Tuunganishe dots Mwanakijiji et al - kwanini Upinzani umeshinda Zambia, Tanzania je..

Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza kufikiria kilichotokea Zambia kinaweza kutokea Tanzania. Watu wengi wanasahau kuwa kilichotokea Zambia siyo sawa na kinachotokea Tanzania. Chama kilichoshinda Zambia safari hii siyo miongoni mwa vyama vya awali vya upinzani. Kumbuka kuwa MMD (kilichoondolewa madarakani) tunaweza kukilinganisha kabisa na CDM au CUF kwani vyote vilianzishwa kama majibu ya kukiondoa chama tawala madarakani. MMD chini ya Chiluba kiliweza kuondoa chama tawala cha Kaunda.

Hivyo mlingano hapa ni kuwa MMD ni sawa na CDM kwani vyote viliongozwa na msingi wa sera za kuondoa chama tawala madarakani. Sata alikuwa ni sehemu hiyo ya MMD lakini baadaye alijimegua.

Sata alianzisha chama nje ya vyama vile vya upinzani vikongwe na sera zake zilikuwa ni kuwakumbusha Wazambia wao ni nani na wametoka wapi na kwanini ni katika past yao ndiko yalipo mafuta ya kuchochea their future. Tukifananisha basi utaona chama cha Sata ni sawa zaidi na kuanzishwa kwa CCJ! Chama cha Sata cha Patriotic Front kilikuwa kimejengwa katika nadharia ya kuwa Wazambia kwanza - siyo wawekezaji!

CDM ya Tanzania bado inasafari ndefu kwani ukiangalia kwa haraka (Kobello humu aliwahi kuhoji sana hili) ni kuwa ni chama chenye mrengo wa kibepari zaidi na kinaogopa (kwa kutaka au kwa bahati mbaya) kuonekana kina mrengo au hisia za ujamaa au kurudia misingi ya Taifa. Lakini tunaona ni jinsi gani katika uchaguzi uliopita kiliweza kufanya vizuri zaidi kikiwa na ujumbe wa uzalendo kwanza, misingi ya taifa - usawa, utu, na kutumia raslimali zetu kuwanufaisha watu wengi zaidi. Sera hizi - japo ni za kwenye manifesto zaidi kuliko za itikadi ya chama ndizo ambazo zimewavuta watu wengi kuikubali CDM lakini bado haijakumbatia hasa hisia hizi.

Matokeo yake ni kuwa yawezekana kabisa kuibuka kwa chama kingine chenye mrengo wa kipatriotic zaidi na ambacho hakioni haya kujitambulisha na past yake kunaweza kusababisha kweli CCM ije kung'olewa madarakani.

Kwa hali ilivyo sasa nchini Dots haziunganiki.
 
hasa nimesikitika CDM nzima kuhamia igunga huku kukiwa na mengi ya kusemea na kufanya.wanaamini wanao wakati! Kuna vichwa vingi tu nchi nzima ingewaka moto.after igunga tunatafutiwa na ccm parapanda jingine!
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza kufikiria kilichotokea Zambia kinaweza kutokea Tanzania. Watu wengi wanasahau kuwa kilichotokea Zambia siyo sawa na kinachotokea Tanzania. Chama kilichoshinda Zambia safari hii siyo miongoni mwa vyama vya awali vya upinzani. Kumbuka kuwa MMD (kilichoondolewa madarakani) tunaweza kukilinganisha kabisa na CDM au CUF kwani vyote vilianzishwa kama majibu ya kukiondoa chama tawala madarakani. MMD chini ya Chiluba kiliweza kuondoa chama tawala cha Kaunda.

Hivyo mlingano hapa ni kuwa MMD ni sawa na CDM kwani vyote viliongozwa na msingi wa sera za kuondoa chama tawala madarakani. Sata alikuwa ni sehemu hiyo ya MMD lakini baadaye alijimegua.

Sata alianzisha chama nje ya vyama vile vya upinzani vikongwe na sera zake zilikuwa ni kuwakumbusha Wazambia wao ni nani na wametoka wapi na kwanini ni katika past yao ndiko yalipo mafuta ya kuchochea their future. Tukifananisha basi utaona chama cha Sata ni sawa zaidi na kuanzishwa kwa CCJ! Chama cha Sata cha Patriotic Front kilikuwa kimejengwa katika nadharia ya kuwa Wazambia kwanza - siyo wawekezaji!

