema tusubiri mchakato wakimahakama ukamilike ndio Nchi itoe msimamo wake.

Itatuweka pagumu kama Taifaiwapo tutafanya haraka kutoa kauli na msimamo wa kiserikali na baadaye Mahakamaikaamua vinginenvyo.
Uganda tayari wametoamsimamo wao wa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta, ni vema Tanzania isubiri kwafaida na kudumisha mahusiano mema katika Afrika Mashariki.

2.Kesi za ICC.

Kwa bahati mbaya sanaUhuru Kenyatta na William Rutto wote ni washtakiwa katika mahakama ya kimataifaya uhalifu, ICC. Kuchaguliwa au kutochaguliwa hakusimamishi mchakato wauendeshaji wa kesi huko The Hague. Kesi zitaendelea. Wao kama washtakiwawatatakiwa kuwapo muda wote wakati kesi zao zikisikilizwa.

Hata hivyo, iwapo mahakama ya Kenya itaamua kusimamiamatokeo ya Tume, maana yake ni kuwa Kenyatta na Rutto watakuwa ni viongoziwakuu wa Nchi waliopo madarakani wenye kesi mahakamani. Upo uwezekano mkubwa wawao kugomea kwenda The Hague kutokana na nafasi zao za kimadaraka na ugumu wakuwakamata. Haya ni maoni yangu kwa kuzingatia uzoefu na tabia za viongozikatika Nchi zetu. Iwapo wataamua kufanya hivyo, inawezakusababisha Mahakama kutoa hukumu bila ya wao kuwapo.

Kwa mantiki hii,tutakuwana viongozi wengine wa aina ya kina Al-Bashiri wa Sudan, ambaye anatembea akiwaanawindwa na ICC ili akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Katika kukwepa kuwindwakimataifa na kukamatwa, Rais huyo wa Sudan amejikuta akitengwa na Dunia,anaogopa kusafiri nje ya Sudan na kuliingiza Taifa hilo katika gharama kubwakwa kusafiri na msururu wa walinzi, vifaa na dhana za kijeshi ili kujilinda asikamatwe.Pamoja na kuheshimu maamuzi ya Wakenya, lakini viongozi wa aina hii ni lazimakufanya nao kazi kwa uangalifu sana.Tukumbuke pia mkono mrefuwa ICC na yaliyowapata Rais Taylor wa Liberia, Gbagbo wa Ivory Coast. Hii nimifano michache tu.

3.Msimamo wa Mataifa ya Ulaya Magharibi na Marekani

Mataifa mengi ya Ulaya Magharibina Marekani tayari yametoa msimamo wao wa kutoshirikiana na viongozi ambao niwashtakiwa wa ICC. Walitoa msimamo huu kabla ya uchaguzi na hata hivi sasamsimamo wao bado haujabadilika.Mataifa haya yana nguvukubwa ya kisiasa na kiuchumi Duniani. Kutoshirikiana na viongozi hawa kutaletaathari kubwa na kuyumba kwa uchumi wa Kenya kwa kipindi chote ambacho viongozihawa watakuwa madarakani.Dunia ni kijiji, huwezikukwepa kushirikiana na wakubwa hawa katika uchumi Duniani.

4.Fursa za kiuchumi

Baada ya kupotezatakribani miaka 10 kwa uchumi wa Tanzania kudidimia, tujipange kutumiakinachotokea Kenya kama fursa ya kiuchumi. Siasa za zamani za asante,nashukuru! Zimepitwa na wakati.Kwa mtazamo wa Watanzaniawengi, jambo hili watalishangaa na kuona kwamba ni roho mbaya. Lakini ni lazimakutambua kwamba siasa ni uchumi! Misaada yote na wema wote ambao tumekuwatukifanya kwa miaka mingi havijatusaidia kupata mendeleo yoyote ya maanakiuchumi. Tumekuwa tukiridhika kwa kushikwa mikono na kuambiwa asante. Nilazima kubadilika. Taifa lifaidike.Hata Nchi kubwa na zenyeuwezo sana kiuchumi, hazitoi msaada wowote bure. Lazima wana malengo ya waokufaidika kwanza. Malengo haya yanaweza kuwa wazi au yamejificha.

Kwa miaka 10 ijayo iwapoKenya itakuwa na viongozi hawa ni wazi kuwa uwekazaji mkubwa na biashara vitapunguasana, biashara ya watalii, makampuni ya mafuta na gesi, viwanda na biasharakimbilio lao litakuwa Tanzania. Kwa hivi sasa, Uganda, Rwanda na Burundihazitoi fursa bora kiuchumi, kiutawala na kisiasa ukilinganisha na Tanzania.

Ni vema Wizara na Taasisi nyinginehusika zikafanya tathmini ya kina kuona kinachoendelea sasa Nchini Kenyakinatoa fursa gani kiuchumi kwa Tanzania. Tuzitumie fursa hizi ili kuujengauchumi wetu ambao umekuwa ukiporomoka mfululizo kwa karibu miaka 10 sasa.

