Princemwalejr
JF-Expert Member
- Nov 9, 2017
- 496
- 492
Tuna utitiri wa vyombo vya habari lakini habari nyingi zinazoandikwa ni za siasa, michezo na vibweka vya mastaa.
Utasikia leo huyu kahama chama, huyo kamjibu raisi vile, msanii huyu kazaa na yule nk. Ndio habari za mjini. Ingekuwa jambo la maana vyombo vya habari vikatumika kutafuta na kuchunguza habari zenye manufaa kwa taifa.
Magari yalikaa bandarini tokea mwaka 2015. Ingekuwa vipi SHILAWADU wangesema
“ebwanaeee kule bandarini leo tumepata ubuyu babu kubwa. Kuna magari yako juu ya mawe muda mrefu kweeeeeli. Tokea mwaka 2015 mwenyewe hajatokea. Yaani noooma kweli”.
Ingekuwa vipi ikitoka kwenye Luninga kuwa Muhimbili ukimkosa daktari ijumaa msubiri jumatatu na ukishindwa kulipia matibabu na huna bima basi tena ndio imeshindikana kukutibu.
Humo kwenye mikasi wangekuwa wanahojiwa wakurugenzi, mawaziri, madaktari nk ili watoe ripoti za mashirika na idara zao badala ya kuwahoji wasanii tu ambao kwa kweli wengine ni wapuuzi tu.
Ni vipi gazeti moja lingeleta udaku kuwa asilimia zaidi ya 60 ya watanzania hawana bima ya afya?
Ingekuwaje magazeti yangekuwa yanatoa data za ukimwi kila wiki, ugoni ungezidi au ungepungua?
Mnaonaje wale wanaotembelea mastaa usiku wangekuwa wanazuka airport na vikamera vyao kupiga picha ulaji wa rushwa na mizigo isiyolipiwa.
Mambo ni mengi yanayowagusa wananchi na kero zao lakini hayapewi nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kama inavyofanyika kwenye habari za siasa na udaku.
Watoto wetu leo wanasikiliza kipindi cha mbuga zetu? Wanaujua ule mwimbo wa “mbuga zetu za Tanzania zina wanyama wengi .............
Tubadilike!