CDM ya Tanzania bado inasafari ndefu kwani ukiangalia kwa haraka (Kobello humu aliwahi kuhoji sana hili) ni kuwa ni chama chenye mrengo wa kibepari zaidi na kinaogopa (kwa kutaka au kwa bahati mbaya) kuonekana kina mrengo au hisia za ujamaa au kurudia misingi ya Taifa. Lakini tunaona ni jinsi gani katika uchaguzi uliopita kiliweza kufanya vizuri zaidi kikiwa na ujumbe wa uzalendo kwanza, misingi ya taifa - usawa, utu, na kutumia raslimali zetu kuwanufaisha watu wengi zaidi. Sera hizi - japo ni za kwenye manifesto zaidi kuliko za itikadi ya chama ndizo ambazo zimewavuta watu wengi kuikubali CDM lakini bado haijakumbatia hasa hisia hizi.

Matokeo yake ni kuwa yawezekana kabisa kuibuka kwa chama kingine chenye mrengo wa kipatriotic zaidi na ambacho hakioni haya kujitambulisha na past yake kunaweza kusababisha kweli CCM ije kung'olewa madarakani.

Kwa hali ilivyo sasa nchini Dots haziunganiki.

Ongezea pia pamoja na ubepari kinaongelea serikali ya MAJIMBO kwenye manifesto yao..

Ubepari na U-majimbo ni sera ambazo hawana uwezo wa kuitamka na kuitetea hadharani japo zipo kwenye manifesto kwanini..hawajui wanataka nini?

Walichofanya si kwamba walipata kura baada ya kuonyesha sera za ki-zalendo big NO

The big boost comes from waraka ..na udini ambao kwa bahati mbaya uliwafaidisha kwa muda mfupindio maana hawakuukemea

lakini pia ndio utakaowaangamiza
 
Maishamapya!

Nimeikubali tathmini yako, kweli umefanya tafakuli za kina. Yaani ulivyoweka hayo mambo ya msingi ili tuendelee katika awamo zote (watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora)...kweli kabisa uko sahihi.

Thanks for that!
 
Tatizo waislam hawana msimamo mara waunge mkono CUF kagombea kikwete tukahamia ccm baada ya kudanganywa pipi ya kadhi,sasa tunarudi tena cuf!pia kura za kina mama huwa hazieleweki wakitishwa juu ya amani na ccm basi hugeukia ccm!
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza kufikiria kilichotokea Zambia kinaweza kutokea Tanzania. Watu wengi wanasahau kuwa kilichotokea Zambia siyo sawa na kinachotokea Tanzania. Chama kilichoshinda Zambia safari hii siyo miongoni mwa vyama vya awali vya upinzani. Kumbuka kuwa MMD (kilichoondolewa madarakani) tunaweza kukilinganisha kabisa na CDM au CUF kwani vyote vilianzishwa kama majibu ya kukiondoa chama tawala madarakani. MMD chini ya Chiluba kiliweza kuondoa chama tawala cha Kaunda.

Hivyo mlingano hapa ni kuwa MMD ni sawa na CDM kwani vyote viliongozwa na msingi wa sera za kuondoa chama tawala madarakani. Sata alikuwa ni sehemu hiyo ya MMD lakini baadaye alijimegua.

Sata alianzisha chama nje ya vyama vile vya upinzani vikongwe na sera zake zilikuwa ni kuwakumbusha Wazambia wao ni nani na wametoka wapi na kwanini ni katika past yao ndiko yalipo mafuta ya kuchochea their future. Tukifananisha basi utaona chama cha Sata ni sawa zaidi na kuanzishwa kwa CCJ! Chama cha Sata cha Patriotic Front kilikuwa kimejengwa katika nadharia ya kuwa Wazambia kwanza - siyo wawekezaji!

