Inaonekana bado hujapata mtoto/watoto wako mwenyewe, vipi kuhusu wadogo zako kwa wazazi wenu, hujawaona kufanya hivi? Mwenyezi Mungu akujaalie kizazi (watoto) walio wema, inshaAllah. Haya ni ya kawaida mtoto kucheza namna hii wakati mzazi/wazazi wamo ndani ya sala.
Hassan na Hussein, wajukuu wa Mtume Muhammad walimfanyia hivi babu yao, Mtume Muhammad, SallaLLaahu alayhi wasallam wakati anafanya ibada ya sala, na kutokana na hapo ndipo waislamu wamepata mafundisho kadhaa kuhusiana na:
- Ustahamilivu na uvumilivu kwa watoto wadogo
- Uhalali wa kurefusha, kuchelewesha vitendo vya sala bila ya kuharibu sala, huku wakati huo huo kuepuka kumdhuru mtoto wakati anacheza-jifunza ibada hii muhimu. Kumbuka kwamba mtoto hafanyi hivi kwa makusudi ya kuharibu sala ya mzazi wake wala hajui undani wa jambo analolifanya, hapo hapo akiona jambo jengine tu, huacha hivi akafuata lile na mara hurudi tena, mara huondoka tena, mara kaka au baba yake kaingia atawafuata hao, na mara atarudi tena. Anacheza
- Ni katika kile kipindi kimojawapo muhimu cha maisha yao yaliyo safi (yasiyo na dhambi) takriban 1-7 years. Watoto hufanya kwa pamoja, hivi (utoto) na vile vile wakati huo huo huona na huiga vitendo muhimu kuhusiana na ibada ya sala.
Ni sawa tu kwa upande mwengine na vile kumuacha mtoto ajifunze ufuska wa leo katika runinga zetu, huona na huiga vile vile bila ya kujua anafanya nini, kumbe ndio tabia na desturi zake hujengeka hivyo hivyo.
Bora hivi kuliko runinga na vipindi vya siku hizi, au afadhali kwamba mtoto hupata muda kidogo kupuuza runinga na kucheza-jifunza mambo yenye maana kama ibada