Tutoe hapa "Uongozi Kama imani na utulete kwenye uongozi Kama dira!"

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,215
56,855
Sikufundishi kazi ila kinachokutafuna ni kile kilichopandwa huko nyuma!, simlaumu mtu ila nitalaumu kama atashindwa kuwa muelewa!.

Nafikiri utakumbuka nyanda za juu walivyokujazia wanafunzi barabarani!,sio kwamba wanafunzi sio watu ni watu ila uliwajengea madarasa ili watulie huko,hivyo muda huo walipaswa wawe madarasani na waliotakiwa wawe barabarani hawakuwepo!

Walimuamini sana, kwasababu aliwaaminisha.

Ukishindwa kufata hiyo imani watakupinga nafikiri unaona na unatambua ni kawaida hilo katika nafasi uliyopo. Tukumbushane kitu kimoja Kuna matabaka matatu ya watu,na matabaka haya hubaguliwa kwa uweza wa akili zao!
Wa Kwanza upo nao hukohuko.

Wapili umechanganyika nao hawa nusu huutambua ukweli na nusu hawautambui,wakicheza vibaya huwa wanashuka na wakicheza vizuri huwa wanapanda! Nimeandika hutegemea akili zao.

Watatu huku tulitoka sote na hawa ndio wengi zaidi!,Hawa ndio naoataka kuwaongelea maana kwao huamini kinachowagusa na hawa ndio hutengeneza picha ya chochote unachokijua japo huwa mnawaona tabaka la chini!.

Sasa nini ni nini..?
Vipi ungetaka kuwa wewe..?

Kwakuwa huwezi kwenda na imani sasa tengeneza dira ambayo itakuundia imani!, namaanisha dira ndio itakutengenezea imani na sio imani ukutengenezee dira!.

Wale wakwanza kuna mahali hawataki ukanyage sasa wewe kanyaga!,ila kanyaga bila kufata nyendo zao maana swala sio kukanyaga tu bali kukanyaga kwa usahihi!.

Usitutengenezee imani nawewe bali tutengenezee dira ambayo itatuzalishia imani nawewe!.

Huu sio wakati wa kujaribu ila wakutenda kwani we huoni wivu..?

Ikumbuke asili yako na usiitupe kila uamkapo!.

Kwa hii lugha nyepesi najua umenielewa sana tena zaidi ya sana,
nikutakie wako ujenzi,wenye urefu na mapana
Mimi wako mtenzi,nasononeko japo sio sana!
Nimevaa yako jezi,ila sio ndefu wala pana!..😊
 
Hizi ni enzi za hoja kujibwa kwa hoja sio hoja kujibiwa kwa kupigwa rungu
 
Ukizoea utamaduni kufokewa fokewa utapata tabu sana kwenye utamaduni wa watu wanaozungumza kistaarabu bila kufoka foka.

Ukizoea kuishi kwa propoganda utapata tabu sana propoganda zinapokoma.
 
Back
Top Bottom