CDM ya Tanzania bado inasafari ndefu kwani ukiangalia kwa haraka (Kobello humu aliwahi kuhoji sana hili) ni kuwa ni chama chenye mrengo wa kibepari zaidi na kinaogopa (kwa kutaka au kwa bahati mbaya) kuonekana kina mrengo au hisia za ujamaa au kurudia misingi ya Taifa. Lakini tunaona ni jinsi gani katika uchaguzi uliopita kiliweza kufanya vizuri zaidi kikiwa na ujumbe wa uzalendo kwanza, misingi ya taifa - usawa, utu, na kutumia raslimali zetu kuwanufaisha watu wengi zaidi. Sera hizi - japo ni za kwenye manifesto zaidi kuliko za itikadi ya chama ndizo ambazo zimewavuta watu wengi kuikubali CDM lakini bado haijakumbatia hasa hisia hizi.

Matokeo yake ni kuwa yawezekana kabisa kuibuka kwa chama kingine chenye mrengo wa kipatriotic zaidi na ambacho hakioni haya kujitambulisha na past yake kunaweza kusababisha kweli CCM ije kung'olewa madarakani.

Kwa hali ilivyo sasa nchini Dots haziunganiki.

Uzuri wako mara moja moja huwa unakubali kuonyesha rangi zako kamili na kuweka uzalendo mbele, kilichotokea Zambia ni chama cha upinzani kutolewa na chama cha upinzani kilicho zaliwa ndani ya upinzani, CCJ ilizaliwa ndani ya chama tawala na walikuja kichwa kichwa kilichofuata unakijua vizuri.

Na mwishoni mwa mchango wako umekubali kwamba ni ndoto kwa vyama vya upinzani kuchukua mikoba ya kuendeleza nchi yetu.

Jaribu kujiuza ikitokea chama chochote cha upinzani kuchukua nchi Tanzania kitadumu kwa miaka 20 kama Zambia?..
 
Maishamapya!

Nimeikubali tathmini yako, kweli umefanya tafakuli za kina. Yaani ulivyoweka hayo mambo ya msingi ili tuendelee katika awamo zote (watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora)...kweli kabisa uko sahihi.

Thanks for that!

Asante SaidAlly! Naamini umeiona pia makala ya Mwanakijiji - Kwa kifupi sote tunakubaliana kuwa hakuna dots za kuunganisha japo hoja zetu za kusupport ziko tofauti. Hata hivyo ukweli unabaki kuwa ni watu ndio watakaoleta mabadiliko iwe kwa kupitia chama kingine kipya chenye mrengo wa patriotic kama anavyosema MKJJ, au kupitia chama cha upinzani kilichopo sasa au kwa nguvu ya watu. Bado naamini Mabadiliko makubwa yanakuja ONLY ikiwa WATU (wananchi) wataamua. CHADEMA inafanya kazi kubwa sana ya kuwafungua watu na kuwafanya wajue kuwa hatima ya nchi iko mikononi mwao na si mikononi mwa watawala. Watawala wanawekwa na kutolewa na watu.
 
Tatizo waislam hawana msimamo mara waunge mkono CUF kagombea kikwete tukahamia ccm baada ya kudanganywa pipi ya kadhi,sasa tunarudi tena cuf!pia kura za kina mama huwa hazieleweki wakitishwa juu ya amani na ccm basi hugeukia ccm!
2010 tulipiga kura maslahi..kwakuwa wakristo na waraka wao walishaegemea kule kwa padre

Siyo kwamba hawana msimamo...ni kuangalia lesser evil..which I think is a good move..
 
Sata ktk ilani za chama chake alisema ataiongoza nchi kwa misingi ya Kikristu na asilimia zaidi ya 90 ya Wazambia ni wakristu. Akawaahidi antafukuza Wachina na Wahindi wote wenye imani za shetani. Hivyo kwa umaskini wao bora wamrudie Mungu na watamwamini mcha Mungu zaidi ya vibaraka wengine. Zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa Tanzania!
 
ni ngumu kuelewa watz tuna nini vichwani mwetu hadi tuwe wazito wa mabadiliko namna hii, nw niko kijiji kimoja huku Iringa yani shida tupu,. watu ni kama wamelishwa limbwata na kijani,daaah,..ukimuuliza mtu unadhani ni nini kinapelekea watu kwenye kijiji hiki kuishi kwa tabu namna hii ilihali ni sehemu ambayo kuna uzalishaji mkubwa mno wa chakula, ardhi ni yenye rutuba pasipo mfano..jibu unalopata ni Baba we acha tu,. Ukiuliza sasa vipi kura yako uliitumia vyema??? Jibu unalopewa ni kuwa baba huoni nguo hizi (kanga na vilemba vya kijani na njano), ningekuwa nimevaa nini saa hizi na hili baridi!!! kwa kweli haya ndiyo mavazi yaliyotawala huku,utadhani ni sare za shule kwa kila mwanakijiji,...

