Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,495
- 38,333
Heshima wanajamvi,
Jana nilikwenda kituo cha afya kupima damu baada ya kuhisi naumwa wakati nasubiri kupimwa kaingia Ustadhi na vijana wawili mmoja mwanaume na wapili mwanamke kajifunika mwili mzima hata uso hauonekani.Wote wakajiunga katika foleni ya kupima damu.Baada ya muda kidogo (5 minutes) Ustadhi alieandamana na vijana wake wawili akaanza kufunguka unajua siku hizi UKIMWI si suala la kulifanyia ajizi vijana wakitaka kufunga ndoa nawaleta mimi mwenyewe kupima.
Bado niko katika foleni nasubiri zamu yangu ifike namwangalia kijana (mume mtarajiwa) jasho linamtoka anajigeuza geuza kwenye kiti utadhani ana majipu kunako makalio anatoka nje anajinyosha kama Paka alitoka usingizini msichana wa watu kajikalia tuli hana wasiwasi hata kidogo anaoneka anajiamini.Muda wangu wa kupima unafika naondoka sijui kilichoendelea.
Nampongeza Ustadhi kazi anayoifanya ni njema ila nadhani hana utaalamu / wataalamu wa kuwaandaa vijana kwaajili ya zoezi la upimaji.
Kupima UKIMWI kunataka Moyo.