Wizaraya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iwe mstari wa mbele katika hili.
Wakati tukiwapa ndugu zetu wa Kenya hongerakwa kukamilisha uchaguzi, tuwape pole kwa makovu yaliyojitokeza na tuzitumiefursa zinazotokana na kinachoendelea huko kwao. Hii si roho mbaya, ndio Duniainavyoenda hivi sasa.
 
Well said but i dont think this parochial government and its obsolete hypocrites will make any move towards economic progress rather than driving our country to the moribund.
 
Rais ameliabisha taifa kwa kumpongeza Uhuru Kenyatta kwa haraka.Hii ni Undiplomatic-diploamcy.Inaonekana Tanzania hatujajifunza ya mwaka 1970 pale Mwalimu Nyerere alipolitambua taifa la BIAFRA likiongozwa na Jenearali ojukwu walipojitenga kutoka Nigeria lakini wakashindwa vita.Ilikua diplomatic embarrasement.kama pongezi alizotoa alisema kwa niaba ya Watanzania basi naomba isomeke hivi'Kwa niaba ya watanzania isipokua Ben wa Saanane'.I don't want to be part of this shame,I value intergrity.Inajulikana Kenya imefanya judiaciary system reform(mageuzi ya mfumo wa mahakama) kupitia katiba mpya ili kuzuia machafuko kama ya yale ya mwaka 2007.Imeruhusiwa matokeo ya urais kupingwa mahakamani.Raila Odinga amepinga matokeo hayo mahakamani kwa kile alichokiita ‘Massive irregularity' yaani Udanganyifu wa kupindukia katika matokeo hayo.Amechagua njia sahihi na ya kistaarabu .Hiyo ni dispute kama ile ya Laurent Gbagabo na Allasaine Outtara kule Cote D'Ivore ila tofauti ni njia za kutatua tu

Nilitegemea waziri wa mambo ya nje ataitumia taaluma yake ya diploamsia vizuri kuchukua pre-caution kwenye matamshi ya Rais kikwete na kumshauri professionally.Koffi Anan (mwanadiplomasia nguli)aliyeshirikiana na Rais kikwete amewapaongeza wakenya kwa kufanya uchaguzi kwa Amani,Mataifa yaliyoendelea na viongozi wanaojali intergrity wamewapongeza wananchi wa Kenya bila kumtaja Uhuru Kenyatta ambaye ushindi wake umepingwa mahakamani .Pia nilitarajia rais ajiulize ikiwa Mahakama zitaamua na kutengua ushindi wa Uhuru itakuaje?Maana hata mwaka 2000 uchaguzi wa marekani Al Gore alikua mshindi ila mahakama ikaaamuru kura za Florida zihesabiwe Upya halafu George bush akaibuka Mshindi baaada ya hapo.
Ni vyema tujiulize iwapo Uhuru baada ya kuchaguliwa akishindwa ku-cooperate na mahakama ya kimataifa itakuaje maana Kenya itawekewa sanction.Nilitegemea miaka 10 ya Rais Kikwete kuwa waziri wa mambo ya nje na sasa ni rais kwa miaka 7 angekua ame-improve diplomatic skills kwenye majukwa ya kimataifa.Lawama hizi pia nazielekeza kwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe(msomi mzuri kwenye diplomasia na ninamuheshimu) kwa kushindwa kuzuia hii aibu,Mbona aliweza kuzuia hii aibu kuhusu kuitambua serikali ya mpito ya Libya hata baada ya waasi kupandisha bendera?Samwel Sitta waziri wa jumuiya ya afrika Mashariki has failed ih his capacity

Nilitarajia kwa kiongozi yeyote anayejali intergrity angewapongeza wananchi wa Kenya kwa mchakato huu wa uchaguzi na kusubiri mahakama itoe uamuzi kuhusu uhalali wa uhuru Kenyatta kuwa Rais.Viongozi wengine kama Museveni(huyu anajulikana kwa kuropoka maana hata uchaguzi uliopita Kenya alikua wa kwanza kumtambua mwizi wa kura) na Jacob Zuma walichofanya ni kuonyesha taswira halisi ya viongozi wa Afrika wasivyo makini.Haipendezi kuona Rais kikwete akiungana na viongozi walioshindwa katika fraternity ya demokrasia kama Museveni kukurupuka na kutoa pongezi.
 
Kwa niaba ya wananchi na wakaazi wote wa Magomeni tunakupa pongezi za dhati President elected Uhuru Kenyata kwa ushindi wako.Mungu akupe maisha marefu na busara katika utawala wako.Ameen Chadomo Bonge la povu.Namsubiri Dj na mjaluo mwenzake kauli zao
 
narrow minded.
 
uhuruk.jpg

Hongera Uhuru Kenyatta!
 
Nchi haiendeshwi kama bavicha...
 
Back
Top Bottom