Piteni na huku kina Zitto,Mnyika Lipumba na wengine wenye kuweza kusema mkasikilizwa...wanaangamia hawa pasipo hatia kwenye ardhi yao wenyewe,inatia sana huruma,.. Nashindwa kuamini kuwa hatia ni kura yao, bali hawa hawajapata nafasi ya kusikia altenatives ya maisha magumu wanayoishi.. Nawaomba mzingatie hili..VIJIJINI BADO.

Hao cha mdori, wananchi wa Igunga hasa maeneo ya vijijini kwenye matatizo kibao wanaoishi nyumba za full suti, walihojiwa 'ikiwa uchaguzi utafanyika leo utamchagua nani?. Wengi walijibu ccm. Swali la pili kwanini? Hiki chama tumekizoe wengine, hivyo vyama vingine hatuvijui na wengine ccm imetukuza. Hebu angalia majibu kama haya, kiukweli vyama vingine vya siasa havinabudi kutoa elimu ya urai, ili watu kama hawa wajitambue.
 
Sata ktk ilani za chama chake alisema ataiongoza nchi kwa misingi ya Kikristu na asilimia zaidi ya 90 ya Wazambia ni wakristu. Akawaahidi antafukuza Wachina na Wahindi wote wenye imani za shetani. Hivyo kwa umaskini wao bora wamrudie Mungu na watamwamini mcha Mungu zaidi ya vibaraka wengine. Zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa Tanzania!

Kumbe mdini sana huyo..i am out
 
Zambia sasa inafuata amri Kumi za Mungu, KATIBA ya nchi pembeni, hii haiwezi tokea kule kwetu.

Kwa sasa tunamalizia mchakato wa mahakama ya kadhi itakayo fadhiliwa na serikali...we aint got no dots to connect.
 
Uzuri wako mara moja moja huwa unakubali kuonyesha rangi zako kamili na kuweka uzalendo mbele, kilichotokea Zambia ni chama cha upinzani kutolewa na chama cha upinzani kilicho zaliwa ndani ya upinzani, CCJ ilizaliwa ndani ya chama tawala na walikuja kichwa kichwa kilichofuata unakijua vizuri.

Hakuna chama cha upinzani kinachotawala. Chama chochote kikishashika madaraka hakiwi tena cha upinzani! Unavyosema ni kana kwamba chama cha Kaunda kilipotolewa madarakani kilibakia kuwa "chama tawala" nje ya madaraka. Ni mawazo haya yanaweza kukufanya kuwa CCM ikitolewa madarakani basi itakuwa ni chama tawala kilicho nje ya madaraka ni kile cha upinzani kinachoshika nchi bado kinabakia kuwa upinzani. Sijui kama mantiki yako ina mantiki. Aliyeachika hawi kaolewa hadi aolewe tena. Huwezi kusema umeachika halafu ukajiita bado mke au mume.

Na mwishoni mwa mchango wako umekubali kwamba ni ndoto kwa vyama vya upinzani kuchukua mikoba ya kuendeleza nchi yetu.

On the contrary, ninachosema ni kuwa with the right message, right strategy and right timing upinzani wanaweza kushika nchi kabisa. Naamini nafasi nzuri kabisa ilikuwa ni mwaka jana na hii ikapotea. Siwezi kuona kwa haraka - kama vitu vikibakia vilivyo sasa - kuweza kushika madaraka in the near future. (msisitizo uko kwenye vitu vikibakiaa vilivyo sasa).

Jaribu kujiuza ikitokea chama chochote cha upinzani kuchukua nchi Tanzania kitadumu kwa miaka 20 kama Zambia?..

Si kwa maslahi ya nchi kwa chama chochote kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka ishirini. So.. at most chama chochote kinaweza kushika madaraka for ten years at least, at most miaka 15.. ikifika ishirini kitang'oka tu.. unless of course kina mfumo mzuri sana wa kujisahihisha.
 
