prince john john
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 2,328
- 3,726
Wapendwa Taifa la Mungu, Mafrateri hawa (pichani chini ) walitekwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walipovamia Seminari kuu ya Mchungaji Mwema (Good Shepherd Seminary) iliyopo Kaduna huko Nigeria usiku wa tarehe 08 Januari 2020.
Tangu kutekwa kwao, watekaji wamekuwa wakiwasiliana na wazazi pamoja na seminari wanakosoma mafrateri hawa kwa njia mbalimbali wakitaka wawalipe pesa ili wawaachie huru la sivyo watawaua.
Waliotekwa ni Frt. Pius Kanwai, Frt. Peter Umenukor, Frt. Stephen Amos na Frt. Michael Nnadi, wote wakiwa ni Mafrateri wa Mwaka wa kwanza wa Masomo ya Falsafa katika seminari hiyo yenye jumla ya waseminari 268.
Juzi Tarehe 18 Januari 2020, siku ya jumamosi, watekaji hao walimtelekeza mmoja wa mafrateri hawa kwenye barabara kuu ya Kaduna - Abuja, baada ya kuhisi atakufa akiwa mikononi mwao kutokana na maheraha makubwa aliyokuwa nayo yaliyotokana na mateso na kipigo. Wasamaria wema walimwokota frateri huyo na sasa anaendelea kupokea matibabu hospitalini japo hali yake sio ya kuridhisha sana.
Tunawaalika tuendelee kuwaombea mafrateri watatu ambao bado wameshikiliwa na watekaji hao ili waweze kupatikana wakiwa salama. Pia tuombe ulinzi wa Mungu kwa kanisa la Nigeria, na Kanisa lote ulimwenguni pamoja na taasisi zake zote zikiwepo seminari wanakolelewa wahudumu wa Kanisa.
Tafadhali sali angalau Baba yetu, Salamu Maria na Atukuzwe Baba kwa nia ya kuomba kupatikana kwa Mafrateri hawa.
Mwenyeheri Alamano Tansi - Utuombee.
Bikira Maria Malkia wa Mitume - Utuombee!
Sent using Jamii Forums mobile app