Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza kufikiria kilichotokea Zambia kinaweza kutokea Tanzania. Watu wengi wanasahau kuwa kilichotokea Zambia siyo sawa na kinachotokea Tanzania. Chama kilichoshinda Zambia safari hii siyo miongoni mwa vyama vya awali vya upinzani. Kumbuka kuwa MMD (kilichoondolewa madarakani) tunaweza kukilinganisha kabisa na CDM au CUF kwani vyote vilianzishwa kama majibu ya kukiondoa chama tawala madarakani. MMD chini ya Chiluba kiliweza kuondoa chama tawala cha Kaunda.
Hivyo mlingano hapa ni kuwa MMD ni sawa na CDM kwani vyote viliongozwa na msingi wa sera za kuondoa chama tawala madarakani. Sata alikuwa ni sehemu hiyo ya MMD lakini baadaye alijimegua.
Sata alianzisha chama nje ya vyama vile vya upinzani vikongwe na sera zake zilikuwa ni kuwakumbusha Wazambia wao ni nani na wametoka wapi na kwanini ni katika past yao ndiko yalipo mafuta ya kuchochea their future. Tukifananisha basi utaona chama cha Sata ni sawa zaidi na kuanzishwa kwa CCJ! Chama cha Sata cha Patriotic Front kilikuwa kimejengwa katika nadharia ya kuwa Wazambia kwanza - siyo wawekezaji!
CDM ya Tanzania bado inasafari ndefu kwani ukiangalia kwa haraka (Kobello humu aliwahi kuhoji sana hili) ni kuwa ni chama chenye mrengo wa kibepari zaidi na kinaogopa (kwa kutaka au kwa bahati mbaya) kuonekana kina mrengo au hisia za ujamaa au kurudia misingi ya Taifa. Lakini tunaona ni jinsi gani katika uchaguzi uliopita kiliweza kufanya vizuri zaidi kikiwa na ujumbe wa uzalendo kwanza, misingi ya taifa - usawa, utu, na kutumia raslimali zetu kuwanufaisha watu wengi zaidi. Sera hizi - japo ni za kwenye manifesto zaidi kuliko za itikadi ya chama ndizo ambazo zimewavuta watu wengi kuikubali CDM lakini bado haijakumbatia hasa hisia hizi.
Matokeo yake ni kuwa yawezekana kabisa kuibuka kwa chama kingine chenye mrengo wa kipatriotic zaidi na ambacho hakioni haya kujitambulisha na past yake kunaweza kusababisha kweli CCM ije kung'olewa madarakani.
Kwa hali ilivyo sasa nchini Dots haziunganiki.