Sata ktk ilani za chama chake alisema ataiongoza nchi kwa misingi ya Kikristu na asilimia zaidi ya 90 ya Wazambia ni wakristu. Akawaahidi antafukuza Wachina na Wahindi wote wenye imani za shetani. Hivyo kwa umaskini wao bora wamrudie Mungu na watamwamini mcha Mungu zaidi ya vibaraka wengine. Zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa Tanzania!

Mimi ni mkristo na mmojawapo wa viongozi; hata hivyo siungi mkono mrengo wa Sata - kama haya uliyoyaandika ni kweli. Naamini katika serikali huru inayosimamia utawala wa sheria ambazo watu wake wamekubaliana na hizi ziko kwenye KATIBA ya nchi.
 
Sata ktk ilani za chama chake alisema ataiongoza nchi kwa misingi ya Kikristu na asilimia zaidi ya 90 ya Wazambia ni wakristu. Akawaahidi antafukuza Wachina na Wahindi wote wenye imani za shetani. Hivyo kwa umaskini wao bora wamrudie Mungu na watamwamini mcha Mungu zaidi ya vibaraka wengine. Zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa Tanzania!

thats true na hilo watu wanaweza wasiliielewe sana. Alichofanya Sata ni kuwaunganisha watu kwa msingi wa kile kinachowaunganisha zaidi kuliko kile kinachowatenganisha. Kwamba Ukristu unawaunganisha zaidi - hata katika tofauti zao - ni rahisi wao kuwa pamoja. Lakini swali ni kuwa hivyo vyama vingine navyo vilikuwa na wakristu wengi vile vile sasa kwanini ni chama cha Sata?

Hili tuliliangaliia kwenye ile mada nyingine na kutolea mifano kama ya Misri, Syria na Iran ambako Waislamu ni zaidi ya 99 percent lakini kuna vyama tofauti. Na utaona ni vile ambavyo vinakuwa vikali katika masuala ya imani vinavyovutia zaidi - Muslim Brotherhood in case of Misr. Kwanini.

Ila ni kweli kwamba kwa kutumia dini hakuna chama Tanzania ambacho kinaweza kushika madaraka ya nchi. Kumbe katika Tanzania hatuwezi kujenga nchi kwa kutumia dini kama wanavyojaribu Zambia au Misri au Iran au hata Saudia kwenyewe. Swali ni kitu gani kinachotuunganisha zaidi sisi Watanzania katika tofauti zetu za dini, rangi, kabila na hata hadhi? Chama ambacho kitapata jibu la swali hili naamini ndicho kitakachokubalika zaidi nchini kwani kitawatenga wale wote wenye kujaribu kutumia dini au tofauti nyingine kuendesha siasa zao.
 
Sasa hapa Mwanakijiji anahusika vp?

Kwa namna ulivyo na vichwa vingi huwezi kuelewa kwani hesabu yahitaji kichwa kimoja kilichotulia. Kubali mapungufu yako, na siku zote Kama hujui style ya kucheza fuatisha mdundo Wa ngoma kubwa mdogo wangu!
 
Mkuu kwa maswali yako hapo juu jibu ni moja tu, ujamaa na kujitegemea - CCM, hapa hakuna dots wala fungua semi.
 
Kwa namna ulivyo na vichwa vingi huwezi kuelewa kwani hesabu yahitaji kichwa kimoja kilichotulia. Kubali mapungufu yako, na siku zote Kama hujui style ya kucheza fuatisha mdundo Wa ngoma kubwa mdogo wangu!
Jina lako haliendan na ulicho comment, Jamaaa mie nimemuelewa nn alikuwa anataka, ingekuwa vyema sana kama angebadilisha heading ya thread yake, kimsingi Content ya Thread yake haiendan na Heading yake, kuna mtu amemshauri ama angem PM MM, au ange post kwenye wall post ya MM,na mie namshauri angebadilisha heading ya Thread yake na kuleta mvuto zaid, jamaa atakuwa amelielewa hilo,hata MM pia nadhan amelielewa hilo,kama wewe hujalielewa hilo, sina haja ya ku argue na wewe coz akili zako zitakuwa zinafikiri the way CCM wanavyofikiri.
Respect
 
Back
Top Bottom