MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Mmarekani aitwaye George Carlin once said, "I'm completely in favour of the separation of Church and State. My idea is that these two institutions screw us up enough on their own, so both of them together is certain death."
Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania kusikia vyama vyote vya siasa kwa pamoja vikihubiri Mabadiliko kama vitachaguliwa katika uchaguzi mkuu 2015. Hii inaonyesha wananchi wengi walikuwa wanataka mabadiliko bora.
Uchaguzi umemalizika na Watanzania wengi wamemchagua Dk. Magufuli kuwa Rais wa Tanzania. Huyu ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa Mabadiliko hata kama unapenda au hupendi.
Mabadiliko ninayotaka kuyaona kwa sasa ni kuhakikisha viongozi wa dini wanaojiingiza kwenye siasa za kishabiki wanapigwa vita kwa nguvu zote. Kiongozi kujiingiza kwenye ushabiki wa kisiasa ni kuwagawa waumini wake na pia kuligawa taifa.
Hutuwezi kuwa Taifa endelevu kama kuna viongozi wa kisiasa au baadhi ya vyama vitakuwa vikiendesha siasa kwa matakwa ya baadhi ya viongozi wakuu wa dini. Kuchanganya Siasa na dini kwenye taifa lenye wananchi wengi wenye imani za dini tofauti ni kama kuchezea moto kwenye mafuta ya petroli.
Tumewaona viongozi wa dini kama Sheikh Rajab Katimba, Askofu Josephat Gwajima na Askofu Zachary Kakobe wakijiingiza kwenye ushabiki wa kisiasa kwa kutanguliza ubinafsi bila kuangalia madhara kwa waumini wao achilia mbali taifa letu. Tumeyaona matendo yao na kuzisikia kauli zao za kishabiki. Kwa kujiingiza kwenye ushabiki wa kisiasa wamewagawa kifikra na kimtazamo wafuasi wao na watanzania kwa ujumla. Mbaya zaidi, wamewalazimisha kimantiki wafuasi wao wakubaliane na matakwa yao yaliyojengeka katika msingi wa ubinafsi.
Kama hakutakuwa na Mabadiliko ya kupiga vita aina ya viongozi kama hawa, taifa litakuwa linajichimbia kaburi. This is a recipe for disaster.
Amani, Umoja na Upendo havinunuliwi bali vinajengwa kwa gharama kubwa lakini pia vinabomolewa kwa gharama ndogo kama inayofanywa na baadhi ya viongozi wa dini wa aina ya Sheikh Rajab Katimba, Askofu Josephat Gwajima na Askofu Zachary Kakobe.
Tusiruhusu religious belief kuwa political identity nchini. Tusiruhusu viongozi wakuu wa madhehebu ya dini kuwa political identity nchini. Chama cha siasa lazima kiwe cha wananchi wote bila kujali imani zao za dini. Viongozi wa kisiasa lazima wawe ni viongozi wa wananchi wote. Makanisa na Misikiti isiwe ni sehemu ya kueneza itikadi za vyama. Taifa letu liwe zaidi ya nafsi na ubinafsi wetu.
Tuendelee kuwakataa viongozi wa dini wa aina hii na wanasiasa wao wanaowatumia viongozi wa aina hii kama tulivyofanya kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.
Haya ndiyo mabadiliko bora ninayotumaini kuyapata katika utawala wa Rais Magufuli.
Bendera za vyama mpaka kwenye nyumba za ibada! tuzikatae siasa za aina hii.
Baadhi ya Viongozi wa dini, wakiwa katika mkutano mkuu wa Chadema jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Sheikh Rajab Katimba, Askofu Josephat Gwajima (wa pili kulia) na Askofu Zachary Kakobe.